Thursday, October 4, 2012

Una nyumba ndogo??Zingatia hili

Wewe mwanaume unajua madhara ya kumpeleka nyumba ndogo sehemu ambayo unaenda na mkeo??
Nadhani bado hujanielewa namaanisha nini, sasa nakudadafulia vizuri.

Mfano wewe mwanaume kuna sehemu hupenda kujivinjari na nyumba ndogo wako inaweza kuwa baa au kwenye mgahawa, na utakuta hata wahudumu washazoea kuwaona pale. Sasa siku moja unaamua kwenda na wife pale pale na mnajiachia vizuri sana. Hapo nadhani mtakuwa mmenipata naongelea nini

Sasa kaka yangu nikwambie hilo ni kosa kubwa mno unafanya, siku zote vya kushoto viache kushoto vya kulia viache kulia kamwe usichanganye utakuja kulivuruga.

Nakwambia hivyo kwasababu mfano imetokea siku moja upo na nyumba ndogo mkeo naye katika pitapita zake akasema hii seshemu nilishakaa na mister ngoja leo nipate msosi au kinywaji hapa, anaingia mara anakukuta unadhani itatokea nini?? Na sisi wanawake tunahiyo tabia sana ya kwenda sehemu ambazo tulishaenda na mister

Pia pata picha umekaa na wife wako mara nyumba ndogo huyo kaingia, unadhani we binafsi utakuwa na amani? haya kama huyo kimada hamjui wife yako basi jua litatokea varangati ila kuna wengine wastaarab ashajua huyu ni mume wa mtu nina mipaka naye kwahiyo atakaa sehemu nyingine kimya kajikausha kama hakujui, sasa japo amekuokoa wewe na ndoa yake ila kumbuka rohoni linamuuma pia unamdhalilisha sana unadhani watu waliozoea kuwaona pale watawafikiria vipi?? usitake kuwapa watu faida pia kwanini umfanyie mwenzako hivyo?? Inakera ati kwani hakuna sehemu nyingine?

Ila sichochoe wala kukufundisha tabia mbaya ya kuwa na nyumba ndogo najaribu tu kuiokoa ndoa yako
Mi ndo nisharopoka likikuuma choma ganzi!www.jescatarimo.blogspot.com

1 comment:

  1. mbona unaongea kwa uchungu kama vile lishakukuta nini??

    ReplyDelete