Monday, December 3, 2012

Kupiga Picha za Utupu!

Imekuwa ni kawaida kusikia na kuona watu wakilalamika mitandaoni na kwenye magazeti baada ya picha zao za utupu/picha chafu kuvuja.

Mimi nina maswali kwenu kwanini upige picha za utupu?? Manake wengine wanajipiga wenyewe wakiwa na akili zao timamu sasa unataka kumuonesha nani huo mwili  wako?? Hujiulizi hiyo simu au camera ikiibiwa huyo atakaye ikamata unadhani hatozirusha mtandaoni? Acha kupiga picha hizo hata kama uko makini kiasi gani.

Pia kuna wale wanawake ambao wanalewa hadi kufikia hatua ya kutokujitambua yaani kazima, mwanaume wake huyohuyo anaamua kumpiga picha za utupu bila yeye kujua na mwingine wala anakuwa hajazima ila kwa kuwa pombe ziko kichwani anajikuta anafanya maamuzi ambayo si sahihi anaulizwa nikupige picha? naye bila hiyana anasaula nguo anajimanua anapigwa picha , ndugu yangu kama pombe huziwezi acha kabisa utakuja jidhalilisha.

Sasa kuna wale wenzangu na mimi waliopofuka kwenye mapenzi wasiojielewa na wasiochuja kitu gani ni sahihi kufanya pale anapokuwa na mpenzi wake. Utakuta anamahusiano na mwanaume hata miezi sita hawajamaliza mwanaume anamwambia ampige picha akiwa mtupu naye anakubali tu! Hivi unajiamini nini na huyo mwanaume?? Hujiulizi endapo mtagombana hatima ya hizo picha ni nini?! Sidhani kama mwanaume anayekupenda atakwambia upige picha za utupu, kwani atakuwa anajali utu wako na kuheshimu mwili wako.. Wengi mnadanganywa eti akikumiss awe anaangalia picha yako, HUO NI UONGO LAANIFU!! Tena kama mwanaume atakwambia hili kuwa naye makini manake ukimkatalia ipo siku atakuvizia umelala na atakupiga bila idhini yako.

Narudia tena mwanaume anayekupenda, anayekujali na kukuheshimu hakupigi picha za utupu, kwahiyo USITHUBUTU! Kama tayari ushapiga nakushauri zifute, kwani utakuwa umeshuhudia story nyingi za mastaa wetu wakilalamika kwenye magazeti kuhusu picha zao zilizovuja na wengi wao wanasema ni watu wao wa karibu ndo wamezivujisha wengine wanasema waliowaibia simu ndo wamezivujisha.. Sasa zote hizi hazikupi fundisho tu!! Kwanini akupige wewe picha za utupu? mbona yeye hapigi hayo mapumbu yake akakutumia??

Tena wengi sana mnatumia whatsapp na BBM kutumiana hizi picha sasa wewe ukituma tu anamforwadia rafiki yake anamwambia 'cheki huyu demu kanitumia hii picha' Sasa kwa style hii unadhani zitaacha kuvuja??

Kama limekukuta pole ila kama bado basi zingatia hili. Na nyie wanaume mkome kuwapiga picha mademu zenu kama unataka piga mapumbu yako yaweke kwenye wall yako.

Limekuuma CHOMA GANZI!

Mnisamehe coz nimekuwa mvivu kidogo wa kuandika, mada, zimejaa kichwani tele ila kutype ndo inakuwa mtiti!

10 comments:

  1. Dada wewe mtaalamu nitakufuta uje gezaulole unipe maujanja ya choma ganzi

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hahahaaaa unataka ufundishwe nyumbani?? mmh we Mzee wa Gezaulole unayako sasa!

      Delete
    2. Dada naomba namba zako za cm,ili 2wasiliane,unifundishe mengi.

      Delete
  2. hii ni blog au nimeipenda kwa kweli

    ReplyDelete
  3. Duuh! Dada we ni noumer...kwan ulisomea wapi hivyo?.

    ReplyDelete
  4. Duuh! Dada we ni noumer...kwan ulisomea wapi hivyo?.

    ReplyDelete
  5. Duuh! Dada we ni noumer...kwan ulisomea wapi hivyo?.

    ReplyDelete
  6. habari inaonekana ni mtaalamu hongera kwa ushauri unaoutuoia

    ReplyDelete
  7. hmmmmmmmmmmm.......................!!!!

    ReplyDelete
  8. Ni kweli unayoyasema kwani katka jamii yetu yamekuwa yakitokea siku hadi siku

    ReplyDelete