Tuesday, July 17, 2012

Acha kutembea na Shemeji yako



Ni kwanini unatembea na rafiki au ndugu wa mpenzi wako(shemeji yako)?? Yani umeshindwa kufanya umalaya wako woooote huko nje hadi uufanye kwa mtu wa karibu na mpenzio?? sasa nakwambia hii ni mbaya sana kwasababu ikigundulika aibu yake ni kubwa mno, na usifikiri huyo shemeji yako anakupenda saaana ila amekuona maharage ya mbeya na malaya wa kutupwa na ndio maana wala hajaona aibu kujiingiza kwenye mahusiano na wewe...na siku ikigundulika usifikiri wao watagomba na kuwa maadui bali watakuona wewe ndo unawachonganisha kutokana na umalaya wako na utaachwa kwenye mataa.

We kaka au dada jitahidi sana usiwajengee mazingira ya faragha mpenzi wako na rafiki/ndugu yako, la sivyo utakuja juta, nakueleza ukweli kila mtu ana mapungufu yake!! Simaanishi ndo wawe wanaogopana la hasha ila kuna yale mazingira ya faragha, kwani we huna wivu bwanaaa sasa inakuwaje hapo??

Na kuna mijitu mingine imebobea kwa kutembea na shemeji zao utakuta umeenda tu chumbani umewaacha sebuleni tayari mtu anaanza kutia sumu mara "ooh shemeji unajua we waukweli sana" au "shem we mi nakukubali sana yani natamani ningekuwa na mtu kama wewe" basi ataanza kummwagia misifa paleeee na kama mwanamke nae mdhaifu basi mwenye mali hana chake watakuwa wanamvizia kila akitoka huku nyuma wao wanakiss au wanachezeana mradi laana tu....na we utagundua mazingira ya ajabuajabu kila ukirudi utashangaa kama walikuwa wanaongea basi watanyamaza halafu kama kunakuwa na ukimya na kujibaraguza flani hivi!

ACHA TABIA MBAYA TAFUTA WA KWAKO!

5 comments:

  1. hakuna bwana, kwani nikionja kidogo tu kuna mbaya gani,tena wadada hee,kitu kizuri ule na nduguyo,sasa aende nje kuleta ukimwi

    ReplyDelete
  2. mimi nimeshaonja wa kwake huyo

    ReplyDelete