Naomba msome kwa umakini na mnisaidie kutoa ushauri kwa huyu dada, ambaye yuko njia panda
Nina bf wangu ambaye tuna mahusiano ya muda mrefu kidogo, mpenzi wangu mimi yuko busy sana kwasababu ya majukumu hivyo kuonana kwetu ni kwa nadra sana, inaweza ikapita miezi 2 nisimtie machoni hapo ni kumuona tu kwenye swala la mapenzi ndo kabisaaa inaweza pita hata miezi 3 ila shida zangu za kifedha zote ananitatulia hata kama ni kodi ya nyumba ikiisha atatuma M-Pesa,
Sasa kinachonitatiza mimi ni kwamba hivi karibuni ametokea mume wa mtu ambaye naamini kuwa ananipenda, anatumia muda wake mwingi kuwasiliana na mimi na kuwa na mimi kwakuwa mpenzi wangu yuko busy sana yeye ndo huwa ananipa company siku zote na mbaya zaidi mapenzi yangu yamezidi kwake kuliko haya kwa bf wangu, mara zote anakuja yeye kwanza mbele ya bf wangu kwenye kichwa changu.
Ananipa kila ninachokitaka anaridhisha kwa kila jambo na ananielewa sana, hata kama sijamwambia kitu yeye huwa anakuwa tayari ameshafikiria na kujikuta napata kile ninachokihitaji, kiukweli uwezo wake kitandani ni mkubwa unaoniridhisha sana ananipa mahaba yote na ananifikisha ipasavyo.
Naomba nieleweke kuwa sijampendea pesa huyu kaka bali mapenzi anayonipa najisikia raha sana kila nikiwa naye imefikia hatua hata siogopi tena kufumaniwa na bf wangu, na kama akipiga simu niko naye naweza hata nisipokee naona kama ananipunguzia radha. Kusema ukweli sina maneno ya kudhihirisha ninachokipata kutoka kwa huyu mume wa mtu ila kiukweli nampenda sana, na naiheshimu sana familia yake na naomba Mungu mkewe asigundue sababu itakuwa imeniharibia.
Jamani naombeni ushauri wenu nifanyeje?? Kwani kwasasa nataka niachane na bf wangu ili niwe na mume wa mtu peke yake. Nishaurini jamani niko njia panda!
Kama una ushauri weka hapo chini, au nitumie kwa tarimojesca@gmail.com au kwenye page yangu ya facebook au twitter.
Jesca kumbe unanicheat mimi!! sikujua kama wataka kuniacha!!!
ReplyDeleteHahahahaaaaaa ebu acha kufurahisha wadau
DeleteJamani sikujua kama nakulidhishaga hivo kitandani!!
ReplyDeleteJamani sio mimi ni mtu mwingine!!! msifurahishe macho ya watu
Deletemmmmh pole 1 day utakuja juta kwa unayoyafanya leo ushasema mume wa ..... na sio mume wangu kamwe kaa ukijua hana malengo na ww
ReplyDeleteduh hii inaniusu sana ntafumaniwa nini ivi karibuni......
ReplyDeleteMme wa mtu sumu ishi nae kwa malengo
ReplyDeleteTupo wengi Jesca bt ukwel n kwamba mume wa m2 si wako hata iweje bora ukae nae mbal lasvyo utakuja kujuta......he cant leave his family fir you.....Chukua Hatua
ReplyDelete