Tuesday, August 14, 2012

Usibweteke

Kuna watu huwa wananishangaza sana yani wao wenyewe wanategemea wapenzi wao wawafanyie kila kitu gharama za matumizi zote wanawaachia wapenzi wao wao hata kusema kujishughulisha na kitu hawana wapo tu! Mradi mpenzi wake anapesa basi yeye anachojua ni matumizi tu, Sio vizuri hata kama mumeo anapesa lazima ujitahidi nawewe ujishughulishe na kitu chochote japo lotion yako ununue kwa pesa yako mwenyewe au we huoni mateso kila ukitaka kitu unaanza kuomba' Dear lotion imeisha'

Vitu vidogo jifunze kununua mwenyewe, kama huyo mpenzi wako anahela sana na anataka maendeleo yako basi hata kama hujasoma atakufungulia biashara sababu atakuwa ashaisoma akili yako ashajua kuwa si mtu wa kubweteka lakini wewe ukijifanya wa kwenda salon na shopping za nguo kwa wingi unadhani atakufungulia biashara yoyote? Ataona kama anapoteza pesa zake bora awe anakupa hivyohivyo tu sasa haya si mateso?

Loh! shostito kama limekuuma choma ganzi! ila mi ndo nisharopoka

No comments:

Post a Comment