Zawadi inaweza kuwa kitu chochote cha gharama au si cha gharama, thamani yake ipo kwa yule mtu anayepewa.
Uzuri wake ni upi?
Kwenye mapenzi zawadi ni kiungo muhimu sana, sio lazima umletee mpenzi wako kitu cha gharama saaaana unaweza ukanunua hata ua au card yenye maneno mazuri ukampelekea au hata chocolate, hii itamfanya ajione kuwa anakumbuka basi kwa kiasi fulani upendo wake utaongezeka kwako ataona anapendwa sana hivyo naye atajitahidi kurudisha mapenzi kwa nguvu zake zote na hapo kwa asilimia fulani mapenzi yenu yatakua.
Ubaya wake ni upi?
Kuna baadhi ya watu hupenda sana kuwapa wapenzi wao zawadi mfano kila akisafiri lazima amletee pafyumu fulani japo sio mbaya, kwahiyo yule mwanamke anakuwa ashajijengea mpenzi wangu mimi akisafiri akirudi lazima ana pafyumu mkononi, sasa hii ni mbaya jaribu kuruka ruka zawadi nyingine mpe hata ukiwa hujasafiri, au siku nyingine ukisafiri unarudi mikono mitupu au unambadilishia zawadi ili usimjengee mazingira ya kukariri. Madhara ya yeye kukariri zawadi ni makubwa sana kwasababu yeye anajua mpenzi wangu akisafiri lazima aniletee kitu fulani halafu unarudi mikono mitupu unadhani inakuwaje? Kuna wengine wanabwatuka kabisa 'inamaana dear hujaniletea zawadi yeyote?" mwingine hasemi kitu anajifanya yuko sawa ila utaona ghafla mapokezi na ule uchangamfu wake ghafla unapotea.Nadhani wote mnaelewa mapenzi ya sikuhizi yapoje
Pamoja na hayo yote mpe mpenzio zawadi hata pipi ni zawadi banaaa! Na wewe unayepewa zawadi jifunze kushukuru!
Sijamlenga mtu yeyote hili ni wazo tu lililonijia leo, usije ukaanza kuleta zawadi japo nitapokea heheheeeeee! Kama limekuuma kachome ganzi
No comments:
Post a Comment