Saturday, December 8, 2012

Nyege baada ya MP!

Ni kawaida kwa msichana kujisikia hali ya nyege au niseme muwashawasha au hamu ya kufanya mapenzi mara pale tu atokapo kwenye siku zake(MP) tena wengine hadi zile siku mbili au moja ya mwisho kabla hajamaliza MP.

Bado sijapata sababu za kitaalam kwanini hali hiyo hutokea, sijajua ni kwa vile ile pad inakutekenya au ni matokeo tu ya hormones. Hapo labda nikawatafute wataalam wanijuze then niwaletee ukumbini.

Sasa lengo la kuandika hii post ni kuwajuza wanaume na kuwapa ushauri, ni hivi mkeo akimaliza tu period HAKIKISHA UNAMPA CHAKE  manake mtoto wa kike hapo atakuwa anahamu zake sasa kama ndo hausomi mchezo mwenzako ataishia tu kuchekacheka bila mpangilio. Japo kuna siku zingine za pale katikati za mwanamke kuwa hot kwelikweli ila na hii pia usiisahau.

Kwahiyo ndugu yangu pale mkeo au mpenzi amalizapo period jaribu kumpa kitu, kama uko naye mbali basi hiyo ni bahati mbaya, na hapo ndiyo penye umuhimu wa kujua mzunguko wa mwanamke wako. Si kila mwanamke anaweza kumwambia mwenza wake kwamba ana hamu japo siku hizi wengi wanajitahidi kuwa wawazi au mwingine utaona tu vitendo vyake mara akushike hapa mara akushike pale mradi tu kukuonesha kwa vitendo anachotaka kwahiyo kama mwerevu utaelewa.

Hayo ndo yangu ya leo kila nikipata muda wa kuandika nitaandika nina mengi mno!

CHOMA GANZI!!

1 comment:

  1. hongera tena kwa darasa lako napenda uje znz kwenye taasisi yetu inaonesha una mengi ya kutupa

    ReplyDelete