Wanawake wengi walio kwenye ndoa au wanaoishi na wapenzi wao huwa wanakosea kitu kimoja, GUBU
Gubu ni nini? Ni ile tabia ya kuongea sana kwa shutuma. Utakuta mume akirudi tu anaulizwa, ulikuwa wapi? ulikuwa na nani? unafanya nini? mbona umechelwa? tena hapo mwanamke kanuna. Jamani jamani jamani mwanaume hata hajapumzika hajapata hata kikombe cha maji? maneno yanaanza??Kwa mtindo huu ndo maana wanaume wengi wanaona bora tu wachelewe kurudi wapite baa wanyweeeee ili akija home hata useme nini yeye hakusikii analala tu, na kwasababu hii wanaume wengi hawapendi kutoka na wake zao manake wakitoka maneno njia nzima mwanamke hayamuishi. Punguza shosti, gubu linakera.
Ni vizuri kujua mahali aliko au alipokuwa mumeo ila tumia njia za busara kumuuliza, akirudi mpokee vizuri muandalie maji ya kuoga, chakula akishapumzika ndo unaweza kumuuliza tena si kwa ugomvi.
NA sio tu kwa mumeo pia kwa mtu yoyote yule acha kuongeaongea sana ndo nyinyi ambao mnakimbiwa na ndugu, hata salamu kutoka kwao hupati wala hata siku moja huoni mtu akija kuwasalimia. Yote hii inasababishwa na gubu, Punguza bibie
Kama linauma choma ganzi, mi ndo nisharopoka!
Chezea JT wewe!!
No comments:
Post a Comment