Kwanini unamjaribu mpenzio? Ili iweje? AU ndo unataka uone
udhaifu wake? Na ukisha uona nini kinafuata?
Acha utoto huo ni ujinga, hata siku moja usimuwekee mitego mpenzi wako
kwa lengo la kujua alivyo kama unataka kujua nyendo zake basi we mfuatilie tu
na umchunguze ila usimuwekee mitego.
Mfano utakuta mtu anapanga na marafiki zake ili wamtongoze
huyo mpenzi wake tena hii ipo Pande zote kwa wanawake na wanaume, eti anataka ajue kama huyo mpenzi wake atamsaliti
au la! Sasa ina maana we humuamini au?
Nakuambia ukweli ukijaribu kufanya hivi jua huo uhusiano
wenu haufiki mbali sababu ndo utakuwa mchezo wako na mwisho wa siku mpenzio
atakereka, tena mwingine akijua ndo kabisa anakuacha na huyo rafiki yako
uliyemtuma anatembea naye. Kwanza usipende sana kuwaamini marafiki kwenye
mapenzi kiasi cha kumtuma akamtongoze
mpenzio kwasababu anaweza fika huko akapewa mambo motomoto akanasa sasa hapo
kuna mawili utaachwa na wao wataendeleza uhusiano au utaanza kudanganywa kumbe
wao wanaendelea kumega tunda wewe huna habari.
Na asikwambie mtu huyo mpenzio akijua umemuwekea mtego huo hata akupende
vipi atakuacha tu.
Pia kuna wale watu wengine ambao sielewi ni pozi au ni nini?
Mfano utakuta mwanaume kwa siku kama mbili hivi hampigii mpenzi wake simu na
akipigiwa hapokei au akipokea anamkaripia, na mwanamke wa watu wala hachoki
wala hachukii anajua mpenzie kabanwa siku wakiongea sasa mwanaume anaanza
kujitapa nilikuwa nimekuchunia makusudi ili nikuone presha inavyokupanda khah!!
Huu ni utoto ndugu yangu na una impact mbaya sana kwenye mapenzi ukimkuta mtu
ambaye uvumilivu wake mdogo lazima akuache, hebu acha mara moja hii tabia kama
kweli unampenda mpenzio!
Mapenzi ni kuaminiana siyo kujaribiana na kutesana umeona
hakufai basi muweke wazi ajue kuliko kupotezeana muda.
Ndio nimekulenga wewe nitupie tu mawe ila lazima uambiwe
ukweli
UJUMBE: KAMA WEWE UNANIONA WA NINI WENZAKO WANAJIULIZA
WATANIPATA LINI
Sawa kungwi!
ReplyDelete