Hivi kweli kabisa kwa moyo mweupe bila hata kutikisika mumeo anatoka nyumbani anaenda kazini shati limejikunja halijanyooka vizuri, au chafu halijafuliwa au ndo kalirudia la jana tena linanuka jasho ukimuangalia miguuni viatu vichafu tena mwingine hata nywele hajachana mindevu imekaa tu ovyo?!!
Unajisikiaje unapopita barabarani ukiwaona wanaume wengine wako smart halafu mumeo ndo vile?? Tena wengine wanavaa hadi mashati yaliyochanika au soksi zilizotoboka, we hauoni kama unajiaibisha wewe?
Hakikisha havai soksi iliyotoboka wa kutoa harufu! |
Kumbuka yeye ni mwanaume hana shida yeye kichwa chake kinawaza wapi apate pesa familia ikae vizuri kwa hiyo usipomwangalia anaweza kwenda kazini hata na kaptula, jukumu la mavazi ni lako wewe mwanamke hata kama na wewe unamajukumu ya watoto ila kumbuka mume ndo mtoto mkubwa naye anapaswa kuangaliwa kama hao wadogo kabla hajaondoka mtupie jicho mumeo, sio umchunguze?la hasha muangalie tu nguo alizovaa je ni zile ulizompangia avae?? kama siyo zinaendana?hazina kasoro? Manake wewe ndo utakuwa unazijua nguo zake kuliko hata yeye mwenyewe, usikubali mumeo atoke ndani kavaa shati la njano, tai ya blue, suruali ya kijani viatu vya brown. Soksi zinanuka hatari. Huoni aibu wewe?? Hakikisha soksi za mumeo ziko katika mpangilio na hazijatoboka manake wao wakiona soksi wanavaa tu hata kama zimetoboka au chafu wao hawajali tena na kama ziko tofauti anavaa hivyohivyo hawana muda wa kuangalia soksi nyingine iko wapi, na kama mume wako muwazi atakwambia "uwe unaniandalia nguo"! sasa hili ni tusi kwa mwanamke, haupaswi kukumbushwa majukumu yako, japo kuna wanaume wengine wanakujipenda, yeye hata usipomchagulia nguo atajing'arisha mwenyewe.
Mwanaume akiwa smart anavutia! |
Hivi hujisikii raha watu wakimsifia mumeo alivyosmart? hujisikii raha hata kumtambulisha kwa mtu 'jamani huyu ndo mume wangu'
Wengi mtasema mnaogopa kuibiwa, asikwambie mtu mwanaume hapendewi mavazi kwahiyo watu wakiamua kukuibia watakuibia tu!
Hili ndo langu la Ijumaa, najua sana kuna watu litakuwa limewauma kama ni mmoja wao CHOMA GANZI!
Kama siyo basi freshh! Endelea kuvisit www.jescatarimo.blogspot.com
Ijumaa njema
U-smart ni kipaji mamii, kuwa msafi ni mpaka ujiandae, na si kukurupuka! Na u-smart si kuvaa suruali ya kitambaa na shati la rangi moja kwa tai ya udhurungi!
ReplyDelete