Saturday, September 15, 2012

Kuna umuhimu wa kumtajia mpenzi watu waliokutongoza?

Japo si vizuri kufichana mambo wewe na mpenzi wako ila si kila kitu unatakiwa umwambie, kwasababu binadamu tumetofautiana kuna mwingine hana shida akijua watu ambao wameshakutongoza ila mwingine inakuwa kidogo shida japo hatosema, kwanza kwanini umwambie lazima ujifunze kuhandle vitu vidogo kama hivi

Kumbuka kwamba kutongoza siyo kosa wala usimchukie anayekutongoza kwasababu majibu unayo wewe kukubali au kukataa. Wewe ndo umebeba maamuzi yote ya kusema YES or NO.

Si vizuri kumwambia mpenzi wako kila mtu anayekutongoza haswa ambao atakuwa anafahamiana nao au marafiki zake kwasababu inamadhara yafuatayo
1. Kama mpenzi wako ana wivu sana basi mahusiano baina ya watu hao wawili au kama ni marafiki utavunjika

2. Unazidi kumjengea mazingira ya wivu mpenzi wako bila we mwenyewe kujijua

3. Unajikosesha uhuru wako bila kujijua kwasababu akishaona unafuatiliwa sana ataanza kuongozana na wewe kila mahali ambapo unataka uende, usipopokea simu itakuwa ugomvi au akikukuta upo na mtu yoyote hata pengine ni ndugu yako halafu yeye hamfahamu atahisi unatongozwa au unamahusiano naye kutokana na namba 2 hapo juu yani umeshamjengea wivu

4. Kwenye mikutano yake na marafiki zake utakuwa huendi kama zamani sababu atakuwa anaogopa kuibiwa

Madhara yapo mengi tu kuendana na mtu atakavyolichukulia hili swala, tena mwingine anaweza hata kukuacha manake atakuwa anajiuliza kwanini utongozwe wewe tu kila siku au ndo unajirahisisha kumbe mtoto wa watu wala.

Kama nilivyosema hapo juu watu tunatofautiana mwingine anapenda aambiwe ili tu ajue so ni vizuri kumsoma mpenzi wako ni wa aina gani sio tu unakurupuka unaanza kusema fulani na fulani wamenitongoza leo.

Ila kuna wale ving'ang'anizi wa kutongoza hata umkatalie vipi yeye bado yumo tu ukiona anakupanda kichwani bora tu umwambie mpenzio ili siku ya siku asije akashuhudia mwenyewe ikawa balaa!

Hilo ndo langu la leo lilionijia kichwani na upeo wangu unavyonituma, kama utakuwa na wazo lako tofauti basi tupia

Leo hakuna ganzi dawa zimeisha mahospitalini ila nadhani hakuna mtu limemuuma.
Basi pouwa!


3 comments:

  1. Sema mama wa maujanja wa chandibwa.......mzee wa geza

    ReplyDelete