Saturday, September 29, 2012

Kwa Ujumbe huu mwanamke yupo hatua 5 mbele ya mwanaume!!


Habari zenu wapenzi!!
Namshukuru Mungu naendelea vizuri japo nilikuwa nasumbuliwa na mafua, sasa mmoja wa marafiki na mpenzi wa blog kanitumia hii email kaniambia niweke bloguni kwa manufaa ya wengi, kwa jinsia yeye ni mkaka. Naomba  usome hapo chini


Hii itasaidia wengi!
Ni kweli kwamba mapenzi hayachagui umri? Umeshajiuiza kwa nn mapenz mengi ya kishuleshule yanaishia njiani? Kwa nn wanaooana na umri sawa ndoa hazidumu au migogoro haiishi?
Kwa mujibu wa utafiti wangu nimegundua kwenye mapenzi umri pia ni kigezo kikubwa. 
Kiukweli wasichana wanafanikiwa kupevuka kiakili ya maisha haraka kuliko wavulana. Najua wanaume wengi mtalipinga hili lakini ngoja nitoe mifano michache ambayo itadhibitisha haya.
Leo msichana wa darasa la pili anaweza kukabidhiwa familia akawapikia, akafua nk. Mvulana wa umri huo huo km kuna kubwa anaweza kufanya bac ni kuendesha gari la mabati tena alilotengenezewa. Tayar huyu msichana kakuacha mbali na huenda mvulana akamaliza primary hajapiga hiyo hatua. 
Jiulize leo mabinti wangapi waliachiwa mimba hawana nyuma wala mbele lakini wamelea bt akili ya mwanaume ilifika kikomo na kuona kukimbia au kukana mimba ndiyo suluhu?
Hiyo ni mifano michache tu kati ya mingi. Kwa ufupi inadhibitisha ukweli huu kwamba wasichana wana upeo mkubwa sana kimaisha kulikio wavulana. 
Watu wawili hawawezi kwenda njia moja wasipopatana na kwa kila kitu hasa kiakili na kifikra. Utakubaliana na mimi kwamba kutokana na mifano hiyo hapo juu kwa mwanaume kwa akili ya maisha analingana na binti mdogo kwake kiumri may be zaidi ya miaka 6 na kuendelea. Niishie hapo ntamalizia siku nyingine. 


Haya kama kuna mwenye chochote cha kuongeza tiririka hapo chini!!

Friday, September 28, 2012

Tusaidiane kumshauri huyu!


Habari zenu wapendwa kuna rafiki yangu wakaribu kanitumia hii email nimemshauri ila naomba nanyie mtoe mawazo yenu hapahapa na siyo facebook wala Twitter.
Hellow!
Jesca kuna issue nahitaji comment yako. Hii imemtokea Mdogo wangu. Ni ndefu Ila usichoke tafadhali nisaidie huu mzigo.
Iko hv: Dogo alitokea kupendana na binti mmoja then wakaanzisha mahusiano mambo yakaendelea na kweli Dogo anakiri alishikwa kwa maana alimpenda sana na alijitahidi kufanya kila lililokuwa ndani ya uwezo wake. Walidumu km mwaka na zaid bila matatizo! Muda baadae yule binti akajichanganya kwa siri na Daktari mmoja hv. Baadae siri ikafichuka Dogo akamuuliza kuhusu hilo akakiri ni kweli na alifanya hivyo kwa sababu alikuwa na shida ya kifedha kwa hiyo kuwa naye alikuwa anapata fedha. Ilimuuma sana mdogo wangu akaamua kumuacha yule binti lakini kwa huzuni coz alikuwa anampenda sana. Bac akawa anajitahd kujikeep busy ili amsahau na kweli akafanikiwa.
Baada ya miezi 3 binti akawa amempigia cmu akimtaka waonane bac tayari ikawa imemuathiri sana Dogo akaja kunilalamikia. Akawa ananiambia cwez kuacha kumuona coz bado nampenda na kweli jana kaja wameonana ss aliyomueleza ni haya!
Kwanza kipindi chote cha zaidi ya miezi mitatu alikuwa na huyo jamaa na ameshabebeshwa mimba Ina zaidi ya mwezi ss km na nusu hv. Anachotaka yy binti anataka warudiane na Dogo na watunze huo ujauzito ambao anakiri kweli ni wa huyo jamaa na mbaya zaidi huyo mhusika ameukataa. Kwa upande mwingine binti anajua Dogo anampenda so anachukulia hiyo advantage.
Mm nimeombwa ushauri nikashtuka nisijibu lolote naweza kuharibu Ila ww nakuamini naomba isome scenario vizuri na uamue km mwanamke. Nashukuru sana mpenzi wangu kwa ushauri wako!


USHAURI WANGU:

Huyo mwanamke anasumbuliwa na tamaa ya fedha, siku zote ukimpenda mtu basi utamvumilia tu. Pia yuko hatarini sana kuambukizwa Ukimwi na magonjwa ya ngono. Na inavyoelekea huyo msichana ashajua mdogo wako anampenda na ndiyo maana alikuwa hata na uhuru wa kumwambia yupo na Doctor kwaajili ya pesa tu. Hii ni hatari sana kama mwanamke anaweza kuwa huru kiasi cha kukwambia anatembea na mtu fulani kwasababu ya pesa basi ni wazi anajua ashaichota akili yako angekuwa mwingine angeogopa tena angeweza hata kudanganya mradi asikupoteze.

Kama ameweza kuja na mimba kesho atamletea UKIMWI, hivyo basi huyu binti aachane naye mara moja na jua kwamba amerudii kwa mdogo wako kwakuwa kule ametelekezwa asingetelekezwa wala asingemkumbuka.

Hata kama akiamua amsamehe na kurudiana naye inamaana mimba itabidi watoe hapo watakuwa wametenda dhambi kubwa pia siyo rahisi kwa fikra za binadamu wa kawaida akasahau hicho kitendo siku zote itaendelea kumuumiza kwenye kichwa chake, kiufupi itamuharibu kisaikolojia na pengine hata mapenzi ya zamani aliyokuwa nayo kwake yatakufa, HAWAWEZI TENA KUWA NA FURAHA! Huyo binti azungumze na familia yake wajue jinsi ya kwenda kuzungumza na huyo dokta au familia yake taratibu nyingine za sheria zifuatwe nadhani hilo ni fundisho kwa wasichana wote.

Huyo mdogo wako mwambie aendelee na maisha yake wasichana wapo wengi sana kwasasa atulie afanye kazi kwa bidii iko siku atajitokeza mtu ambaye atamdatisha kuliko huyo wa sasa.

WASICHANA JITUMENI WENYEWE TAFUTENI KWA MAJASHO ONA SASA MNAJIKUTA MNAWAPOTEZA WAPENZI WENU KWASABABU YA TAMAA YA PESA

Kama kuna ushauri wowote tiririka!

Kama limekuuma CHOMA GANZI

Tuesday, September 25, 2012

Wapenzi kufanya kazi ofisi moja!

Ni wengi sana wameshajiingiza katika mahusiano na mfanyakazi mwenzake yaani ofisi moja kwahiyo najua wengi litawagusa.

Ki ukweli kwa jinsi nilivyoona wengi waliodumu kwenye mapenzi haya hadi kufikia ndoa na ndoa zao zikadumu ni wazee wa zamani lakini si kizazi hiki cha sasa, japo wapo wachache ambayo wameweza kufikia malengo yao ila si wote.

Sasa naomba niwaelezee kwanini wengi hawajafika popote

Kwenye maofisi kama mnavyojua kuna mambo mengi sana bila kusahau utani bila kusahau maneno ya umbeya.
 Sasa shida itakuja kama mmoja wenu anapenda kusikiliza maneno ya watu na pia wivu, wewe kama umekubali kufanya kazi ofisi moja na mpenzio basi punguza wivu pia usisikilize maneno ya watu, Kwasababu maneno ya pembeni huwa hayakosekani especially mpenzio awe ndo mtu wa kutaniana na watu.

Ngao yenu kubwa ni mazungumzo, kama mtakuwa huru kuzungumza chochote basi hakika mtafika mbali pia jaribu kupunguza wivu hata kama unamuona mwanaume wako anamshika mfanyakazi mwengine kiuno huku wanacheka, we assume wapo katika matani then mkifika home sasa mkae chini mzungumze vinginevyo wala hamfiki kokote kwasababu kwenye maofisi kuna changamoto nyingi sana.

Kingine epuka kuwa na mahusiano ya karibu na bosi wako ilihali mpenzio naye anafanya kazi hapo, itamfanya ajisikie vibaya kwani atakuwa anahisi moja kwamoja bosi anatumia cheo chake kukurubuni na mwisho wa siku mmoja wenu ataona kazi chungu na atajikuta hana kazi bila sababu zozote za msingi.

Asanteni sana, wala sijamlenga mtu msinirushie mawe mtoto wa mwenzenu au kama vipi CHOMA GANZI

www.jescatarimo.blogspot.com

Friday, September 21, 2012

Mwanaume kutokuwa Smart nini shida?

Nitakushangaa sana wewe mwanamke unamuona mumeo anaondoka lakini kavaa nguo ya ajabu.

Hivi kweli kabisa kwa moyo mweupe bila hata kutikisika mumeo anatoka nyumbani anaenda kazini shati limejikunja halijanyooka vizuri, au chafu halijafuliwa au ndo kalirudia la jana tena linanuka jasho ukimuangalia miguuni viatu vichafu tena mwingine hata nywele hajachana mindevu imekaa tu ovyo?!!

Unajisikiaje unapopita barabarani ukiwaona wanaume wengine wako smart halafu mumeo ndo vile?? Tena wengine wanavaa hadi mashati yaliyochanika au soksi zilizotoboka, we hauoni kama unajiaibisha wewe?

Hakikisha havai soksi iliyotoboka wa kutoa harufu!

Kumbuka yeye ni mwanaume hana shida yeye kichwa chake kinawaza wapi apate pesa familia ikae vizuri kwa hiyo usipomwangalia anaweza kwenda kazini hata na kaptula, jukumu la mavazi ni lako wewe mwanamke hata kama na wewe unamajukumu ya watoto ila kumbuka mume ndo mtoto mkubwa naye anapaswa kuangaliwa kama hao wadogo kabla hajaondoka mtupie jicho mumeo, sio umchunguze?la hasha muangalie tu nguo alizovaa je ni zile ulizompangia avae?? kama siyo zinaendana?hazina kasoro? Manake wewe ndo utakuwa unazijua nguo zake kuliko hata yeye mwenyewe, usikubali mumeo atoke ndani kavaa shati la njano, tai ya blue, suruali ya kijani viatu vya brown. Soksi zinanuka hatari. Huoni aibu wewe?? Hakikisha soksi za mumeo ziko katika mpangilio na hazijatoboka manake wao wakiona soksi wanavaa tu hata kama zimetoboka au chafu wao hawajali tena na kama ziko tofauti anavaa hivyohivyo hawana muda wa kuangalia soksi nyingine iko wapi, na  kama mume wako muwazi atakwambia "uwe unaniandalia nguo"! sasa hili ni tusi kwa mwanamke, haupaswi kukumbushwa majukumu yako, japo kuna wanaume wengine wanakujipenda, yeye hata usipomchagulia nguo atajing'arisha mwenyewe.
Mwanaume akiwa smart anavutia!

Hivi hujisikii raha watu wakimsifia mumeo alivyosmart? hujisikii raha hata kumtambulisha kwa mtu 'jamani huyu ndo mume wangu'

Wengi mtasema mnaogopa kuibiwa, asikwambie mtu mwanaume hapendewi mavazi kwahiyo watu wakiamua kukuibia watakuibia tu!

Hili ndo langu la Ijumaa, najua sana kuna watu litakuwa limewauma kama ni mmoja wao CHOMA GANZI!
Kama siyo basi freshh! Endelea kuvisit www.jescatarimo.blogspot.com

Ijumaa njema

Thursday, September 20, 2012

Unapiga kelele wakati wa tendo?Soma hapa

Hili najua litakuwa linatugusa wengi!

Utamu bwana nikitu kingine asikwambie mtu, pata picha unawashwa sehemu yoyote ile kwenye mwili wako mfano mkononi halafu unakucha kidogo ndefu jinsi unavyojikuna unaonaje raha yake? Tena hapo ukute muwasho ndo umekushika balaa, dah yani kama nakuona unavyojikuna huku unafumba macho assshhhh! Unasikia raha eenh?? Haya sasa nadhani hapo mtanielewa kitu nitakachokiongelea hapa

Kila mtu anajinsi anavyoreact anapojisikia furaha, hasira, wivu, uchungu na hata utamu, sasa mimi naongelea utamu wetu uleeee! Unakunwa na mtu hadi unajihisi uko dunia nyingine unajikuta bila kutegemea unatoa kelele tena mwingine hadi kulia kabisa, mwingine yeye wala hatoi sauti atafumba zake macho tu huku anausikilizia utamu.

Sasa kama unajijua wewe ni wa kupiga kelele tena zile za sauti kubwa basi ni vizuri ukafungulia redio na kama ikiwezekana hakikisha wakati unataka mautamu nyumba haina watu haswa watoto.
Najua wengi mtasema hili haliwezekani kama haiwezekani basi wakati mnaendelea na utamu vuta shuka au mto kuwa kama unaung'ata huo mto au hilo shuka, kidogo itasaidia sauti isisikike nje. Pia kama mtakuwa katika pozi ambalo midomo yenu inaweza kukutana wakati utamu unaendelea ni vizuri mpenzio au mzinzi mwenzio akawa anakunyonya ulimi basi hapo sauti itaishilia mdomoni mwake na pia itazidi kuongeza msisimko kwake!

Ila maswala ya USWAZI chumba kimoja wewe kinachofuata mpangaji mwingine halafu huna hata kiredio au umeme ndo umekatika mnapiga gemu sauti wanazisikia wao sio vizuri unawaletea kero na mwisho wa siku mtajikuta mnapigwa chabo!

Umelipata ndugu yangu? milio kwenye sita kwa sita ina raha yake. Pale unapojisikia utamu jiachie tu!! Muache mwenzio ajue anakupagawisha kiasi gani!!!

Hilo ndo langu la leo.

Limekuuma?? Kama kawa CHOMA.......................???

Wednesday, September 19, 2012

Utambulisho

Hii ni kwa watu wote, watu wengi sana wanapenda kutambulishwa na wapenzi wao kwa watu wao wa karibu au marafiki zao pindi wakutanapo nao.

Hujisikia sana kupendwa pindi umtambulishapo kwa watu wako, mfano;mmetoka mmeenda sehemu kukaa kwa chakula au drinks mara wakatokea marafiki au ndugu mkawa mnajumuika nao kitendo cha wewe kuwaambia watu wako jamani huyu mpenzi wangu(tena wengi hupenda kuitwa mke/mume hata kama hawajaoana) huwa anajisikia raha sana na utaona tu jinsi atakavyoongeza mapenzi.

Ila kuna utambulisho mwingine unaweza kumfanya akajisikia vibaya mfano, unamtambulisha jamani huyu anaitwa fulani(unataja jina lake) halafu unamwambia na yeye hawa ndugu zangu au marafiki zangu, hapo lazima atajisikia vibaya ataona kwamba wewe kumbe huna future naye yoyote na wala humpendi ataanza kufikiria upo naye kwaajili ya ngono tu au unaona aibu kumtambulisha kwa vile labda anakuaibisha yeye mbaya au kavaa vibaya...Ni wengi sana huwa na mawazo haya japo huwa si kweli. Sasa kwa ushauri tu kama mpenzi wako si muelewa bora tu usimtambulishe waache wasalimiane basi! ila kama mpenzi wako muelewa basi we mtambulishe tu kwa jina au kama rafiki sababu najua kuna sababu za wewe kutomtambulisha kama mpenzi kutokana na kwamba labda bado hujaamua kuweka wazi au bado hamjajuana sana na sababu nyingine nyingi.

Nakuja kwa wewe ambaye unataka kutambulishwa ni vizuri ukawa muelewa sababu ukijifanya kuchukia kisa hujatambullishwa mwenzako atakushangaa kwanini unataka kurush vitu na hapo utajikuta unaharibu mambo.

Ila kama kweli unampenda mpenzi wako na hakuna unachomficha kwanini usimtambulishe kwa watu wako wa karibu? Atajisikia raha sana na atazidi kukupenda na atazidi kuwa huru na wewe!

Hapo najua nimewagusa wanaume wengi kwasababu wao ndo wagumu wa kutambulisha, manake jana katambulisha mwingine, juzi mwingine na leo tena mwingine watu watamshangaa ndo maana huwa wanakuwa wagumu kweli

Kama vipi CHOMA GAAAAANZI!

Ahsante!

Monday, September 17, 2012

Simpendi huyu!

Nadhani ni mmoja ya watu ninao wachukia tena kazidi kunikera kwa kuwa aliyemtukana ni Kiba . Naombeni msome ujinga huu wa TID


TID


"ALLY KIBA NA MAMA YAKE WANAMAMBO YA

KIJINGA SANA"......HILI NI TUSI LA TID

Baada ya kukabiliwa na scandal kubwa ya
kupanga njama za kumuua Ali Kiba, Khalid
Mohamed aka Top in Dar, amezungumza na
kusema Ali Kiba na mama yake wamekosa la kufanya na anawaona wajinga wakubwa. Akizungumza kwenye kipindi cha Tagz Weekly
cha DTV, msanii huyo amesema huenda Ali Kiba
alienda kwa mganga ambaye alimwambia TID
anataka kumuua. Msanii huyo wa ‘Nyota Yangu’ aliongeza kuwa
kutokana na kusingiziwa kitu asichokijua, kamwe
haiwezi ikatokea siku atampigia tena simu Ali Kiba
Ali Kiba(left) & TID(right)
aliyekuwa mshikaji wake wa karibu. “Siwezi naogopa,” alisema. “Naweza kumpigia simu nikaambiwa sasa ndo natamtafuta kumuua, achana naye tu mwache yeye aendelee na vitu vyake, because I felt he and his family were up to it, mama yake namuona sana, najua mama yake hanijui hajawahi kuniona hata siku moja. Ali Kiba kwa kitu gani ambacho amefanya yeye mimi nimfanyie baya? Nipo na watu kibao pale nao wamejilist eti nataka kuwaua sasa mimi hela ngapi nitatoa kuwaua watu wote wale? For what purpose watu kibao wamejilist. Am not gonna tell you what reactions I’m gonna do, I’m keeping it to myself, I aint gonna talk about it, seriously they are stupid, yaani they should come up with the best concept.” Pia Top In Dar alisema ameshakutana na Diamond
ambaye amesema hata haelewi kinachoondelea
na hana tatizo naye.
Ali Kiba

Saturday, September 15, 2012

Kuna umuhimu wa kumtajia mpenzi watu waliokutongoza?

Japo si vizuri kufichana mambo wewe na mpenzi wako ila si kila kitu unatakiwa umwambie, kwasababu binadamu tumetofautiana kuna mwingine hana shida akijua watu ambao wameshakutongoza ila mwingine inakuwa kidogo shida japo hatosema, kwanza kwanini umwambie lazima ujifunze kuhandle vitu vidogo kama hivi

Kumbuka kwamba kutongoza siyo kosa wala usimchukie anayekutongoza kwasababu majibu unayo wewe kukubali au kukataa. Wewe ndo umebeba maamuzi yote ya kusema YES or NO.

Si vizuri kumwambia mpenzi wako kila mtu anayekutongoza haswa ambao atakuwa anafahamiana nao au marafiki zake kwasababu inamadhara yafuatayo
1. Kama mpenzi wako ana wivu sana basi mahusiano baina ya watu hao wawili au kama ni marafiki utavunjika

2. Unazidi kumjengea mazingira ya wivu mpenzi wako bila we mwenyewe kujijua

3. Unajikosesha uhuru wako bila kujijua kwasababu akishaona unafuatiliwa sana ataanza kuongozana na wewe kila mahali ambapo unataka uende, usipopokea simu itakuwa ugomvi au akikukuta upo na mtu yoyote hata pengine ni ndugu yako halafu yeye hamfahamu atahisi unatongozwa au unamahusiano naye kutokana na namba 2 hapo juu yani umeshamjengea wivu

4. Kwenye mikutano yake na marafiki zake utakuwa huendi kama zamani sababu atakuwa anaogopa kuibiwa

Madhara yapo mengi tu kuendana na mtu atakavyolichukulia hili swala, tena mwingine anaweza hata kukuacha manake atakuwa anajiuliza kwanini utongozwe wewe tu kila siku au ndo unajirahisisha kumbe mtoto wa watu wala.

Kama nilivyosema hapo juu watu tunatofautiana mwingine anapenda aambiwe ili tu ajue so ni vizuri kumsoma mpenzi wako ni wa aina gani sio tu unakurupuka unaanza kusema fulani na fulani wamenitongoza leo.

Ila kuna wale ving'ang'anizi wa kutongoza hata umkatalie vipi yeye bado yumo tu ukiona anakupanda kichwani bora tu umwambie mpenzio ili siku ya siku asije akashuhudia mwenyewe ikawa balaa!

Hilo ndo langu la leo lilionijia kichwani na upeo wangu unavyonituma, kama utakuwa na wazo lako tofauti basi tupia

Leo hakuna ganzi dawa zimeisha mahospitalini ila nadhani hakuna mtu limemuuma.
Basi pouwa!


Wednesday, September 12, 2012

Kisa cha kweli!

Kuna siku niliongelea wivu na madhara yake, sasa leo naongezea jambo ambalo nimeliona hivi karibuni, na hii ikiwa ni matokeo ya wivu.

Kuna dada mmoja alikuwa na wivu sana kwa mumewe alikuwa akihisi mumewe anawanawake zake wa nje, japo kwa upande mwingine ni kweli yule jamaa ana wanawake wengi tu ambao huwa anaburudika nao akishatoka kwa ofisi na wakati mwingine anachelewa hadi kurudi nyumbani, sasa hichi kitu kilikuwa kinamuumiza sana huyu dada(mke) . Japokuwa hakuna ushahidi wowote ule ila alikuwa tu akihisi mumewe anamchezea rafu.

Akajaribu kutumia njia ya marafiki wamchunguze ila kwa kuwa jamaa ni very smart hawakupata kitu walimpa tu jibu mumeo huwa anatoka na marafiki zake tu then anarudi home. Lakini yule dada(mke) bado hakutaka kuamini ndipo siku moja akamuamulia,

Ijumaa moja asubuhi jamaa akaaga kwenda kazini kama kawaida na akamwambia wife leo nitachelewa kidogo kurudi ila hakumpa sababu na wife nae akamwambia leo naenda kwenye kitchen party nami nitachelewa kurudi, basi mume akaondoka. Ilipofika mida ya saa 10 mke akachukua taxi bubu akaenda maeneo ya karibu na ofisi ya mumewe akapaki gari imefika saa 11 kasoro akamuona mumewe anatoka ofisini, wakaanza kumfuatilia hadi wakafika maeneo ya Uhuru park kinondoni. Mumewe akatafuta mahali akakaa baada ya muda wakaja marafiki zake mumewe wakaendelea kujumuika yeye(mke bado anamfuatilia hapo)
Hapo usiku umeingia, katika kuendelea kuchunguza mara akatokea mume wa shostito wake wakaanza kusalimiana huyo shemeji mtu akamwambia rafiki yako yupo ndani mango garden twende ukamsalimie na ukae japo kidogo, sasa kwavile hakutaka huyo shemeji ajue lolote ikabidi tu amdanganye kwamba kaja kuenjoy kidogo tu halafu anarudi home so ikabidi akubali, wakawa wanasubiri magari yapite waweze kuvuka barabara upande wa pili ili waingie mango. Kumbe huku mumewe kanyanyuka anataka kuondoka ndo mara anamuona wife yupo na jamaa wanavuka barabara na jamaa wala hamjui. Si ndo akaanza kuwafuata? Ile jamaa anataka kulipia kiingilio tu mume huyu hapa, kawaka kafura bila kuuliza kitu, ngumi zikarushwa na yule shemeji nae ili kujitetea akarusha ngumi basi pakawaka kweli! Baada ya kuamuliwa jamaa akaenda kuwasha gari yake hadi home, ikabidi mwanamke achukue ile taxi bubu aliyokuja nayo hadi home. Kwakuwa jamaa alikuwa keshafika akaiona ile gari ikiondoka so moja kwa moja akajua mkewe kaletwa na yule jamaa.

Kibaya zaidi mkewe alivyoondoka alibeba nguo za harusi kwa mawazo yake ni kuwa akiwa anarudi azivae mumewe aamini alitoka kwenye kitchen party, sasa ameingia ndani mumewe kumkagua begi lina nguo.

Sitaki kukwambia kilitokea nini ila baada ya kutengana kwa mwezi mmoja ndoa ikaja kusuluhishwa na familia zote mbili akiwepo yule shosti yake na mume wa shosti

Sasa isingekuwa kuchunguzana haya yangetokea????



Is It true??Hahahahaaaa



Tuesday, September 11, 2012

Jua madhara ya kukaa na mtoto baa

Watoto hufurahia beach
Ni jambo jema sana kumtoa mtoto out, ila ubaya unakuja ni wapi unampeleka? Sasa utakuja mzazi mwingine hata hajui mtoto ampeleke wapi ili aweze kuenjoy anachojua yeye wapi atatoka naye ambapo kutakuwa na marafiki zake anywe ulabu na mara nyingi mtu mwenye hizi fikra atampeleka mtoto baa tena ile ambayo imechangamka haswa ninaposema imechangamka nadhani mnanielewa yani kuna kila aina ya walevi akiamini mtoto atakula chips na soda atafurahi huku na yeye akiendelea na ulabu.

Sasa nikuulize unajua madhara yake? Unajua baada ya hapo mtoto wako ataondoka na nini? Kitu cha kwanza magonjwa asipopata UTI basi ataumwa tumbo, UTI ataipata chooni coz kila mtu anajua vyoo vya baa kila mtu anaingia na ustaarabu unakuwa hakuna na tumbo ataumwa kwasababu ya chakula baa kinapikwa chakula cha walevi wanavyopika wanajua we mlevi huwezi hata kukichunguza kama chakula kiko sawa kama nyama utakuta haijaiva vizuri na kama chips utakuta ni za baridi zilizonyonya mafuta mengi.

Watoto hufurahi wakiwa na wenzao
Sasa kama haitoshi mtoto atajifunza mengi sana kwenye baa na atasikia mengi sana kama matusi atashuhudia maugomvi atashuhudia tabia za ajabu ajabu sasa hapo ndo manzo wa mtoto kuharibikiwa kimaadili bila wewe mwenyewe kujijua fikiria katika maisha yake ya utoto umeenda naye sehemu hizo mara 10 baadaye atakuwa mtoto wa namna gani? Unadhani hatokuwa mlevi? Tena mwingine hadi saa sita za usiku bado yupo naye tu, hivi huoni kama unamtesa huyo mtoto?


Kuna sehemu nyingi sana ambazo unaweza ukakaa na mtoto mdogo ila jitahidi usiwe kwenye vilabu vya pombe tena isiwe usiku. Unaweza kumpeleka beach au sehemu yoyote yenye michezo ya watoto mbona sehemu zote hizi wanauza vilevi ambavyo unaweza kunywa wakati mtoto wako anacheza?Tena wanakuwa na vyakula vizuri sana kwa watoto na ukishaona mtoto kaenjoy vya kutosha mrudishe nyumbani wewe uendelee na mambo yako ukitaka hata kulala huko we lala lakini amepumzika nyumbani.

Nimeliona hili zaidi y mara tano na ndiyo maana leo nimeamua niliseme tu. Sidhani kama haki ya mtoto inaruhusu hii

Asanteni sana nadhani mtazingatia hili

Kama vipi choma ganzi


Kununanuna si kuzuri!

Kuna watu huwa nashindwa kuwaelewa wanamatatizo gani, sijui wamezaliwa hivyo au sijui kujifanyisha?
Au ndo unataka kuniambia wivu? Manake utakuta mtu kanuna siku nzima, alichonunia hakieleweki tena hii ipo sana kwa watoto wa kike.

Siwezi kukataa wakati wa hedhi wasichana wengi wanakuwa na kama hasira hasira hivi, hii ni kawaida na hapa wala siwaongelei hawa ila mtu hayupo kwenye hedhi wala hajakosewa na mtu lakini basi tu kavimba mdomo kautunisha loh! Yani hata kama unakitu muhimu unataka umwambie unajikuta unaahirisha.

Ila kuna mwingine wivu tu akikuona umependeza zaidi yake kosa, lazima anune. Au akikuona unagari mpya au mambo yako yanafanikiwa tu yeye huku keshavimba, tena utashangaa tu ule uchangamfu hata haupo tena na kama urafiki unaweza hata kufa, sasa ulitaka mwenzake asande siku zote?

Au mwingine kitu kidogo tu kakosewa na rafiki au mpenzi wake au hata barabarani kapita kachokozwa na wamachinga basi yeye atamnunia kila mtu, Siyo vizuri hivyo ndugu yangu punguza kununa mtoto wa kike hutakiwi kuwa hivyo na hata wewe mwanaume kama kweli we rijali hupaswi kununa umekosewa kuwa wazi ongea mwambie mwenzako la moyoni mmalize maisha yaendelee ukinuna jua unajikosesha amani mwenyewe ndugu yangu, tena si amani tu na bahati pia mfano kama kuna jambo zuri mtu anataka akueleze kama la bishara sasa anakuja anakuta umenuna unavyodhani atakwambia? Kwanza wengi huwa hatupendi kufanya kazi au kuishi na watu wa aina hii badilika ndugu eeenh?? Mjini hapa, shauri yako unajizibia bahati kwa kununanuna.

Cheka babu hata kama huna senti mfukoni yanini kumuonesha mtu udhaifu wako?
JT
Limeuma choma ganzi

Friday, September 7, 2012

Acha Dharau!

Inakuwaje hadi unamdharau binadamu mwenzako ambaye wote mmekuja kwa njia moja, wote mmelala kwenye matumbo ya mama zenu kwa miezi tisa?

Naomba nikwambie ndugu yangu maisha bado yanaendelea huyo unayemdharau hujui atakuwa nani kwako hapo baadaye, tena usimdharau mtu usiye mjua. Kuna wengine wanadharau majirani zao eti sababu wao wananyumba nzuri ukivamiwa na majambazi au ukiunguliwa na nyumba utapata wapi msaada?

Mwingine especially wasichana wanapenda kudharau sana wamama wanaokutana nao barabarani au kwenye mabasi na mara nyingi huwa wanawajibu ovyo sasa jiulize siku huyo bf wako anaenda kukutambulisha kwao unakutana na sura ya huyo mama utafanyaje? utakimbia au utainama chini??
JT

Kingine kwa wapenzi, kuna watu wanapenda sana sifa mbele ya rafiki zao kama ni mpenzi wako wa zamani ukikutana naye akiwa mwenyewe anakuwa mdogooooo kama nukta, anakuwa mstaarabu kweli sasa awe na ndugu au rafiki, hizo nyodo na dharau atakazo kuonyesha utashangaa wakati siku mbili zilizopita mlipokutana wala hakuwa hivyo sasa nashindwa kuelewa ni kwamba anataka ajioneshe kwamba yeye kidume?au ajifanye na aonekane yeye ndo alikuacha au vipi? Tena hapo ukute yeye ndo kaachwa kutokana na mitabia yake. Ndugu yangu acha dharau ukitaka kumuonesha dharau hata yeye anao uwezo wa kufanya hivyo. Hakuna mtu asiyejua kumuonesha mtu dharau isipokuwa tu wengine hawapendi kufanya hivyo. Nyie kama mmetemana temaneni mambo ya dharau ni us***e, halafu aibu kwa mtoto wa kiume unafanya mambo kama choko bwana! Eti utakuta mwingine anakupandisha na kukushusha kwa macho huo uswahili, mwanaume kamilifu hawezi fanya hivyo mimi mwenyewe wa kike lakini sifanyi hivyo.

Maisha bado yanaendelea kama mmeshindwana basi, yeye anawake na wewe unawako sasa yanini kuingiliana??

Wala sifichi ni kweli nimekulenga wewe, kama mawe tupa tu...au kama vipi CHOMA GANZI



Tuesday, September 4, 2012

Barua ya Loveness Diva



Hii ni barua ya Diva aliyoiandika kwenye blog yake kwa fans wake ambayo imenikuna hasa ukifikiria i don't like this lady naomba muisome

BARUA YANGU YA MWEZI MZIMA TO MY FANS : SIPENDI MARAFIKI KABISA HASA WA KIKE




Nimeona niandike hii kwanza labda itasaidia sana mambo yawasichana kutaka sana urafiki na mimi.
guys me sipendi urafiki kabisa na watoto wa kike , had a friend once ilini cost sana nilipotofautiana nae na because nilimuamini sana niliumia , that was high school , then from there on sitaki sana marafiki kusema za ukweli....sio mtu wa marafiki wala mtu wa mazoea ya ovyoovyo na wala siringi but sipendi tu najua matatizo yake hasa kwa watoto wa kike!!
i always miss my high school friends, they were dope yaani compared na ambao nakutana nao hivi karibuni , na kuhusu kuchagua marafiki nachagua sana wa kiume, this is not a joke but napatana sana na soudy brown gossipcpotz ,licha ya kunishauri alot about life but ni mpole , mstaarabu sana na ana imani ya dini kama mimi , so tunapatana sana na nadiriki kusema thats my best friend , he actually knows good and bad , knows if am not ok and when am ok!! na apart from kuwa my manager but he is good hearted , my mentor pia
tunapatana sana thats why hata tulipoenda Tanga he was the only person niliempeleka home akamsalimie my aunt and it was awesome and good sana. he such a friend like i never had

 girls got issues sana ambazo to me siwezi kabisa kukaa na hizo issues zao ,wengi wanapenda umbea ,kuongea vitu visivyowahusu, kusingizia mambo ya ajabu coz me yaani nina atittude basi i have to stay away kabisa sehemu penye wasichana hasa ambao wana tabia za kike ,ambao masaa24 wanazungumzia wanaume na jinsi ya kuwachuna , wanaokaa kusema wenzao coz ikno na mimi nikitoka watanisema asa mi nikae nao wanini si bora nikae na simu yangu busy na twitter



nahisi mind za wanaume ziko active compared na wasichana wengi wa mjini
kiukweli sihitaji marafiki................nahitaji marafiki wachache tena wa kiume wataoniambia which is good , which is bad 
am Proud kujuana na soudy brown,b12,baba johny,dommy,faraja ,venture ,peter mo and the rest
feel safe around hawa my brothers 
God is good ..................kuwa my fan , be that and pliz endelea kuwa hivyo na will make u happy in my show but nje ya hapo , my life is different , very strictly and ku avoid that am always at home after work and sina rafiki celebrity wa kike sina kabisa ukweli ndo huo.
and am totally avoiding girls sio wote lakini wenye drama wachache wakike ninaojuana nao wa kike wananitosha LOL
MONTHLY LETTER TO MY FANS 
THANKU
Yours
Lovely Diva

Hayo ndo maneno Diva wa clouds kwa fans wake, HATAKI MARAFIKI WA KIKE  EEENH? SO MSIMFUATEFUATE MUACHENI NA LIFE YAKE. Kwangu mi njooni tu ukinizingua nitakuchana wala sitakuogopa Mi nahitaji marafiki nahitaji kujua wenzangu wanafanya nini na wanafikiri nini ili na mimi nifanye nini nifikiri nini, nahitaji kujua maisha ya wengine na kujifunza toka kwa wengine hivyo sitaweza kufanikisha hilo hadi niwe na marafiki! Kwani umbeya kitu gani bwana wakikusema kwakitu ambacho hujafanya unadhurika nini?? Mungu wako ndo anayekujua ndani nje.

Msinitumpie mawe jamani ni mawazo yangu tu na wala msimtupie mawe Diva ni mawazo yake na ndivyo apendavyo, so kama na wewe una yako tupia hapo chini! 

Saturday, September 1, 2012

Utamu wa Sikio

Sikio sikio sikio!

Sikio bwana linasisimua sana kama ukilipatia, ila linaumiza sana kama ukilikosea.

Sikio linatekenywa taratibu kwa kidole cha nne kama una vidole vinene tumia kidole kidogo cha mwisho na kama vidole vyako vyote vinene basi acha tumia tu ulimi, manake utakuta mwingine mavidole manene lakini kakazana kuingiza masikioni aaah bwana hapo unamuumiza mwenzio wala hasikii chochote!

Ulimi lazima ukunjwe kuweka angle
Kumbuka ngozi ya sikio ni laini sana sasa ukiwa unaingiza kidole chako hakikisha unaingiza taratibu bila haraka wala papara tena unakuwa kama unapapasa sio kama unasugua manake mwingine anataka akusugueee mpaka uumie.

Kingine ambacho ndo kizuri zaidi tumia ulimi wako, pia hapa nako usitake kutumbukiza liulimi lako lote lizimalizima hata kama unaulimi wa aina gani ni lazima uukunje ulimi wako utengeneze kama ncha kwa mbele halafu taratiiiiibu unaingiza kwa sikio tena unaanzia nje unazungusha ulimi wako then unaingiza ndani narudia tena taratibu kama unapapasa tu tena inaleta mvuto zaidi kama utakuwa kama unahemea kidogo ndani coz ule mvuke na joto la mdomo wako huleta msisimko ILA hakikisha humjazi mate mwenzako yani hapo mate hayahusiki kabisa so jitahidi usimpake mate mwenzio manake hilo ni sikio lazima uwe nalo makini sawa???

Umenipata?

Nawatakia week end njema!