Habari zenu, ni muda kidogo umepita ni majukumu ndio yamenizidi. Nina imani tupo pamoja.
Leo kuna kitu muhimu sana ningependa niwaambie au niwakumbushe. MAWASILIANO, mawasiliano ni kitu kizuri sana na muhimu katika mahusiano. Ila kuna watu nadhani hawajui au hawaelewi maana yake, namaanisha kuna wengine MMEZIDISHA!!!! Yaani utakuta kila saa kila wakati unataka kumpigia simu mpenzi wako hauangalii kuwa muda huu labda yupo kazini au kwenye kikao, wewe ni kupiga simu tuuuuu! Na asipopokea ishakuwa shida, au utume sms akichelewa kujibu ishakuwa tabu. Hivi akitumia siku nzima kuongea na wewe tu hizo kazi zitafanyika saa ngapi??
Sasa nakwambia kummiss mtu kuna raha yake, hivi ukiongea nae kwenye simu siku nzima utakuwa hata na hamu ya kumuona jioni akirudi?? Maana yote mtakuwa mshaongea kwenye simu, mkionana mtakuwa na lipi la kuongea? Kama kuna jambo la haraka sawa waweza kumpigia mara moja ukakata simu lakini sio kila dakika wewe unapiga tu simu utadhani mmetongozana jana bwana, yani kila dakika 'i love u' ' i love u too' aaarrrgh badilika!
Kama kawaida mi ndo nishalimwaga limekuuma ................ CHOMA GANZI.