Tuesday, September 11, 2012

Jua madhara ya kukaa na mtoto baa

Watoto hufurahia beach
Ni jambo jema sana kumtoa mtoto out, ila ubaya unakuja ni wapi unampeleka? Sasa utakuja mzazi mwingine hata hajui mtoto ampeleke wapi ili aweze kuenjoy anachojua yeye wapi atatoka naye ambapo kutakuwa na marafiki zake anywe ulabu na mara nyingi mtu mwenye hizi fikra atampeleka mtoto baa tena ile ambayo imechangamka haswa ninaposema imechangamka nadhani mnanielewa yani kuna kila aina ya walevi akiamini mtoto atakula chips na soda atafurahi huku na yeye akiendelea na ulabu.

Sasa nikuulize unajua madhara yake? Unajua baada ya hapo mtoto wako ataondoka na nini? Kitu cha kwanza magonjwa asipopata UTI basi ataumwa tumbo, UTI ataipata chooni coz kila mtu anajua vyoo vya baa kila mtu anaingia na ustaarabu unakuwa hakuna na tumbo ataumwa kwasababu ya chakula baa kinapikwa chakula cha walevi wanavyopika wanajua we mlevi huwezi hata kukichunguza kama chakula kiko sawa kama nyama utakuta haijaiva vizuri na kama chips utakuta ni za baridi zilizonyonya mafuta mengi.

Watoto hufurahi wakiwa na wenzao
Sasa kama haitoshi mtoto atajifunza mengi sana kwenye baa na atasikia mengi sana kama matusi atashuhudia maugomvi atashuhudia tabia za ajabu ajabu sasa hapo ndo manzo wa mtoto kuharibikiwa kimaadili bila wewe mwenyewe kujijua fikiria katika maisha yake ya utoto umeenda naye sehemu hizo mara 10 baadaye atakuwa mtoto wa namna gani? Unadhani hatokuwa mlevi? Tena mwingine hadi saa sita za usiku bado yupo naye tu, hivi huoni kama unamtesa huyo mtoto?


Kuna sehemu nyingi sana ambazo unaweza ukakaa na mtoto mdogo ila jitahidi usiwe kwenye vilabu vya pombe tena isiwe usiku. Unaweza kumpeleka beach au sehemu yoyote yenye michezo ya watoto mbona sehemu zote hizi wanauza vilevi ambavyo unaweza kunywa wakati mtoto wako anacheza?Tena wanakuwa na vyakula vizuri sana kwa watoto na ukishaona mtoto kaenjoy vya kutosha mrudishe nyumbani wewe uendelee na mambo yako ukitaka hata kulala huko we lala lakini amepumzika nyumbani.

Nimeliona hili zaidi y mara tano na ndiyo maana leo nimeamua niliseme tu. Sidhani kama haki ya mtoto inaruhusu hii

Asanteni sana nadhani mtazingatia hili

Kama vipi choma ganzi


No comments:

Post a Comment