Thursday, November 8, 2012

MUME ANASIANA NA HAWARA

Vidole vyangu vimepata nguvu ghafla baada ya kusikia hii habari

'BREAKING NEWS:DAR-ES-SALAAM.kuna mwanamke aliaga kwa mume wake
anaenda tanga kusalimia
kumbe kaenda gusti tandika na mwanaume mwengine
so wakafanya mapenzi
UUME Umenasa Hautoki
so polisi wamewabeba
na kuwapeleka
temeke hospitali
naksikia kuna vurugu
kiasi polisi wanapiga mabomu ya machozi
wamewaweka mochuari
so wanajaribu kuwanasua
ila mume wa huyo mwanamke
kasema anataka milioni tano ili awatoe
so vurugu kila mtu anataka kuona'


Hivi kweli we mwanamke/mwanaume unamuwekea mumeo/mkeo mtego ili akienda nje anasane na huyo mtu?? Sijawahi kuona mapenzi ya namna hii, tena mbaya zaidi unasema huwanasui hadi upewe millioni 5.

Kwanza mwanamke/mwanaume wa namna hii namtafsiri hivi
1. Ana roho mbaya, kiasi cha kwamba haoni vibaya akiona mwenzake akikumbwa na aibu hii
2. Ana tamaa na ndiyo maana katanguliza pesa kwamba bila pesa hawanasui na mtu huyu hashindwi hata kukuua sababu ya pesa
3. Ni mshirikina, kitendo cha kwenda kwa waganga kufanya hayo yote ni ushirikina
4. Hana mapenzi ya kweli kwasababu mtu unayempenda huwezi kutaka kumuwekea mitego itakayomdhalilisha mumewe/mkewe kiasi hicho.

Wakati mwingine kabla hujafanya kitu fikiria mara mbili unaweza ukadhani unamkomoa mtu kumbe unajikomoa mwenyewe, Je, unadhani baada ya kufanya hivyo huyo mwanaume/mwanamke ndo atakupenda? au ndo ataacha umalaya? Hauoni kama unajijengea uadui wewe na mumeo/mkeo? Unadhani baada ya kumnasua atakuacha hivihivi bila kulipa kisasi? Familia yake na watu wake watakuchukulia vipi? Haya ni maswali ambayo ni lazima ujiulize

Wewe kama ni mwanamke/mwanaume wa kweli mtulize mumeo/mkeo kupitia mapenzi mpe yale anayoyafuata nje, na kama umeona kashindikana kuna taratibu zingine ila si kumdhalilisha kiasi hicho. Imefikia kipindi lazima tuwe na ubinaadam je ungefanyiwa wewe hivyo ungefurahi???

Sio kama natetea upande wowote ila nasema ambalo mimi naliona sahihi na ukitaka kunielewa ukiwa kama mwanamke / mwanaume jaribu kufikiria umefanyiwa wewe.

"POLENI SANA KWA WAHUSIKA NADHANI HILO NI FUNDISHO TOSHA"

Haya JT ndo nishasema, limekuuma CHOMA GANZI

4 comments:

  1. "ila mume wa huyo mwanamke
    kasema anataka milioni tano ili awatoe"

    Nimeona ni quote kile ulichoandika maana naona unajichanganya. Umesema mwanaume anataka 5M ili awachomoe alafu umegeuka unasema mwanamke ana roho mbaya kwa kuweka tego? How? Please edit your post. Naona umeichukulia too personal (there must be something wrong somewhere)hadi unaji contradict!

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hapa sitoi taarifa ya habari Maria, kuna source nyingi za kufanya hivyo nilichojaribu kukielezea hapo ni tabia hiyo, na nilichokieleza ni kutokana na kwamba sisi ni binadamu hivi vinatokea kwenye jamii yetu, usimcheke mwenzako kwa vile yamemkuta yeye je, huyo mwanaume uliyenaye una uhakika hajawekewa mtego?? Lazima ujiulize, tena hii inaweza hata kuwakuta wale ambao hawako kwenye ndoa utakuta mtu ana mahusiano na mtu kumbe ni mume wa mtu bila yeye kujua halafu ikamkuta hii, unadhani ni sahihi?? Acheni mambo ya kushabikia kama mtu ni malaya ni malaya tu leo utamfanyia hivyo baada ya miaka kadhaa atasahau atafanya tena...na usifikirie nimeichukulia too personal ni vitu ambavyo naviongelea kwenye blog hii labda bado hujasoma dhumuni la kufunguliwa hii blog Maria kama vipi CHOMA GANZI!Asante kwa kuvisit blog

      Delete
  2. Hata mimi Jesca siungi mkono tabia ya ushirikina; ila kama kungekuwa na njia nyingine ya kufanya watu wanasiane na mimi ningeipenda; kuna watu wengi wako kwenye ndoa lakini ni wahuni. Mimi mara kadha wife ananielezea matukia ya wanaume kumtaka kimapenzi, na kumuahidi zawadi kadhaa; si hivyo tu kuna mfanyakazi mwenzagu alikuwa anasumbuliwa sana na mke wa mtu eti anataka offer ya bia tena wakati mmewe kasafiri; kuna nini tena hape? Halafu Jesca kama unatetea uchafu huo vile!

    ReplyDelete
  3. hahahaha good maria

    ReplyDelete