Habari zenu wapenzi!!
Namshukuru Mungu naendelea vizuri japo nilikuwa nasumbuliwa na mafua, sasa mmoja wa marafiki na mpenzi wa blog kanitumia hii email kaniambia niweke bloguni kwa manufaa ya wengi, kwa jinsia yeye ni mkaka. Naomba usome hapo chini
Hii itasaidia wengi!
Ni kweli kwamba mapenzi hayachagui umri? Umeshajiuiza kwa nn mapenz mengi ya kishuleshule yanaishia njiani? Kwa nn wanaooana na umri sawa ndoa hazidumu au migogoro haiishi?
Kwa mujibu wa utafiti wangu nimegundua kwenye mapenzi umri pia ni kigezo kikubwa.
Kiukweli wasichana wanafanikiwa kupevuka kiakili ya maisha haraka kuliko wavulana. Najua wanaume wengi mtalipinga hili lakini ngoja nitoe mifano michache ambayo itadhibitisha haya.
Leo msichana wa darasa la pili anaweza kukabidhiwa familia akawapikia, akafua nk. Mvulana wa umri huo huo km kuna kubwa anaweza kufanya bac ni kuendesha gari la mabati tena alilotengenezewa. Tayar huyu msichana kakuacha mbali na huenda mvulana akamaliza primary hajapiga hiyo hatua.
Jiulize leo mabinti wangapi waliachiwa mimba hawana nyuma wala mbele lakini wamelea bt akili ya mwanaume ilifika kikomo na kuona kukimbia au kukana mimba ndiyo suluhu?
Hiyo ni mifano michache tu kati ya mingi. Kwa ufupi inadhibitisha ukweli huu kwamba wasichana wana upeo mkubwa sana kimaisha kulikio wavulana.
Watu wawili hawawezi kwenda njia moja wasipopatana na kwa kila kitu hasa kiakili na kifikra. Utakubaliana na mimi kwamba kutokana na mifano hiyo hapo juu kwa mwanaume kwa akili ya maisha analingana na binti mdogo kwake kiumri may be zaidi ya miaka 6 na kuendelea. Niishie hapo ntamalizia siku nyingine.
Haya kama kuna mwenye chochote cha kuongeza tiririka hapo chini!!
No comments:
Post a Comment