Thursday, August 23, 2012

Acha kumjaribu mpenzio! Acha pozi


Kwanini unamjaribu mpenzio? Ili iweje? AU ndo unataka uone udhaifu wake? Na ukisha uona nini kinafuata?  Acha utoto huo ni ujinga, hata siku moja usimuwekee mitego mpenzi wako kwa lengo la kujua alivyo kama unataka kujua nyendo zake basi we mfuatilie tu na umchunguze ila usimuwekee mitego.
Mfano utakuta mtu anapanga na marafiki zake ili wamtongoze huyo mpenzi wake tena hii ipo Pande zote kwa wanawake na wanaume, eti  anataka ajue kama huyo mpenzi wake atamsaliti au la! Sasa ina maana we humuamini au?
Nakuambia ukweli ukijaribu kufanya hivi jua huo uhusiano wenu haufiki mbali sababu ndo utakuwa mchezo wako na mwisho wa siku mpenzio atakereka, tena mwingine akijua ndo kabisa anakuacha na huyo rafiki yako uliyemtuma anatembea naye. Kwanza usipende sana kuwaamini marafiki kwenye mapenzi  kiasi cha kumtuma akamtongoze mpenzio kwasababu anaweza fika huko akapewa mambo motomoto akanasa sasa hapo kuna mawili utaachwa na wao wataendeleza uhusiano au utaanza kudanganywa kumbe wao wanaendelea kumega tunda wewe huna habari.  Na asikwambie mtu huyo mpenzio akijua umemuwekea mtego huo hata akupende vipi atakuacha tu.
Pia kuna wale watu wengine ambao sielewi ni pozi au ni nini? Mfano utakuta mwanaume kwa siku kama mbili hivi hampigii mpenzi wake simu na akipigiwa hapokei au akipokea anamkaripia, na mwanamke wa watu wala hachoki wala hachukii anajua mpenzie kabanwa siku wakiongea sasa mwanaume anaanza kujitapa nilikuwa nimekuchunia makusudi ili nikuone presha inavyokupanda khah!! Huu ni utoto ndugu yangu na una impact mbaya sana kwenye mapenzi ukimkuta mtu ambaye uvumilivu wake mdogo lazima akuache, hebu acha mara moja hii tabia kama kweli unampenda mpenzio!

Mapenzi ni kuaminiana siyo kujaribiana na kutesana umeona hakufai basi muweke wazi ajue kuliko kupotezeana muda.
Ndio nimekulenga wewe nitupie tu mawe ila lazima uambiwe ukweli


UJUMBE: KAMA WEWE UNANIONA WA NINI WENZAKO WANAJIULIZA WATANIPATA LINI

1 comment: