Si kila unachoomba unapewa kwa moyo mweupe vingine unapewa kwa moyo wenye giza, tena huwezi jua mtu anaumia kiasi gani kukupa hicho kitu sema kutokana na mazingira mliyoishi, mapenzi na heshima anaamua tu kukupa.
Kabla hujaomba kitu kwa mtu fikiria mara mbili, watu wengine wanamioyo ya kutoa hashindwi kukupa wewe chakula chake chote kisha yeye akashinda njaa. Angalia kitu gani unaomba kwanza na huyo mtu unayemuomba ni nani na uwezo wake wa kukupa. Anaweza kukupa ila moyoni anasononeka sana imemuuma sana moyoni sasa usitegemee utabarikiwa na hicho kitu alichokupa kama ni pesa basi hutaifanyia hata kitu cha maana, kama ni gari basi hata wiki nyingi utaona ajali, kama nyumba utashangaa ajali za moto hazikuishi na ikiwa ni mpenzi sijui hapo inakuwaje.
Kuwa makini
Sijamlenga mtu hili ni wazo tu limenijia, msinirushie mawe
No comments:
Post a Comment