Habari zenu?? Mpo pouwa??? Hata mi niko poa kabisa.
Nadhani wengi mtakuwa mmesikia au wengine yamewakuta haya,
1.mke kukuta lipstick kwenye shati la mumewe
2. mke kukuta condom kwenye nguo ya mumewe
3. mke kukuta kipodozi au nguo au kitu chochote kwenye gari la mumewe
4. mke kukuta picha ya mwanamke kwenye simu au laptop au kwenye bahasha za mumewe
Sasa jiulize uzembe uko wapi?? Ni mkeo ndo ana kiherehere cha kuchunguzachunguza au ni wewe ndo umejisahau au umemfanya mkeo bwege kiasi cha kuacha vitu ovyo na kutojali?
Siku zote ukiwa mwizi uwe mjanja, sikufundishi utoke nje ya ndoa wala sikufundishi umalaya la hasha ninachofanya ni kumkinga mkeo ili asiumie, we unadhani akishagundua una mwanamke nje atafurahia na kukupongeza?Unadhani atakwambia 'mume wangu hongera sana kumbe we mwanaume wa ukweli eenh? ITAMUUMA SANA tena usipoangalia ndo itakuwa MWANZO WA NDOA YAKO KUYUMBA.
Sasa basi kitu cha kufanya, endapo utakuwa umetoka kwenye nyumba ndogo yako kabla hujafika home jiangalie unalipstick kwenye nguo?? Au kwenye gari kuna kitu chochote ambacho huyo mwanamke ameacha?? Ukishaangalia ukiona hamna basi waweza kwenda home pia usisahau simu yako kuiangalia manake huwezi jua kitatokea nini mbele ya safari.
ANGALIZO: Hii sio tu kwa mwenye nyumba ndogo hata kama huna mwanamke nje pia uwe unakagua gari lako coz njiani unaweza mpa mtu lift kwa bahati mbaya akasahau au akadondosha kitu huku wewe huna habari halafu wife akakuta ikawa mtiti.
Na usiseme mkeo ndo anakiherehere wewe umeshakuwa mali yake anahaki na wewe, hawezi kukuta condom iliyobakia kwenye suruali yako halafu yeye akacheka tu.
ONYO: Wewe kimada au ndo nikuite nyumba ndogo usithubutu kuacha staffs zako kwenye gari au nguo ya huyo mwanaume ilihali unajua kabisa ni mume wa mtu hiyo ni TABIA MBAYA, nasema hivi kwa kuwa mwingine anafanya makusudi kuacha mradi kumpa taarifa mke wa jamaa ili ajue ana mke mwenza, ebu wacha uswahili JIFUNZE KULA NA KIPOFU, huwezi tafuta wako wanaume wenyewe wachache halafu unataka kuharibu kwa taarifa yako umuharibii mwenzako unajiharibia mwenyewe na nilishasema na NARUDIA TENA usidhani atamuacha mkeo kwa ajili yako bali atakuacha wewe ili kuokoa ndoa yake.
SIKUFUNDISHI UWE NA NYUMBA NDOGO ILA KAMA UNAYO TAFADHALI USIMUUMIZE MKEO!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
Kama limekuuma we
CHOMA GANZI tu!!!