Hakuna binadamu asiyekuwa na wivu kwa mtu ampendaye ila ukizidi unaharibu hata hayo mapenzi yenyewe.
Utakuta mtu anamfuatilia mpenzi wake hadi kufikia hatua ya kumtumia watu ili wamtongoze ajue kama huyo mpenzi wake mwaminifu au lah sasa ukikutana na mshenzi mwingine huyo uliyemtuma anatembea naye na wewe anakumwaga vilevile,
Pia kuna wale wa simu, akikupigia akikuta simu busy tu ugomvi sasa yeye hana ndugu, jamaa na marafiki? kwenye hiyo simu kuna namba yako wewe tu? na hawa wanatabia ya kushika sana simu za wapenzi wao ikiingia sms wa kwanza utafikiri simu yake au simu ikiita tu utaona alivyotoa mijicho kama mjusi aliebanwa na mlango.
Japokuwa wanasema mapenzi bila wivu hakuna mapenzi ila mi nakwambia, ukiwa na wivu uliopitiliza unakuwa kero kwa mpenzio so jitahidi uwe na wivu ule wa kibinadamu usitake kuchunguza chunguza sana au kusikiliza ya watu wanayoongea nje, msikilize mpenzio na jifunze kuamini kile cha mdomoni mwake hata kama unahisi anakudanganya we muitikie tu coz atajichanganya tu na ukweli utajulikana.
Halafu nikwambie siri yule anayejifanya anakuonea wivu sana na kukuchunguza chunguza jua kuna kitu nyuma ya pazia kuna uovu anaufanya sasa anahisi na wewe unafanya hivyohivyo.
Angalizo: si wote wenye wivu uliopitiliza wanamambo wanafanya nyuma ya pazia wengine ndo hivyo wamezaliwa
Ila kwa ushauri wangu hakuna binadamu asiyekuwa na wivu hata mimi mwenyewe nina wivu sana, ila tu punguza wivu kidogo jaribu kumtrust mpenzi wako japo kidogo, wivu ukizidi ni kero. Siku ukiona kama unachezewa rafu kabisa sasa hapo fanya mchakato.
BATA UKIMCHUNGUZA SANA HAUTAMLA!
No comments:
Post a Comment