Friday, September 28, 2012

Tusaidiane kumshauri huyu!


Habari zenu wapendwa kuna rafiki yangu wakaribu kanitumia hii email nimemshauri ila naomba nanyie mtoe mawazo yenu hapahapa na siyo facebook wala Twitter.
Hellow!
Jesca kuna issue nahitaji comment yako. Hii imemtokea Mdogo wangu. Ni ndefu Ila usichoke tafadhali nisaidie huu mzigo.
Iko hv: Dogo alitokea kupendana na binti mmoja then wakaanzisha mahusiano mambo yakaendelea na kweli Dogo anakiri alishikwa kwa maana alimpenda sana na alijitahidi kufanya kila lililokuwa ndani ya uwezo wake. Walidumu km mwaka na zaid bila matatizo! Muda baadae yule binti akajichanganya kwa siri na Daktari mmoja hv. Baadae siri ikafichuka Dogo akamuuliza kuhusu hilo akakiri ni kweli na alifanya hivyo kwa sababu alikuwa na shida ya kifedha kwa hiyo kuwa naye alikuwa anapata fedha. Ilimuuma sana mdogo wangu akaamua kumuacha yule binti lakini kwa huzuni coz alikuwa anampenda sana. Bac akawa anajitahd kujikeep busy ili amsahau na kweli akafanikiwa.
Baada ya miezi 3 binti akawa amempigia cmu akimtaka waonane bac tayari ikawa imemuathiri sana Dogo akaja kunilalamikia. Akawa ananiambia cwez kuacha kumuona coz bado nampenda na kweli jana kaja wameonana ss aliyomueleza ni haya!
Kwanza kipindi chote cha zaidi ya miezi mitatu alikuwa na huyo jamaa na ameshabebeshwa mimba Ina zaidi ya mwezi ss km na nusu hv. Anachotaka yy binti anataka warudiane na Dogo na watunze huo ujauzito ambao anakiri kweli ni wa huyo jamaa na mbaya zaidi huyo mhusika ameukataa. Kwa upande mwingine binti anajua Dogo anampenda so anachukulia hiyo advantage.
Mm nimeombwa ushauri nikashtuka nisijibu lolote naweza kuharibu Ila ww nakuamini naomba isome scenario vizuri na uamue km mwanamke. Nashukuru sana mpenzi wangu kwa ushauri wako!


USHAURI WANGU:

Huyo mwanamke anasumbuliwa na tamaa ya fedha, siku zote ukimpenda mtu basi utamvumilia tu. Pia yuko hatarini sana kuambukizwa Ukimwi na magonjwa ya ngono. Na inavyoelekea huyo msichana ashajua mdogo wako anampenda na ndiyo maana alikuwa hata na uhuru wa kumwambia yupo na Doctor kwaajili ya pesa tu. Hii ni hatari sana kama mwanamke anaweza kuwa huru kiasi cha kukwambia anatembea na mtu fulani kwasababu ya pesa basi ni wazi anajua ashaichota akili yako angekuwa mwingine angeogopa tena angeweza hata kudanganya mradi asikupoteze.

Kama ameweza kuja na mimba kesho atamletea UKIMWI, hivyo basi huyu binti aachane naye mara moja na jua kwamba amerudii kwa mdogo wako kwakuwa kule ametelekezwa asingetelekezwa wala asingemkumbuka.

Hata kama akiamua amsamehe na kurudiana naye inamaana mimba itabidi watoe hapo watakuwa wametenda dhambi kubwa pia siyo rahisi kwa fikra za binadamu wa kawaida akasahau hicho kitendo siku zote itaendelea kumuumiza kwenye kichwa chake, kiufupi itamuharibu kisaikolojia na pengine hata mapenzi ya zamani aliyokuwa nayo kwake yatakufa, HAWAWEZI TENA KUWA NA FURAHA! Huyo binti azungumze na familia yake wajue jinsi ya kwenda kuzungumza na huyo dokta au familia yake taratibu nyingine za sheria zifuatwe nadhani hilo ni fundisho kwa wasichana wote.

Huyo mdogo wako mwambie aendelee na maisha yake wasichana wapo wengi sana kwasasa atulie afanye kazi kwa bidii iko siku atajitokeza mtu ambaye atamdatisha kuliko huyo wa sasa.

WASICHANA JITUMENI WENYEWE TAFUTENI KWA MAJASHO ONA SASA MNAJIKUTA MNAWAPOTEZA WAPENZI WENU KWASABABU YA TAMAA YA PESA

Kama kuna ushauri wowote tiririka!

Kama limekuuma CHOMA GANZI

3 comments:

  1. Dogo achana kabisa na huyo binti na jaribu kuzishinda hisia zako kwake sababu kama utamsamehe na kurudiana nae na mkafanya maamuzi ya kulea au kuitoa mimba lolote linaweza kutokea muda wowote ambalo linaweza kuatarisha hata uhai wako. Kumbuka kina dada hisia zao ziko kwene mioyo yao na sio kwene akili kama tulivyo wanaume wengi hivyo ni wepesi sana kusahau na kusamehe sababu moyo siku zote una huruma hivyo basi mtaitoa mimba na kurudiana ila kesho atamsamehe daktari na kurudiana nae au atampata mtu mwingine ambaye atampa fedha au msaada mwingine wowote na atakukimbia tena sababu huyo binti ni "MATERIAL WISE LADY".......

    ReplyDelete
  2. Mapenzi ni kizunguzungu kwa kweli na kila mtu ana maana yake linapokuja suala la mapenzi. Ila wakati mwingine, KUNAHITAJIKA MAAMUZI TENA MAGUMU SANA kwenye mapenzi kwa manufaa ya baadaye. Kwa hali ya dogo, maamuzi magumu anayopaswa kufanya ni KUACHANA NA HUYO BINTI. Hali inaonyesha kuwa mapenzi yao ni ya upande mmoja, yaani dogo anampenda msichana lakini msichana hampendi dogo na ndio maana akaamua kutoka na huyo Dr. Angekuwa anampenda kwa dhati kama dogo anavyompenda wala asingefanya mambo kama hayo. Dogo hakuna ujanja hapo, yeye aachane naye na dogo aendelee na mambo yake mengine, wasichana wazuri, wenye tabia nzuri, wenye kujiheshimu n.k wako wengi sana. Dogo vuta pumzi, usiwe na haraka tena. Kuwa mwangalifu.

    ReplyDelete
  3. Achana naye kabisa.

    ReplyDelete