Wednesday, September 19, 2012

Utambulisho

Hii ni kwa watu wote, watu wengi sana wanapenda kutambulishwa na wapenzi wao kwa watu wao wa karibu au marafiki zao pindi wakutanapo nao.

Hujisikia sana kupendwa pindi umtambulishapo kwa watu wako, mfano;mmetoka mmeenda sehemu kukaa kwa chakula au drinks mara wakatokea marafiki au ndugu mkawa mnajumuika nao kitendo cha wewe kuwaambia watu wako jamani huyu mpenzi wangu(tena wengi hupenda kuitwa mke/mume hata kama hawajaoana) huwa anajisikia raha sana na utaona tu jinsi atakavyoongeza mapenzi.

Ila kuna utambulisho mwingine unaweza kumfanya akajisikia vibaya mfano, unamtambulisha jamani huyu anaitwa fulani(unataja jina lake) halafu unamwambia na yeye hawa ndugu zangu au marafiki zangu, hapo lazima atajisikia vibaya ataona kwamba wewe kumbe huna future naye yoyote na wala humpendi ataanza kufikiria upo naye kwaajili ya ngono tu au unaona aibu kumtambulisha kwa vile labda anakuaibisha yeye mbaya au kavaa vibaya...Ni wengi sana huwa na mawazo haya japo huwa si kweli. Sasa kwa ushauri tu kama mpenzi wako si muelewa bora tu usimtambulishe waache wasalimiane basi! ila kama mpenzi wako muelewa basi we mtambulishe tu kwa jina au kama rafiki sababu najua kuna sababu za wewe kutomtambulisha kama mpenzi kutokana na kwamba labda bado hujaamua kuweka wazi au bado hamjajuana sana na sababu nyingine nyingi.

Nakuja kwa wewe ambaye unataka kutambulishwa ni vizuri ukawa muelewa sababu ukijifanya kuchukia kisa hujatambullishwa mwenzako atakushangaa kwanini unataka kurush vitu na hapo utajikuta unaharibu mambo.

Ila kama kweli unampenda mpenzi wako na hakuna unachomficha kwanini usimtambulishe kwa watu wako wa karibu? Atajisikia raha sana na atazidi kukupenda na atazidi kuwa huru na wewe!

Hapo najua nimewagusa wanaume wengi kwasababu wao ndo wagumu wa kutambulisha, manake jana katambulisha mwingine, juzi mwingine na leo tena mwingine watu watamshangaa ndo maana huwa wanakuwa wagumu kweli

Kama vipi CHOMA GAAAAANZI!

Ahsante!

No comments:

Post a Comment