Bado sijajua undani wa hili jina na origin yake ila ndilo jina linalotumiwa kumwita kijana mdogo anayekuwa na mahusiano na mwanamke mtu mzima ambaye anaweza hata kumzaa, mara nyingi 'marioo' huyu anafuata pesa tu kwa huyo mwanamke wala si kingine na pembeni atakuwa na msichana mwingine ambaye ndiye atakuwa anampenda
Sasa hivi mjini hawa watu wamejaa sana, tena sikuhizi hawaoni hata aibu wanajionesha waziwazi. Utakuta kijana mdogo sana lakini anampetipeti jimama huyo hadi utabaki mdomo wazi na hapo pengine anajua kabisa labda huyo mwanamke ni mke wa mtu lakini wala hashtuki, kwanini ashtuke wakati yeye yupo pale kuchuma pesa? Utakuta amekabidhiwa gari aendeshe sasa hizo fujo mtaani kwao hapakaliki mradi tu mbwembwe, sasa ndugu yangu kama wewe ni marioo jua upo hatarini sana kuhariibikiwa na maisha yako hizo pesa unazozifuata utakuja kuziona chungu, wenzako yamewatokea na tumewaona sasa itakuwa zamu yako.
Acha umarioo wewe fanya kazi, mwanaume atakula kwa jasho we vipi????
No comments:
Post a Comment