Tuesday, August 28, 2012

Unatembea na Mume wa Mtu? Soma hapa

Sasa leo nawaibukia wanawake wanaotembea na waume za watu,

Utakuta mtu anaanza mahusiano na mwanaume ilihali akijua kabisa ni mume wa mtu. Mwanaume wa watu kamweleza ukweli kabisa kuwa mimi nimeoa ila nataka kuwa na wewe we mwanamke na nyege zako na tamaa zako au pengine na wewe umempenda unakubali ila ninapokwazika mimi ni pale mwanaume akikwambia muda umeenda wacha niwahi home we unanuna sasa unanuna ili iweje? Ulitaka alale kwako? Si alishakwambia ana mke na unajua lazima alale kwa mkewe, kama unataka mtu wa hivyo basi tafuta wa kwako ila kama umeamua kuwa na mume wa mtu basi heshimu familia yake, usitake kumkwaza wala kumvurugia ndoa. Kwanza we huoni raha kama mwanaume atakuwa na furaha muda wote kuliko wasiwasi? Manake ukimvurugia ndoa hata wewe utamkosa asikudanganye mtu hakuna mwanaume asiyempenda mkewe, watakwaruzana mwisho wa siku watasuluhisha wataendelea na maisha shosti we utabaki kuumbuka.

Maji ukiyavulia nguo sharti uyaoge na ukipenda boga penda na ua lake umependa mume wa mtu basi heshimu familia yake!

Jifunze kula na kipofu shoga hahahaaaaa lako hilo!

Hii imemtokea rafiki yangu wa karibu sana, ila nashukuru ndoa yake haijavunjika.

Linauma, choma ganziiiiiiiiiiiiiiiiii

3 comments:

  1. Kushuhudia mambo kama haya kuna mawili, aidha ni muhusika wa moja kwa moja ama limemgusa mtu wa karibu yako. Hapa umetuambia rafiki yako ndio yamemkuta hayo, je wewe ulishawahi kuwa na bwana ambae ni mume wa mtu?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hili limemkuta rafiki yangu wa karibu ndo maana niliandika, unataka kujua kama nilishatembea na mume wa mtu, hahahaaaa tayari tena alikuwa mtamu huyo, sema nilikuwa sijui kama kawahiwa.....Jingine????????????????

      Delete
    2. Baada ya kugundua kuwa amewahiwa ulifanyaje?

      Delete