Tuesday, November 20, 2012

Wapenzi kuishi pamoja kabla ya ndoa

Habari,

Kuna kitu ambacho ni muhimu sana leo nahitaji kuwaambia na nimekiona sana tu kwa watu wangu wa karibu.
Kuna tabia ambayo inazidi kushamiri kwenye jamii yetu tofauti na miaka ya nyuma, tabia ya wapenzi wawili kuishi nyumba moja. Si jambo baya kufanya hivyo manake wengi watasema wanataka wajuane kabla hawajajipanga na ndoa ila ni vigezo gani umechukua hadi kufikia uamuzi huo? Mi nadhani kabla ya kukurupuka kufanya hivyo hebu fikiria kwanza, je familia zenu zinaruhusu hivyo?? Unauhakika mnawezana kuishi nyumba moja manake nimeona watu wengi wanafanya hivyo hadi kufikia hatua ya kununua vitu kwa kushare mwisho wa siku wanashindwana ugomvi mwanzo mwisho na hatimaye kuanza kugombea vitu 'hiki nilinunua mimi mara hiki siyo cha kwako' huko ni kujiaibisha kama mnajiamini mnapendana na kuwezana basi fungeni ndoa na kama mnachunguzana basi mchunguzane kwa tahadhari manake mtu hashindwi kuficha makucha kwa kipindi chote ambacho unakaa naye kabla ya ndoa hata kama ikiwa mwaka. Pia dada yangu usidanganyike si kila mwanaume atakaye kwambia mkae wote atakuoa mwingine ndo kwanza anazidi kubweteka, manake ameshaona kuna mwanamke anamfanyia kila kitu kupika kufua kuosha ovyo, unadhani atakaa afikirie ndoa? Hapana, utasikia kila asiku anakwambia ngoja nijipange..... ajipange na nini? kwanini msijipange wote na maisha muanze pamoja? Kuwa makini mwanamke!

Simaanishi usikae naye ila ndo utumie akili sio ubweteke tu mwisho wa siku utajikuta unazalishwa watoto watano bila ndoa wala nini!

Mi nisharopoka hivyo na kama limekuuma CHOMA GANZI,......

No comments:

Post a Comment