Wednesday, July 11, 2012

HII MAKALA IMENIVUTIA NA INA UKWELI TUPU HEBU SOMENI
Wengine hutafsiri kwamba mwenzi wa maisha yako utamtambua kwa namna ambavyo anakufanya ujisikie hamu ya tendo mara kwa mara hata baada ya kutoka naye faragha muda mfupi uliopita. Mtazamo huu nao ni potofu, badala yake jiulize tena, je, mwenzi wako anakufanya ujihisi mtulivu?
Je, anakufanya ujione ni mwenye furaha? Nazungumzia furaha ambayo inakuja yenyewe, siyo ile ya kulazimisha. Mwenzi sahihi kwako kwa zaidi ya asilimia 99, anapaswa kuongeza kitu chanya kwenye maisha yako. Endapo ukijitazama unajikuta unazidi kupotea badala ya kusafiri kwenye mstari ulionyooka, hapo unazidi kupotea.
Yatazame maisha yako kabla hujakutana naye, halafu jiulize mabadiliko yako. Je, ni hasi au chanya? Inawezekana kweli ameyafanya maisha yako kuwa na furaha lakini hiyo furaha anaidumisha vipi? Isije ikawa anakufurahisha pale tu anapokuwa na shida zake, pindi unapomtatulia huyo anakwenda zake, akirudi tena ujue ana shida.
Mathalan, mwenzi wako anatimiza kila kitu unachohitaji. Anageuka mtu wa ndiyo na kutekeleza kila ombi lako. Wewe unajiona unatisha kwa kuona kwamba mwenzi wako anakunyenyekea unavyotaka. Kumbe mwenzako ana malengo yake, mkishaingia faragha na kukidhi haja zake, ule unyenyekevu wake wote unaondoka, anarudi kuwa yuleyule. Huyu mtu hakufai ni bora uachane nae na kutafuta ustaarabu mwingine.

1 comment:

  1. thats true wng smtms frustratn za maisha znaeza 2danganya n feel that man/lady z perfect bt may b 4da tym being n nt 4ever...

    ReplyDelete