Ni wengi sana wameshajiingiza katika mahusiano na mfanyakazi mwenzake yaani ofisi moja kwahiyo najua wengi litawagusa.
Ki ukweli kwa jinsi nilivyoona wengi waliodumu kwenye mapenzi haya hadi kufikia ndoa na ndoa zao zikadumu ni wazee wa zamani lakini si kizazi hiki cha sasa, japo wapo wachache ambayo wameweza kufikia malengo yao ila si wote.
Sasa naomba niwaelezee kwanini wengi hawajafika popote
Kwenye maofisi kama mnavyojua kuna mambo mengi sana bila kusahau utani bila kusahau maneno ya umbeya.
Sasa shida itakuja kama mmoja wenu anapenda kusikiliza maneno ya watu na pia wivu, wewe kama umekubali kufanya kazi ofisi moja na mpenzio basi punguza wivu pia usisikilize maneno ya watu, Kwasababu maneno ya pembeni huwa hayakosekani especially mpenzio awe ndo mtu wa kutaniana na watu.
Ngao yenu kubwa ni mazungumzo, kama mtakuwa huru kuzungumza chochote basi hakika mtafika mbali pia jaribu kupunguza wivu hata kama unamuona mwanaume wako anamshika mfanyakazi mwengine kiuno huku wanacheka, we assume wapo katika matani then mkifika home sasa mkae chini mzungumze vinginevyo wala hamfiki kokote kwasababu kwenye maofisi kuna changamoto nyingi sana.
Kingine epuka kuwa na mahusiano ya karibu na bosi wako ilihali mpenzio naye anafanya kazi hapo, itamfanya ajisikie vibaya kwani atakuwa anahisi moja kwamoja bosi anatumia cheo chake kukurubuni na mwisho wa siku mmoja wenu ataona kazi chungu na atajikuta hana kazi bila sababu zozote za msingi.
Asanteni sana, wala sijamlenga mtu msinirushie mawe mtoto wa mwenzenu au kama vipi CHOMA GANZI
www.jescatarimo.blogspot.com
No comments:
Post a Comment