Hii ni kwa wanawake walio kwenye ndoa
Jamani mwanaume anapoamua kukuoa ni kwamba amekupenda na ameridhika na wewe na anakupa dhamana ya familia yake.
Sasa wewe kipindi cha mwanzo wa ndoa mapenzi motomoto baada ya muda kidogo tu basi mapenzi yote yanayeyuka hata vile vitu ulivyokuwa unafanya mwanzoni ambavyo ndo vilimpelekea yeye kukupenda huvifanyi tena, tena wengi wanakuwa na viburi na wabishi sana sasa unategemea nini? Unadhani ataacha kukesha kwenye mabaa au ataacha kutafuta nyumba ndogo? Wakati mwingine wewe mwenyewe unasababisha ndoa kuwa chungu, mpe vile vitu vyote ulivyokuwa unampa mwanzo tena ikiwezekana ongeza mahaba, Ili hata mwanaume akisema katoka nje ujue ni umalaya wake tu.
Kuna wengine yani hata ushiriki wao wa tendo la ndoa ni wa manati na wakishiriki ni kama mambwa yani mwanamke kalala mwanaume karudi zake huko kampandia juu kaingiza mashine kafanya kamaliza kaenda kuoga na mwanamke anaenda kuoga wanalala just like that! no romance! no what.... sasa raha yake hapo ni nini?? Wewe ndo wakumbadilisha mumeo kumbuka mwanaume akishaoa yeye anachofikiria ni kutafuta pesa tu vingine vyote anaamini wife yupo ndo kazi yake kusimamia.
Nadhani mmenielewa, kama vipi CHOMA GANZI
Tuesday, November 20, 2012
Wapenzi kuishi pamoja kabla ya ndoa
Habari,
Kuna kitu ambacho ni muhimu sana leo nahitaji kuwaambia na nimekiona sana tu kwa watu wangu wa karibu.
Kuna tabia ambayo inazidi kushamiri kwenye jamii yetu tofauti na miaka ya nyuma, tabia ya wapenzi wawili kuishi nyumba moja. Si jambo baya kufanya hivyo manake wengi watasema wanataka wajuane kabla hawajajipanga na ndoa ila ni vigezo gani umechukua hadi kufikia uamuzi huo? Mi nadhani kabla ya kukurupuka kufanya hivyo hebu fikiria kwanza, je familia zenu zinaruhusu hivyo?? Unauhakika mnawezana kuishi nyumba moja manake nimeona watu wengi wanafanya hivyo hadi kufikia hatua ya kununua vitu kwa kushare mwisho wa siku wanashindwana ugomvi mwanzo mwisho na hatimaye kuanza kugombea vitu 'hiki nilinunua mimi mara hiki siyo cha kwako' huko ni kujiaibisha kama mnajiamini mnapendana na kuwezana basi fungeni ndoa na kama mnachunguzana basi mchunguzane kwa tahadhari manake mtu hashindwi kuficha makucha kwa kipindi chote ambacho unakaa naye kabla ya ndoa hata kama ikiwa mwaka. Pia dada yangu usidanganyike si kila mwanaume atakaye kwambia mkae wote atakuoa mwingine ndo kwanza anazidi kubweteka, manake ameshaona kuna mwanamke anamfanyia kila kitu kupika kufua kuosha ovyo, unadhani atakaa afikirie ndoa? Hapana, utasikia kila asiku anakwambia ngoja nijipange..... ajipange na nini? kwanini msijipange wote na maisha muanze pamoja? Kuwa makini mwanamke!
Simaanishi usikae naye ila ndo utumie akili sio ubweteke tu mwisho wa siku utajikuta unazalishwa watoto watano bila ndoa wala nini!
Mi nisharopoka hivyo na kama limekuuma CHOMA GANZI,......

Thursday, November 8, 2012
MUME ANASIANA NA HAWARA
Vidole vyangu vimepata nguvu ghafla baada ya kusikia hii habari
'BREAKING NEWS:DAR-ES-SALAAM.kuna mwanamke aliaga kwa mume wake
anaenda tanga kusalimia
kumbe kaenda gusti tandika na mwanaume mwengine
so wakafanya mapenzi
UUME Umenasa Hautoki
Hivi kweli we mwanamke/mwanaume unamuwekea mumeo/mkeo mtego ili akienda nje anasane na huyo mtu?? Sijawahi kuona mapenzi ya namna hii, tena mbaya zaidi unasema huwanasui hadi upewe millioni 5.
Kwanza mwanamke/mwanaume wa namna hii namtafsiri hivi
1. Ana roho mbaya, kiasi cha kwamba haoni vibaya akiona mwenzake akikumbwa na aibu hii
2. Ana tamaa na ndiyo maana katanguliza pesa kwamba bila pesa hawanasui na mtu huyu hashindwi hata kukuua sababu ya pesa
3. Ni mshirikina, kitendo cha kwenda kwa waganga kufanya hayo yote ni ushirikina
4. Hana mapenzi ya kweli kwasababu mtu unayempenda huwezi kutaka kumuwekea mitego itakayomdhalilisha mumewe/mkewe kiasi hicho.
Wakati mwingine kabla hujafanya kitu fikiria mara mbili unaweza ukadhani unamkomoa mtu kumbe unajikomoa mwenyewe, Je, unadhani baada ya kufanya hivyo huyo mwanaume/mwanamke ndo atakupenda? au ndo ataacha umalaya? Hauoni kama unajijengea uadui wewe na mumeo/mkeo? Unadhani baada ya kumnasua atakuacha hivihivi bila kulipa kisasi? Familia yake na watu wake watakuchukulia vipi? Haya ni maswali ambayo ni lazima ujiulize
Wewe kama ni mwanamke/mwanaume wa kweli mtulize mumeo/mkeo kupitia mapenzi mpe yale anayoyafuata nje, na kama umeona kashindikana kuna taratibu zingine ila si kumdhalilisha kiasi hicho. Imefikia kipindi lazima tuwe na ubinaadam je ungefanyiwa wewe hivyo ungefurahi???
Sio kama natetea upande wowote ila nasema ambalo mimi naliona sahihi na ukitaka kunielewa ukiwa kama mwanamke / mwanaume jaribu kufikiria umefanyiwa wewe.
"POLENI SANA KWA WAHUSIKA NADHANI HILO NI FUNDISHO TOSHA"
Haya JT ndo nishasema, limekuuma CHOMA GANZI

so polisi wamewabeba
na kuwapeleka
temeke hospitali
naksikia kuna vurugu
kiasi polisi wanapiga mabomu ya machozi
wamewaweka mochuari
so wanajaribu kuwanasua
ila mume wa huyo mwanamke
kasema anataka milioni tano ili awatoe
so vurugu kila mtu anataka kuona'

Subscribe to:
Posts (Atom)