Hata salamu leo sitaki,
Hivi we mwnaume wa aina gani?? Umekaa na mkeo au mpenzi wako anapita mwanamke mwingine unageuka na kumtolea mimacho tena unaduwaa kabisa, hivi we hauna haya na kama huyo mwanamke atakuwa amekaa meza ya nyuma basi ndo kabisaaaaa kila saa unageukageuka. Hakyanani mi nikikuona nitakumwagia maji.
Haya kwa wale waendesha magari, utakuta mpenzi wake yuko pembeni na yeye anaendesha sasa akimuona msichana tu pembeni anapita au kasimama barabarani basi kosa lazima aangalie mara mbilimbili, vipi baba? utapata ajali bureee,
Najua wengi hapo mnanijibu "aaah si fahari ya macho?" Sawa we unaona fahari ya macho lakini hiyo inamuumiza mwenzako.Na yeye akipita mwanaume mwenye mvuto aangalie?? Au akipita mwanaume ana gari ya nguvu kuliko hiyo Vits yako aangalie??Najua na nyie inawauma sana, sasa kwa nini umfanyie mwenzio? Mjini sasa hivi kila mtu mzuri kila mtu anajua kuvaa utaangalia wangapi? Jifunze kuridhika na kujivunia ulichonacho, kama unamuona hajapendeza mpendezeshe ati! wannakwambia USIONE VYAELEA UJUE VIMEUNDWA hao unaowaona warembo wamerembeshwa sasa hata ukisema umchukue huyo mrembo usipomgharamia atakongoroka vilevile.
Na niwaambie ukweli wengi wanalalamika ooh mi demu wangu hayupo serious kwenye mahusiano yetu sijui nini...sasa ye ashakuona mwanaume macho waluwalu unadhani atakaa anaona bora na yeye aendelee na mambo yake manake asije akalia bure mwisho wa siku.
Hata kama atapita mrembo gani angalia tu kama ambavyo jicho halina pazia endelea na mambo yako, kuduwaa na kugeuzageuza shingo huo ni ushamba!! Unamwaibisha mpenzio.
Najua hili limewauma sanaaa sasa nasema hivi nendeni kwa hospitali wote mkachome ganzi
Mi ndo nisharopoka
Copy and paste!
ReplyDeleteKiutoka wapi? tiririka na ushahidi juu!
DeleteKutoka Orijino Komedi kwenye segment ya Joti (Makavu Live) Alhamis iliyopita, kama haukubali basi waambie mashosti zako mkae leo kwny marudio saa 12 jioni muangalie kipindi cha Orijino Komedi! Teh tehee teheeeee, lkn kutumia mlenda kwny barabara ya lami haikataliwi, ndio asili yetu wabongo! Ni mtazamo tu
ReplyDeleteMmmh ubaya ni kwamba hata siangaliagi hicho kipindi kwa mlioona naombieni mniambia kama kuna ukweli na kama utakuwepo basi utakuwa mgongano wa mawazo na sidhani kama atakuwa amefikisha ujumbe sawa na mimikikubwa hili ni jambo ambalo lipo kwenye jamii na kama wewe ni mwanaume basi najua hili tatizo pia unalo na kama ni mwanamke basi analo mpenzio au unabisha?? najua huwezi kukubali ukweli. All in all ujumbe umefika, limekuuma choma gaaanzi!
Delete