Tuesday, September 11, 2012

Kununanuna si kuzuri!

Kuna watu huwa nashindwa kuwaelewa wanamatatizo gani, sijui wamezaliwa hivyo au sijui kujifanyisha?
Au ndo unataka kuniambia wivu? Manake utakuta mtu kanuna siku nzima, alichonunia hakieleweki tena hii ipo sana kwa watoto wa kike.

Siwezi kukataa wakati wa hedhi wasichana wengi wanakuwa na kama hasira hasira hivi, hii ni kawaida na hapa wala siwaongelei hawa ila mtu hayupo kwenye hedhi wala hajakosewa na mtu lakini basi tu kavimba mdomo kautunisha loh! Yani hata kama unakitu muhimu unataka umwambie unajikuta unaahirisha.

Ila kuna mwingine wivu tu akikuona umependeza zaidi yake kosa, lazima anune. Au akikuona unagari mpya au mambo yako yanafanikiwa tu yeye huku keshavimba, tena utashangaa tu ule uchangamfu hata haupo tena na kama urafiki unaweza hata kufa, sasa ulitaka mwenzake asande siku zote?

Au mwingine kitu kidogo tu kakosewa na rafiki au mpenzi wake au hata barabarani kapita kachokozwa na wamachinga basi yeye atamnunia kila mtu, Siyo vizuri hivyo ndugu yangu punguza kununa mtoto wa kike hutakiwi kuwa hivyo na hata wewe mwanaume kama kweli we rijali hupaswi kununa umekosewa kuwa wazi ongea mwambie mwenzako la moyoni mmalize maisha yaendelee ukinuna jua unajikosesha amani mwenyewe ndugu yangu, tena si amani tu na bahati pia mfano kama kuna jambo zuri mtu anataka akueleze kama la bishara sasa anakuja anakuta umenuna unavyodhani atakwambia? Kwanza wengi huwa hatupendi kufanya kazi au kuishi na watu wa aina hii badilika ndugu eeenh?? Mjini hapa, shauri yako unajizibia bahati kwa kununanuna.

Cheka babu hata kama huna senti mfukoni yanini kumuonesha mtu udhaifu wako?
JT
Limeuma choma ganzi

1 comment:

  1. Kuwa na furaha au kucheka kila mara pasipo kununa nacho ni kipaji, na si kila mtu huzaliwa na kipaji!

    ReplyDelete