Friday, September 21, 2012

Mwanaume kutokuwa Smart nini shida?

Nitakushangaa sana wewe mwanamke unamuona mumeo anaondoka lakini kavaa nguo ya ajabu.

Hivi kweli kabisa kwa moyo mweupe bila hata kutikisika mumeo anatoka nyumbani anaenda kazini shati limejikunja halijanyooka vizuri, au chafu halijafuliwa au ndo kalirudia la jana tena linanuka jasho ukimuangalia miguuni viatu vichafu tena mwingine hata nywele hajachana mindevu imekaa tu ovyo?!!

Unajisikiaje unapopita barabarani ukiwaona wanaume wengine wako smart halafu mumeo ndo vile?? Tena wengine wanavaa hadi mashati yaliyochanika au soksi zilizotoboka, we hauoni kama unajiaibisha wewe?

Hakikisha havai soksi iliyotoboka wa kutoa harufu!

Kumbuka yeye ni mwanaume hana shida yeye kichwa chake kinawaza wapi apate pesa familia ikae vizuri kwa hiyo usipomwangalia anaweza kwenda kazini hata na kaptula, jukumu la mavazi ni lako wewe mwanamke hata kama na wewe unamajukumu ya watoto ila kumbuka mume ndo mtoto mkubwa naye anapaswa kuangaliwa kama hao wadogo kabla hajaondoka mtupie jicho mumeo, sio umchunguze?la hasha muangalie tu nguo alizovaa je ni zile ulizompangia avae?? kama siyo zinaendana?hazina kasoro? Manake wewe ndo utakuwa unazijua nguo zake kuliko hata yeye mwenyewe, usikubali mumeo atoke ndani kavaa shati la njano, tai ya blue, suruali ya kijani viatu vya brown. Soksi zinanuka hatari. Huoni aibu wewe?? Hakikisha soksi za mumeo ziko katika mpangilio na hazijatoboka manake wao wakiona soksi wanavaa tu hata kama zimetoboka au chafu wao hawajali tena na kama ziko tofauti anavaa hivyohivyo hawana muda wa kuangalia soksi nyingine iko wapi, na  kama mume wako muwazi atakwambia "uwe unaniandalia nguo"! sasa hili ni tusi kwa mwanamke, haupaswi kukumbushwa majukumu yako, japo kuna wanaume wengine wanakujipenda, yeye hata usipomchagulia nguo atajing'arisha mwenyewe.
Mwanaume akiwa smart anavutia!

Hivi hujisikii raha watu wakimsifia mumeo alivyosmart? hujisikii raha hata kumtambulisha kwa mtu 'jamani huyu ndo mume wangu'

Wengi mtasema mnaogopa kuibiwa, asikwambie mtu mwanaume hapendewi mavazi kwahiyo watu wakiamua kukuibia watakuibia tu!

Hili ndo langu la Ijumaa, najua sana kuna watu litakuwa limewauma kama ni mmoja wao CHOMA GANZI!
Kama siyo basi freshh! Endelea kuvisit www.jescatarimo.blogspot.com

Ijumaa njema

2 comments:

  1. U-smart ni kipaji mamii, kuwa msafi ni mpaka ujiandae, na si kukurupuka! Na u-smart si kuvaa suruali ya kitambaa na shati la rangi moja kwa tai ya udhurungi!

    ReplyDelete
  2. Ushuhuda Wangu Kuhusu Dkt. Dawn – Mtu Aliyerejesha Nyumba Yangu na Furaha Yangu

    Nataka kushiriki ushuhuda wangu wa dhati kuhusu jinsi Dkt. Dawn alivyobadilisha maisha yangu kabisa.

    Kwa karibu mwaka mmoja, mume wangu aliniacha mimi na watoto wetu wawili. Aliacha kujali, akaacha kupiga simu, na alikuwa ameenda kabisa. Nilikuwa nimevunjika moyo, nimechanganyikiwa, na karibu kupoteza tumaini. Kisha siku moja, rafiki aliniambia kuhusu Dkt. Dawn, mtu wa kiroho aliyepewa kipawa na ulimwengu kuwasaidia watu kurejesha upendo na amani.

    Mwanzoni, nilikuwa na shaka, lakini kitu kuhusu maneno yake kilinipa amani. Aliniambia haswa kilichokuwa kibaya na kwamba mtu alikuwa ametupa uchawi mkali kututenganisha. Aliandaa kazi maalum ya kiroho na uchawi wa kuungana tena kwangu — na ndani ya siku chache, mume wangu alinipigia simu ghafla, akilia na kuomba msamaha.

    Tangu wakati huo, maisha yangu hayajawahi kuwa sawa. Ndoa yetu sasa ni tamu na yenye furaha zaidi duniani. Tunapendana zaidi kuliko hapo awali, na nyumba yetu imejaa vicheko na baraka.

    Lakini si hayo tu — Dkt. Dawn pia alisaidia kuondoa bahati mbaya na nishati hasi iliyokuwa ikizunguka familia yetu. Tangu wakati huo, kila kitu kimekuwa laini: amani nyumbani kwetu, maendeleo ya kifedha, afya njema, na furaha safi.

    Ninashukuru ulimwengu kila siku kwa kuniongoza kwa Dkt. Dawn. Kwa kweli ni mtu mwenye nguvu na mwanga wa kimungu. Ikiwa unapitia hali yoyote — huzuni, bahati mbaya, au mkanganyiko — usikate tamaa. Mfikie na uache ulimwengu ufanye kazi kupitia yeye ili kubadilisha hadithi yako, kama vile alivyobadilisha yangu.

    Wasiliana naye kwenye WhatsApp: +2349046229159
    Barua pepe: dawnacuna314@gmail.com

    ReplyDelete