Kuna siku niliongelea wivu na madhara yake, sasa leo naongezea jambo ambalo nimeliona hivi karibuni, na hii ikiwa ni matokeo ya wivu.
Kuna dada mmoja alikuwa na wivu sana kwa mumewe alikuwa akihisi mumewe anawanawake zake wa nje, japo kwa upande mwingine ni kweli yule jamaa ana wanawake wengi tu ambao huwa anaburudika nao akishatoka kwa ofisi na wakati mwingine anachelewa hadi kurudi nyumbani, sasa hichi kitu kilikuwa kinamuumiza sana huyu dada(mke) . Japokuwa hakuna ushahidi wowote ule ila alikuwa tu akihisi mumewe anamchezea rafu.
Akajaribu kutumia njia ya marafiki wamchunguze ila kwa kuwa jamaa ni very smart hawakupata kitu walimpa tu jibu mumeo huwa anatoka na marafiki zake tu then anarudi home. Lakini yule dada(mke) bado hakutaka kuamini ndipo siku moja akamuamulia,
Ijumaa moja asubuhi jamaa akaaga kwenda kazini kama kawaida na akamwambia wife leo nitachelewa kidogo kurudi ila hakumpa sababu na wife nae akamwambia leo naenda kwenye kitchen party nami nitachelewa kurudi, basi mume akaondoka. Ilipofika mida ya saa 10 mke akachukua taxi bubu akaenda maeneo ya karibu na ofisi ya mumewe akapaki gari imefika saa 11 kasoro akamuona mumewe anatoka ofisini, wakaanza kumfuatilia hadi wakafika maeneo ya Uhuru park kinondoni. Mumewe akatafuta mahali akakaa baada ya muda wakaja marafiki zake mumewe wakaendelea kujumuika yeye(mke bado anamfuatilia hapo)
Hapo usiku umeingia, katika kuendelea kuchunguza mara akatokea mume wa shostito wake wakaanza kusalimiana huyo shemeji mtu akamwambia rafiki yako yupo ndani mango garden twende ukamsalimie na ukae japo kidogo, sasa kwavile hakutaka huyo shemeji ajue lolote ikabidi tu amdanganye kwamba kaja kuenjoy kidogo tu halafu anarudi home so ikabidi akubali, wakawa wanasubiri magari yapite waweze kuvuka barabara upande wa pili ili waingie mango. Kumbe huku mumewe kanyanyuka anataka kuondoka ndo mara anamuona wife yupo na jamaa wanavuka barabara na jamaa wala hamjui. Si ndo akaanza kuwafuata? Ile jamaa anataka kulipia kiingilio tu mume huyu hapa, kawaka kafura bila kuuliza kitu, ngumi zikarushwa na yule shemeji nae ili kujitetea akarusha ngumi basi pakawaka kweli! Baada ya kuamuliwa jamaa akaenda kuwasha gari yake hadi home, ikabidi mwanamke achukue ile taxi bubu aliyokuja nayo hadi home. Kwakuwa jamaa alikuwa keshafika akaiona ile gari ikiondoka so moja kwa moja akajua mkewe kaletwa na yule jamaa.
Kibaya zaidi mkewe alivyoondoka alibeba nguo za harusi kwa mawazo yake ni kuwa akiwa anarudi azivae mumewe aamini alitoka kwenye kitchen party, sasa ameingia ndani mumewe kumkagua begi lina nguo.
Sitaki kukwambia kilitokea nini ila baada ya kutengana kwa mwezi mmoja ndoa ikaja kusuluhishwa na familia zote mbili akiwepo yule shosti yake na mume wa shosti
Sasa isingekuwa kuchunguzana haya yangetokea????
No comments:
Post a Comment