Naomba nikwambie ndugu yangu maisha bado yanaendelea huyo unayemdharau hujui atakuwa nani kwako hapo baadaye, tena usimdharau mtu usiye mjua. Kuna wengine wanadharau majirani zao eti sababu wao wananyumba nzuri ukivamiwa na majambazi au ukiunguliwa na nyumba utapata wapi msaada?
Mwingine especially wasichana wanapenda kudharau sana wamama wanaokutana nao barabarani au kwenye mabasi na mara nyingi huwa wanawajibu ovyo sasa jiulize siku huyo bf wako anaenda kukutambulisha kwao unakutana na sura ya huyo mama utafanyaje? utakimbia au utainama chini??
JT |
Kingine kwa wapenzi, kuna watu wanapenda sana sifa mbele ya rafiki zao kama ni mpenzi wako wa zamani ukikutana naye akiwa mwenyewe anakuwa mdogooooo kama nukta, anakuwa mstaarabu kweli sasa awe na ndugu au rafiki, hizo nyodo na dharau atakazo kuonyesha utashangaa wakati siku mbili zilizopita mlipokutana wala hakuwa hivyo sasa nashindwa kuelewa ni kwamba anataka ajioneshe kwamba yeye kidume?au ajifanye na aonekane yeye ndo alikuacha au vipi? Tena hapo ukute yeye ndo kaachwa kutokana na mitabia yake. Ndugu yangu acha dharau ukitaka kumuonesha dharau hata yeye anao uwezo wa kufanya hivyo. Hakuna mtu asiyejua kumuonesha mtu dharau isipokuwa tu wengine hawapendi kufanya hivyo. Nyie kama mmetemana temaneni mambo ya dharau ni us***e, halafu aibu kwa mtoto wa kiume unafanya mambo kama choko bwana! Eti utakuta mwingine anakupandisha na kukushusha kwa macho huo uswahili, mwanaume kamilifu hawezi fanya hivyo mimi mwenyewe wa kike lakini sifanyi hivyo.
Maisha bado yanaendelea kama mmeshindwana basi, yeye anawake na wewe unawako sasa yanini kuingiliana??
Wala sifichi ni kweli nimekulenga wewe, kama mawe tupa tu...au kama vipi CHOMA GANZI
Teh tehee teheeeee, maumivu ya moyo hayapoi kwa ganzi!
ReplyDelete