Thursday, December 27, 2012

INVITATION!!

Napenda kuwaalika wote kwenye party hii, mkiwa kama fans wa hii blog kwaajili ya sherehe ya kuukaribisha mwaka, msijeniita mchoyo bure!!


                                       “IN HOUSE PARTY”  

The party will be on the night of 31st Dec at Chadibwa hostel opposite Chadibwa beach Kigamboni from 12pm till dawn!! 

Entertainments:(Free) 
.Music from the best DJ in town
.Performance from FIRST PLANET DANCERS
.Performance from KANGA MOKO NDEMBENDEMBE
.Drinks of all kinds
.Food(Nyama Choma and BBQ)
.FIREWORKS
.Red carpet

Entrace: 10,000/=tshs- u get a coupon for 3 beers and food ( should be paid in advance before 31st Dec)

Contacts: 0714 460 360 JT
              0715 484 866 Sadath

                                                  "KARIBU SANA"

Friday, December 14, 2012

Jikague kabla hujaenda kwa mkeo!

Habari zenu?? Mpo pouwa??? Hata mi niko poa kabisa.

Nadhani wengi mtakuwa mmesikia au wengine yamewakuta haya,

 1.mke kukuta lipstick kwenye shati la mumewe
2. mke kukuta condom kwenye nguo ya mumewe
3. mke kukuta kipodozi au nguo au kitu chochote kwenye gari la mumewe
4. mke kukuta picha ya mwanamke kwenye simu au laptop au kwenye bahasha za mumewe

Sasa jiulize uzembe uko wapi?? Ni mkeo ndo ana kiherehere cha kuchunguzachunguza au ni wewe ndo umejisahau au umemfanya mkeo bwege kiasi cha kuacha vitu ovyo na kutojali?

Siku zote ukiwa mwizi uwe mjanja, sikufundishi utoke nje ya ndoa wala sikufundishi umalaya la hasha ninachofanya ni kumkinga mkeo ili asiumie, we unadhani akishagundua una mwanamke nje atafurahia na kukupongeza?Unadhani atakwambia 'mume wangu hongera sana kumbe we mwanaume wa ukweli eenh? ITAMUUMA SANA tena usipoangalia ndo itakuwa MWANZO WA NDOA YAKO KUYUMBA.

Sasa basi kitu cha kufanya, endapo utakuwa umetoka kwenye nyumba ndogo yako kabla hujafika home jiangalie unalipstick kwenye nguo?? Au kwenye gari kuna kitu chochote ambacho huyo mwanamke ameacha?? Ukishaangalia ukiona hamna basi waweza kwenda home pia usisahau simu yako kuiangalia manake huwezi jua kitatokea nini mbele ya safari.

ANGALIZO: Hii sio tu kwa mwenye nyumba ndogo hata kama huna mwanamke nje pia uwe unakagua gari lako coz njiani unaweza mpa mtu lift kwa bahati mbaya akasahau au akadondosha kitu huku wewe huna habari halafu wife akakuta ikawa mtiti.

Na usiseme mkeo ndo anakiherehere wewe umeshakuwa mali yake anahaki na wewe, hawezi kukuta condom iliyobakia kwenye suruali yako halafu yeye akacheka tu.

ONYO: Wewe kimada au ndo nikuite nyumba ndogo usithubutu kuacha staffs zako kwenye gari au nguo ya huyo mwanaume ilihali unajua kabisa ni mume wa mtu hiyo ni TABIA MBAYA, nasema hivi kwa kuwa mwingine anafanya makusudi kuacha mradi kumpa taarifa mke wa jamaa ili ajue ana mke mwenza, ebu wacha uswahili JIFUNZE KULA NA KIPOFU, huwezi tafuta wako wanaume wenyewe wachache halafu unataka kuharibu kwa taarifa yako umuharibii mwenzako unajiharibia mwenyewe na nilishasema na NARUDIA TENA usidhani atamuacha mkeo kwa ajili yako bali atakuacha wewe ili kuokoa ndoa yake.


SIKUFUNDISHI UWE NA NYUMBA NDOGO ILA KAMA UNAYO TAFADHALI USIMUUMIZE MKEO!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Kama limekuuma we CHOMA GANZI tu!!!

Monday, December 10, 2012

SEHEMU ZENYE HISIA SANA KWA MWANAMKE

Hii post nimeitoa PASSION kwa dada mmoja anaitwa Angel, ina ukweli wake na nimeipenda sana ndo maana nimeileta hapa ili nanyi mjue.

SEHEMU ZENYE HISIA SANA KWA MWANAMKE.

Tendo la ndoa ni sanaa hivyo inatakiwa ufundi na ubunifu ili kuweza kufurahia tendo hili.

Yafuatayo ni maeneo 12 yenye msisimko na kama mwanaume utayashughulikia ipasavyo bila shaka mtafurahia uumbaji
wake Mungu.

1. MIDOMO YAKE.
Tumia midomo yako,ulimi wako na meno yako kuchezea mdomo wake wa juu na wa chini na umbusu kwa msisimko mkubwa.
Kunyonya ulimi pia huchangia
kuongeza kasi ya mwanamke kwenda kileleni.(usafi wa kinywa kwa wote wawili ni muhimu).

2. UKE NA KINEMBE.
Tumia kidole chako cha kwanza cha mkono wa kulia polepole pitisha katika mfereji wa uke ukianzia chini (kutokea kwenye k**a)
ukipandisha juu,fanya hivyo mara
kadhaa.

Kutegemea umbo lako na
urefu,unaweza kuchanganya zoezi hili na kunyonya matiti yake na hapo utaona upumuaji wake ukibadilika na majimaji yakiongezeka kwenye uke.
Kwa kawaida kinembe cha mwanamke kimejificha lakini ukifanya vizuri
zoezi la hapo juu na chenyewe kama uume kitajaa damu na kuinuka.

3. MATITI YAKE.
Matiti yake ni sehemu muhimu sana kwa
mwanamke kama ilivyo kwa uke
wake.
Utampatia raha kamili mwanamke kama
utayapapasa papasa matiti yake,utayaminyaminya kwa upole wa
kimahaba,utayalambalamba na kuyanyonya.

4. MASIKIO YAKE.
Wanawake wengi hupata burudani masikio yao yanapolambwa au kunyonywa au kupigwa busu.

5. SEHEMU YA NYUMA YA SHINGO
Tumia ulimi wako kulamba sehemu ya shingo yake kwa mwendo w kutekenya tekenya.
Tumia ncha ya ulimi kutekenya tekenya kwa kufanya mduara na kuendelea kuchora mduara na kurudiarudia.

6. SEHEMU YA NYUMA YA GOTI.
Sehemu ya nyuma ya goti ina miishio mingi ya mishipa ya fahamu na utashangaa jinsi ammbavyo mwanamke atapata burudani kwa kuishughulikia vyema sehemu hii.

7. SEHEMU YA NDANI YA MAPAJA.
Tumia ubapa wa kiganja chake kupapasa kwa ulaini sehemu ya ndani ya mapaja yake,fanya hivyo juu juu huku ukimbusu busu mapaja yake.

8. MAKALIO YAKE.
Wanawake wengi wanapenda makalio yao
yachezewe kimahaba,anza kwa kuyapapasa papasa,endelea kwa kuyaminya minya kwa kutumia vidole.

9. MIISHIO YAKE.
Miguu yake imejaa miishio ya mishipa ya
fahamu kiasi ambacho baadhi ya wanawake wanaweza kufika katika kilele cha burudani ya tendo la ndoa kwa miguu yao kusuguliwa na kupapaswa.

10. USO WAKE.
Mwanamke atafurahi sana utakaposhika uso wake katika hali ya mahaba na huku
ukitabasamu.
Wakati ukifanya hivyo unaweza
kumbusu midomo yake,mashavu na kwenye paji la uso.

11. HIPS ZAKE.
Sehemu hii ni moja ya sehemu ambazo
zitamfanya mwanamke ajisikie amekubalika kabisa iwapo utashika wakati wa tendo la ndoa.

12. G-SPOT
Sehemu hii iko ndani ya uke ambayo inapata hisia kubwa sana ikibonyezwa
bonyezwa,sehemu hii ipo sentimeta 5 kutoka mlango wa uke na iko katika ukuta wa juu wa uke.

Sehemu hii ikibonyezwa na kuchezewa
ipasavyo mwanamke anaweza akapiz mara mbili au zaidi kwa wakati mmoja.Hii ni njia rahisi ya
kumfikisha mwanamke kileleni,mwanaume aingize kidole kwenye uke na kubonyeza na
kusugua sehemu ya juu ya uke,sehemu hii imekaa kama sponji na huwa ngumu kwa kadiri inavyobonyezwa.

Mwanamke anaweza kujisikia
kama anataka kukojoa kabisa na hawezi
kukojoa ila raha atakayopata ni kubwa sana.

Maswali Sitaki mi nimefanya kucopy tu! CHOMA GANZI!

Saturday, December 8, 2012

Nyege baada ya MP!

Ni kawaida kwa msichana kujisikia hali ya nyege au niseme muwashawasha au hamu ya kufanya mapenzi mara pale tu atokapo kwenye siku zake(MP) tena wengine hadi zile siku mbili au moja ya mwisho kabla hajamaliza MP.

Bado sijapata sababu za kitaalam kwanini hali hiyo hutokea, sijajua ni kwa vile ile pad inakutekenya au ni matokeo tu ya hormones. Hapo labda nikawatafute wataalam wanijuze then niwaletee ukumbini.

Sasa lengo la kuandika hii post ni kuwajuza wanaume na kuwapa ushauri, ni hivi mkeo akimaliza tu period HAKIKISHA UNAMPA CHAKE  manake mtoto wa kike hapo atakuwa anahamu zake sasa kama ndo hausomi mchezo mwenzako ataishia tu kuchekacheka bila mpangilio. Japo kuna siku zingine za pale katikati za mwanamke kuwa hot kwelikweli ila na hii pia usiisahau.

Kwahiyo ndugu yangu pale mkeo au mpenzi amalizapo period jaribu kumpa kitu, kama uko naye mbali basi hiyo ni bahati mbaya, na hapo ndiyo penye umuhimu wa kujua mzunguko wa mwanamke wako. Si kila mwanamke anaweza kumwambia mwenza wake kwamba ana hamu japo siku hizi wengi wanajitahidi kuwa wawazi au mwingine utaona tu vitendo vyake mara akushike hapa mara akushike pale mradi tu kukuonesha kwa vitendo anachotaka kwahiyo kama mwerevu utaelewa.

Hayo ndo yangu ya leo kila nikipata muda wa kuandika nitaandika nina mengi mno!

CHOMA GANZI!!

Monday, December 3, 2012

Kupiga Picha za Utupu!

Imekuwa ni kawaida kusikia na kuona watu wakilalamika mitandaoni na kwenye magazeti baada ya picha zao za utupu/picha chafu kuvuja.

Mimi nina maswali kwenu kwanini upige picha za utupu?? Manake wengine wanajipiga wenyewe wakiwa na akili zao timamu sasa unataka kumuonesha nani huo mwili  wako?? Hujiulizi hiyo simu au camera ikiibiwa huyo atakaye ikamata unadhani hatozirusha mtandaoni? Acha kupiga picha hizo hata kama uko makini kiasi gani.

Pia kuna wale wanawake ambao wanalewa hadi kufikia hatua ya kutokujitambua yaani kazima, mwanaume wake huyohuyo anaamua kumpiga picha za utupu bila yeye kujua na mwingine wala anakuwa hajazima ila kwa kuwa pombe ziko kichwani anajikuta anafanya maamuzi ambayo si sahihi anaulizwa nikupige picha? naye bila hiyana anasaula nguo anajimanua anapigwa picha , ndugu yangu kama pombe huziwezi acha kabisa utakuja jidhalilisha.

Sasa kuna wale wenzangu na mimi waliopofuka kwenye mapenzi wasiojielewa na wasiochuja kitu gani ni sahihi kufanya pale anapokuwa na mpenzi wake. Utakuta anamahusiano na mwanaume hata miezi sita hawajamaliza mwanaume anamwambia ampige picha akiwa mtupu naye anakubali tu! Hivi unajiamini nini na huyo mwanaume?? Hujiulizi endapo mtagombana hatima ya hizo picha ni nini?! Sidhani kama mwanaume anayekupenda atakwambia upige picha za utupu, kwani atakuwa anajali utu wako na kuheshimu mwili wako.. Wengi mnadanganywa eti akikumiss awe anaangalia picha yako, HUO NI UONGO LAANIFU!! Tena kama mwanaume atakwambia hili kuwa naye makini manake ukimkatalia ipo siku atakuvizia umelala na atakupiga bila idhini yako.

Narudia tena mwanaume anayekupenda, anayekujali na kukuheshimu hakupigi picha za utupu, kwahiyo USITHUBUTU! Kama tayari ushapiga nakushauri zifute, kwani utakuwa umeshuhudia story nyingi za mastaa wetu wakilalamika kwenye magazeti kuhusu picha zao zilizovuja na wengi wao wanasema ni watu wao wa karibu ndo wamezivujisha wengine wanasema waliowaibia simu ndo wamezivujisha.. Sasa zote hizi hazikupi fundisho tu!! Kwanini akupige wewe picha za utupu? mbona yeye hapigi hayo mapumbu yake akakutumia??

Tena wengi sana mnatumia whatsapp na BBM kutumiana hizi picha sasa wewe ukituma tu anamforwadia rafiki yake anamwambia 'cheki huyu demu kanitumia hii picha' Sasa kwa style hii unadhani zitaacha kuvuja??

Kama limekukuta pole ila kama bado basi zingatia hili. Na nyie wanaume mkome kuwapiga picha mademu zenu kama unataka piga mapumbu yako yaweke kwenye wall yako.

Limekuuma CHOMA GANZI!

Mnisamehe coz nimekuwa mvivu kidogo wa kuandika, mada, zimejaa kichwani tele ila kutype ndo inakuwa mtiti!

Tuesday, November 20, 2012

Mpe mumeo raha!

Hii ni kwa wanawake walio kwenye ndoa

Jamani mwanaume anapoamua kukuoa ni kwamba amekupenda na ameridhika na wewe na anakupa dhamana ya familia yake.

Sasa wewe kipindi cha mwanzo wa ndoa mapenzi motomoto baada ya muda kidogo tu basi mapenzi yote yanayeyuka hata vile vitu ulivyokuwa unafanya mwanzoni ambavyo ndo vilimpelekea yeye kukupenda huvifanyi tena, tena wengi wanakuwa na viburi na wabishi sana sasa unategemea nini? Unadhani ataacha kukesha kwenye mabaa au ataacha kutafuta nyumba ndogo? Wakati mwingine wewe mwenyewe unasababisha ndoa kuwa chungu, mpe vile vitu vyote ulivyokuwa unampa mwanzo tena ikiwezekana ongeza mahaba, Ili hata mwanaume akisema katoka nje ujue ni umalaya wake tu.

Kuna wengine yani hata ushiriki wao wa tendo la ndoa ni wa manati na wakishiriki ni kama mambwa yani mwanamke kalala mwanaume karudi zake huko kampandia juu kaingiza mashine kafanya kamaliza kaenda kuoga na mwanamke anaenda kuoga wanalala just like that! no romance! no what.... sasa raha yake hapo ni nini?? Wewe ndo wakumbadilisha mumeo kumbuka mwanaume akishaoa yeye anachofikiria ni kutafuta pesa tu vingine vyote anaamini wife yupo ndo kazi yake kusimamia.

Nadhani mmenielewa, kama vipi CHOMA GANZI

Wapenzi kuishi pamoja kabla ya ndoa

Habari,

Kuna kitu ambacho ni muhimu sana leo nahitaji kuwaambia na nimekiona sana tu kwa watu wangu wa karibu.
Kuna tabia ambayo inazidi kushamiri kwenye jamii yetu tofauti na miaka ya nyuma, tabia ya wapenzi wawili kuishi nyumba moja. Si jambo baya kufanya hivyo manake wengi watasema wanataka wajuane kabla hawajajipanga na ndoa ila ni vigezo gani umechukua hadi kufikia uamuzi huo? Mi nadhani kabla ya kukurupuka kufanya hivyo hebu fikiria kwanza, je familia zenu zinaruhusu hivyo?? Unauhakika mnawezana kuishi nyumba moja manake nimeona watu wengi wanafanya hivyo hadi kufikia hatua ya kununua vitu kwa kushare mwisho wa siku wanashindwana ugomvi mwanzo mwisho na hatimaye kuanza kugombea vitu 'hiki nilinunua mimi mara hiki siyo cha kwako' huko ni kujiaibisha kama mnajiamini mnapendana na kuwezana basi fungeni ndoa na kama mnachunguzana basi mchunguzane kwa tahadhari manake mtu hashindwi kuficha makucha kwa kipindi chote ambacho unakaa naye kabla ya ndoa hata kama ikiwa mwaka. Pia dada yangu usidanganyike si kila mwanaume atakaye kwambia mkae wote atakuoa mwingine ndo kwanza anazidi kubweteka, manake ameshaona kuna mwanamke anamfanyia kila kitu kupika kufua kuosha ovyo, unadhani atakaa afikirie ndoa? Hapana, utasikia kila asiku anakwambia ngoja nijipange..... ajipange na nini? kwanini msijipange wote na maisha muanze pamoja? Kuwa makini mwanamke!

Simaanishi usikae naye ila ndo utumie akili sio ubweteke tu mwisho wa siku utajikuta unazalishwa watoto watano bila ndoa wala nini!

Mi nisharopoka hivyo na kama limekuuma CHOMA GANZI,......

Thursday, November 8, 2012

MUME ANASIANA NA HAWARA

Vidole vyangu vimepata nguvu ghafla baada ya kusikia hii habari

'BREAKING NEWS:DAR-ES-SALAAM.kuna mwanamke aliaga kwa mume wake
anaenda tanga kusalimia
kumbe kaenda gusti tandika na mwanaume mwengine
so wakafanya mapenzi
UUME Umenasa Hautoki
so polisi wamewabeba
na kuwapeleka
temeke hospitali
naksikia kuna vurugu
kiasi polisi wanapiga mabomu ya machozi
wamewaweka mochuari
so wanajaribu kuwanasua
ila mume wa huyo mwanamke
kasema anataka milioni tano ili awatoe
so vurugu kila mtu anataka kuona'


Hivi kweli we mwanamke/mwanaume unamuwekea mumeo/mkeo mtego ili akienda nje anasane na huyo mtu?? Sijawahi kuona mapenzi ya namna hii, tena mbaya zaidi unasema huwanasui hadi upewe millioni 5.

Kwanza mwanamke/mwanaume wa namna hii namtafsiri hivi
1. Ana roho mbaya, kiasi cha kwamba haoni vibaya akiona mwenzake akikumbwa na aibu hii
2. Ana tamaa na ndiyo maana katanguliza pesa kwamba bila pesa hawanasui na mtu huyu hashindwi hata kukuua sababu ya pesa
3. Ni mshirikina, kitendo cha kwenda kwa waganga kufanya hayo yote ni ushirikina
4. Hana mapenzi ya kweli kwasababu mtu unayempenda huwezi kutaka kumuwekea mitego itakayomdhalilisha mumewe/mkewe kiasi hicho.

Wakati mwingine kabla hujafanya kitu fikiria mara mbili unaweza ukadhani unamkomoa mtu kumbe unajikomoa mwenyewe, Je, unadhani baada ya kufanya hivyo huyo mwanaume/mwanamke ndo atakupenda? au ndo ataacha umalaya? Hauoni kama unajijengea uadui wewe na mumeo/mkeo? Unadhani baada ya kumnasua atakuacha hivihivi bila kulipa kisasi? Familia yake na watu wake watakuchukulia vipi? Haya ni maswali ambayo ni lazima ujiulize

Wewe kama ni mwanamke/mwanaume wa kweli mtulize mumeo/mkeo kupitia mapenzi mpe yale anayoyafuata nje, na kama umeona kashindikana kuna taratibu zingine ila si kumdhalilisha kiasi hicho. Imefikia kipindi lazima tuwe na ubinaadam je ungefanyiwa wewe hivyo ungefurahi???

Sio kama natetea upande wowote ila nasema ambalo mimi naliona sahihi na ukitaka kunielewa ukiwa kama mwanamke / mwanaume jaribu kufikiria umefanyiwa wewe.

"POLENI SANA KWA WAHUSIKA NADHANI HILO NI FUNDISHO TOSHA"

Haya JT ndo nishasema, limekuuma CHOMA GANZI

Wednesday, October 24, 2012

Madhara ya kuangalia picha za ngono

Kuna watu wanapenda sana kuangalia sinema za ngono, siwezi kukataa mimi mwenyewe huwa naangalia mara mojamoja.

Ila kutokana na reserch yangu niliyoifanya kiholela nimegundua kwa kiasi fulani zina madhara nakuelezea kama ifuatavyo.

Kwanza inakupunguzia uwezo wako au hisia zako yani wewe utakuwa huwezi kusimamisha au kupata hamu bila ya kuangalia filamu za ngono, hata demu wako akiwa uchi lazima uwashe movie ya ngono ndo uanze shughuli

Pili, Itakufanya usifurahie tendo, manake utakuwa unatamani mpenzio kufanya kama ambavyo unaona kwenye sinema kitu ambacho muda mwingine hakiwezekani kwani hizo ni movie watu wamelipwa wafanye ni sehemu ya biashara ndo maana utakuta mikao mingine ni ngumu kuifanya yote hiyo so utakuwa uko attention kuangalia mwenzio anafanya nini au uko attention ukikumbuka na kufikiria mikao ya kwenye movie kitu ambacho kwa namna moja au nyingine hupoteza radha.

Tatu, kwa asilimia 99 huchochea punyeto, nadhani mtakuwa mnakumbuka kwenye mada iliyopita nilizungumzia madhara ya punyeto, kwa hiyo utajikuta unappata madhara yale yale ya upigaji punyeto

Nne, unapunguza uwezo wa kufikiri na kufanya kazi, jaribu kuchunguza hili ukiwa unaangalia movie ya ngono hata kama kuna kazi ipo mezani kwako au ndani unakuwa mvivu hata wa kuifanya na hata kama mtu akikupigia simu ghafla akakuuliza kitu hutaweza kumjibu papo kwa hapo lazima utamwambia subiri kwakuwa umesahau pia umeshajijengea uvivu mkubwa kupitia hiyo picha ya ngono.

Haya nimepata tu madhara hayo manne kama unayajua mengine tupia hapo kati au kwa email yangu tarimojesca@gmail.com au kwenye page yangu ya facebook jescatarimo.blogspot

Kumbuka ya kwamba hao ni waigizaji tu kama bongo movie wanavyoigiza wanachokifanya hawakifeel kabisa, so usione wanafuck huku wanapiga sarakasi nawewe ukaiga utaumia!

Adui yangu CHOMA GANZI!


Unajua utamu wa denda???Nakujuza sasa

Nitashindwa kukuelewa wewe ambaye mnaanza tu kukukuruka na mpenzio au mkeo/mumeo bila hichi kitu 'denda' au french kiss

Bwana asikwambie mtu denda lina raha yake, denda lina uwezo uwezo wa kuhamisha fikra kutoka upande mmoja hadi mwingine. Mfano mkeo/mumeo kuna kitu kimemuudhi muombe msamaha huku unamsogelea taratibu halafu ukimfikia mpe ulimi uone, yani automatically hasira zooote zinakatika naye utaona atakavyojibu mapigo na mwisho wa siku mnajikuta hata mkimaliza mchezo kabisa.

Siwezi kuficha mimi mwenyewe JT ni mbovu sana wa hiyo kitu yani nikipewa denda tu mwili wote wanilegea sasa siyo kwangu tu asilimia kubwa ya watu wote wapo hivyo hata wewe mwenyewe najua utakuwa upo hivyo.



Sasa denda linakuwa tamu zaidi kama wote midomo yenu ni misafi isiyotoa harufu, sidhani kama utaenjoy endapo mwenzako kinywa kinatema mmmmh hapo ndo utakuta wengi hawapendi kukiss wapenzi wao, sasa kwanini ukose na umkoseshe raha mwenzio kwa kitu kidogo hivyo?? Kuna wengine mna matatizo ya kunuka mdomo basi hakikisha unamuona mtaalam ndugu yangu bila hivyo utaaibika na kujua kama unanuka mdomo ni rahisi sana sogeza kiganja chako mdomoni na utoe hewa wewe mwenyewe utaisikia au nyonya kidole chako halafu nusa, harufu lazima ibaki kwenye kidole kama una huo ugonjwa nenda kwa wataalam ila vinginevyo jitahidi kupiga mswaki mara kwa mara kwa dawa maalum pia kama penda kutafuna BIG G mara kwa mara hii kidogo itasaidia kupoteza harufu. Au siku hizi kuna manukato ya mdomo pia waweza tumia

Pia kingine ambacho napenda niwaambie usije ukatoka kula samaki, dagaa au karanga halafu bila hata kusafisha mdomo ukaenda kumpa denda mpenzio nikwambie ukweli unampa kero sababu harufu ya hivyo vitu hufanya mdomo utie kichefuchefu,so safisha kwanza mdomo au tafuta hata big g halafu ndo mambo yaendelee usimpe shombo mwenzio wengine wanakinyaa eeenh?

CHOMA GANZI!
Haya hilo ndo la leo la kumoyo 'denda linautamu wake jamani' dah! haswa umpate anayelijulia mbona utadata!

Mi ndo nishalopoka likikuuma kama kawaida choma ganzi!!

Wednesday, October 17, 2012

Nampenda Mume Wa Mtu Kuliko Mpenzi wangu!

Naomba msome kwa umakini na mnisaidie kutoa ushauri kwa huyu dada, ambaye yuko njia panda

Nina bf wangu ambaye tuna mahusiano ya muda mrefu kidogo, mpenzi wangu mimi yuko busy sana kwasababu ya majukumu hivyo kuonana kwetu ni kwa nadra sana, inaweza ikapita miezi 2 nisimtie machoni hapo ni kumuona tu kwenye swala la mapenzi ndo kabisaaa inaweza pita hata miezi 3 ila shida zangu za kifedha zote ananitatulia hata kama ni kodi ya nyumba ikiisha atatuma M-Pesa,

 Sasa kinachonitatiza mimi ni kwamba hivi karibuni ametokea mume wa mtu ambaye naamini kuwa ananipenda, anatumia muda wake mwingi kuwasiliana na mimi na kuwa na mimi kwakuwa mpenzi wangu yuko busy sana yeye ndo huwa ananipa company siku zote na mbaya zaidi mapenzi yangu yamezidi kwake kuliko haya kwa bf wangu, mara zote anakuja yeye kwanza mbele ya bf wangu kwenye kichwa changu. 

Ananipa kila ninachokitaka anaridhisha kwa kila jambo na ananielewa sana, hata kama sijamwambia kitu yeye huwa anakuwa tayari ameshafikiria na kujikuta napata kile ninachokihitaji, kiukweli uwezo wake kitandani ni mkubwa unaoniridhisha sana ananipa mahaba yote na ananifikisha ipasavyo.

Naomba nieleweke kuwa sijampendea pesa huyu kaka bali mapenzi anayonipa najisikia raha sana kila nikiwa naye imefikia hatua hata siogopi tena kufumaniwa na bf wangu, na kama akipiga simu niko naye naweza hata nisipokee naona kama ananipunguzia radha. Kusema ukweli sina maneno ya kudhihirisha ninachokipata kutoka kwa huyu mume wa mtu ila kiukweli nampenda sana, na naiheshimu sana familia yake na naomba Mungu mkewe asigundue sababu itakuwa imeniharibia.

Jamani naombeni ushauri wenu nifanyeje?? Kwani kwasasa nataka niachane na bf wangu ili niwe na mume wa mtu peke yake. Nishaurini jamani niko njia panda!

Kama una ushauri weka hapo chini, au nitumie kwa tarimojesca@gmail.com au kwenye page yangu ya facebook au twitter.

Tuesday, October 16, 2012

Soma ujue madhara ya kupiga Punyeto

Punyeto(Masturbation) au wengine wanaita ‘pool’ au ‘nyeto’ ni kitendo cha wewe mwenyewe kujitelea msisimko na kuweza kujifikisha kileleni kwa njia ya kujichua.

Najua wanaume wengi mmepita happa na wengine mnao sana huu mchezo, ukiingia bafuni unapaka sabuni yako unaanza kazi, au umekaa chumbani kwako ghafla hisia zimekujia au ulikuwa unaangalia blue movies mzuka ukakushika ukajikuta unapapasa mashine mara uweke mate kidogo huku unasugua na mwingine anamafuta maalam kwaajili ya nyeto tu! Haya si mbaya maana 

Punyeto ni sehemu ya maisha ya binaadam na baadhi ya madaktari hushauri siyo tu kuongeza uzoefu katika tendo la ngono ila pia katika kuboresha afya kwa ujumla wake. Ingawaje kuzidi kwa kila jambo hata kama ni jema huwa baya, vivyo hivyo kukithiri kwa ufanyaji wa ‘nyeto’ husababisha matatizo mbalimbali kama hayo chini

ATHARI za PUNYETO
Wanaume waliowengi hukidhi haja zao kwa kutuliza matamanio yao kwa njia ya kujichua/ kupiga punyeto bila kufahamu madhara yake: Nikweli punyeto inasaidia kupunguza hamu ya tendo na ni njia nzuri ya kujiepusha na zinaa kwa kujilinda na maradhi ila kiukweli ina madhara na madhara yake mara nyingi hutokea kwa mtu anaependelea sana kupiga punyeto, kutokana na utafiti uliofanywa kisayansi imeonekana punyeto ni nzuri kiafya ila endapo kama utakuwa unapiga mara moja moja na sio kila siku. Napenda kuwashauri watu wanaopiga punyeto wawe makini na wasiendekeze jambo hili kwani madhara yake ni makubwa sana na Athari zake kubwa ni hizi zifuatazo:
1. PUNYETO INAUA NGUVU ZA KIUME:
Upigaji wa punyeto unaweza kusababisha upungufu wa nguvu za kiume, kwani kipindi unapiga punyeto jua ile mishipa inayofanya uume usimame unakuwa unaichua na uume unakuwa umesimama kwa muda mrefu sasa ikitokea ukawa unafanya hivi kila siku ile mishipa inalegea na uume unakuwa unakosa nguvu hata ukisimama haui strong unakuwa kama umelegea.

2. KUWAHI KUMALIZA MAPEMA KATIKA TENDO:
Mara nyingi mtu aliezoea kupiga punyeto huwahi kumaliza mapema pindi akiwa anafanya mapenzi na mpenzi wake na wakati mwingine uume hushindwa kusimama kwa mara ya pili na kujikuta anashindwa kurudia tendo ikiwa mpenzi wake bado hajaridhika na anahitaji kuendelea kusex.

Athari nyingine ni kama zifuatazo

3.Uchovu wakati wote / Fatigue. Feeling tired all the time.
4.Maumivu ya nyonga / Lower back pain.
5.Kusinyaa kwa Nywele / Nywele kunyonyoka / Thinning hair / Hair Loss
6.Maumivu ya kende / Groin / Testicular Pain
7.Maumivu ya kiuno / Pain / cramp in the pelvic cavity or/and tail bone

Pia kuna kitu nataka niwadokeze kidogo, hiyo hapo

Njia ya kufanya au kukusaidia upige game ndefu

Mtu anaweza kujamiiana mara mbili mpaka tatu kwa wiki katika hali ya kawaida ya tendo la ndoa. Ingawaje tendo la ndoa linaweza kufanyika mara nyingi zaidi pale ambapo mwanaume atajifunza kufikia kutika kilele cha Raha (orgasm) bila ya kutoa manii (shahawa) na kwa kufanya hivyo atajihifadhia nguvu ya kibaiolojia katika mfumo wake na kuufanya Uume kuwa wenye nguvu na kuendelea na mwendo kwa muda mrefu zaidi na mwishoni kupata mshindo wenye ujazo tosha mkubwa na ulio katika viwango vya ukweli.(Unajua maana yake yaani ukitaka kukojoa unakuwa kama unajizua au unajibana)

Utajuaje kama ushaaathirika na Punyeto??

 Ukiona unatokwa na shahawa bila hata uume kusimama jua ‘kwishney’ imekula kwako, wewe unapaswa uende ukawaone wataalam haraka sana dalili nyingine ni kama za hapo juu maumivu ya kende, kiuno, nyonga, uchove, nguvu za kiume kupotea, unacheza gemu

Ila bado hujachelewa ndugu yangu kama umeathiriwa na hili tatizo solution ipo waone madaktari watakusaidia

Acheni kupiga pool mtakuja kuumbuka jamani!!!

Hilo ndo langu la leo
Kama vipi choma ganzi! (Wanawake mjiandae naandaa yenu pia)

Tuesday, October 9, 2012

Unajua kazi ya Kisunzu?

Kisunzu ni ndevu za kwenye kidevu chini kidogo ya lips zako kama zinavyoonekana kwenye picha hapo.

Watu wengi huzifuga kwaajili ya fashion tu, ila kuna wachache wanaojua kazi zao kwa ufukunyuku wangu nimeambiwa wapemba ndo huwa wanazitumia sana, ok hayo hayatuhusu iwe kweli iwe uongo mi naenda kuwaambia jinsi zinavyotumika.

Kisunzu
Kwanza kabisa hicho kisunzu chako lazima kiwe kimechongwa vizuri sio kimekaa tu hovyo hovyo, pia ni lazima kiwe laini hivyo ni muhimu kuwa unapakaa mafuta ambayo yatafanya ndevu zako ziwe laini.

Sasa matumizi yake kwenye sita kwa sita ni hivi katika kupagawishana na mpenzio namaanisha unapokuwa unamnyonya mwezio unakitumia kisunzu chako kama unasugua kwenda juu na kurudi chini kwenye ile sehemu yetu ya utamu na kama kisunzu chako kikavu na kigumu kama msasa basi acha tu, manake utamchubua mwenzako ila kama ndo umekilainisha na mafuta ni kilaini basi huyo mwanamke lazima apagawe na nadhani atashangaa huo utundu umeutoa wapi manake si wengi wenye ujuzi huu.

Si kila siku unampa mambo yaleyale badilika, vitu vingine unaweza ukajitungia tu kichwani na ukajaribu ukajikuta unampagawisha mwenzio.

Thursday, October 4, 2012

Una nyumba ndogo??Zingatia hili

Wewe mwanaume unajua madhara ya kumpeleka nyumba ndogo sehemu ambayo unaenda na mkeo??
Nadhani bado hujanielewa namaanisha nini, sasa nakudadafulia vizuri.

Mfano wewe mwanaume kuna sehemu hupenda kujivinjari na nyumba ndogo wako inaweza kuwa baa au kwenye mgahawa, na utakuta hata wahudumu washazoea kuwaona pale. Sasa siku moja unaamua kwenda na wife pale pale na mnajiachia vizuri sana. Hapo nadhani mtakuwa mmenipata naongelea nini

Sasa kaka yangu nikwambie hilo ni kosa kubwa mno unafanya, siku zote vya kushoto viache kushoto vya kulia viache kulia kamwe usichanganye utakuja kulivuruga.

Nakwambia hivyo kwasababu mfano imetokea siku moja upo na nyumba ndogo mkeo naye katika pitapita zake akasema hii seshemu nilishakaa na mister ngoja leo nipate msosi au kinywaji hapa, anaingia mara anakukuta unadhani itatokea nini?? Na sisi wanawake tunahiyo tabia sana ya kwenda sehemu ambazo tulishaenda na mister

Pia pata picha umekaa na wife wako mara nyumba ndogo huyo kaingia, unadhani we binafsi utakuwa na amani? haya kama huyo kimada hamjui wife yako basi jua litatokea varangati ila kuna wengine wastaarab ashajua huyu ni mume wa mtu nina mipaka naye kwahiyo atakaa sehemu nyingine kimya kajikausha kama hakujui, sasa japo amekuokoa wewe na ndoa yake ila kumbuka rohoni linamuuma pia unamdhalilisha sana unadhani watu waliozoea kuwaona pale watawafikiria vipi?? usitake kuwapa watu faida pia kwanini umfanyie mwenzako hivyo?? Inakera ati kwani hakuna sehemu nyingine?

Ila sichochoe wala kukufundisha tabia mbaya ya kuwa na nyumba ndogo najaribu tu kuiokoa ndoa yako
Mi ndo nisharopoka likikuuma choma ganzi!www.jescatarimo.blogspot.com

Monday, October 1, 2012

MKE VS KIMADA

MKE VS KIMADA
Nani unae mkubali ??

MKE nikama TV,wakati KIMADA nikama
Simu yamkononi,
Ukiwa Nyumbani unaangalia TV ,
ukitoka outing Unaenda na Simu,
Huna Pesa unauza TV,ukiwa na Pesa
unabadilisha Simu ,
Mda mwingine unafuahia TV ,lakini
Mda mwingi unachezea Simu,
TV ni bure mda wote wa Maisha
kuangalia ,Simu usipo lipia
mawasiliano Hukatika,
TV nikubwa na mda mwingi huwa
Imezeeaka, lakini Simu ni
nzuri ,nyembamba na kiportable,
Uendeshaji wa TV kiuchumi ni mdogo
na unakubalika ,lakini Simu uendeshaji
ni Mkubwa na wa gharama
unaohitajika kila siku..
TV ina remote ya kuiendesha , SIMU
haina
Lamwisho na Muhimu kabisa Simu
inanjia mbili za mawasiliano unaongea
na kusikilizwa lakini kumbuka TV lazma
uwe unasikiliza tuuh (utake usitake )
Mwisho kabisa kumalizia TV hazina
Virusi, lakini SIMU Mda mwingi zina
Virusi...
Je ni Kweli au Sio Kweli ?
heheeeeee


(KOPI ENDI PESTI)

Saturday, September 29, 2012

Kwa Ujumbe huu mwanamke yupo hatua 5 mbele ya mwanaume!!


Habari zenu wapenzi!!
Namshukuru Mungu naendelea vizuri japo nilikuwa nasumbuliwa na mafua, sasa mmoja wa marafiki na mpenzi wa blog kanitumia hii email kaniambia niweke bloguni kwa manufaa ya wengi, kwa jinsia yeye ni mkaka. Naomba  usome hapo chini


Hii itasaidia wengi!
Ni kweli kwamba mapenzi hayachagui umri? Umeshajiuiza kwa nn mapenz mengi ya kishuleshule yanaishia njiani? Kwa nn wanaooana na umri sawa ndoa hazidumu au migogoro haiishi?
Kwa mujibu wa utafiti wangu nimegundua kwenye mapenzi umri pia ni kigezo kikubwa. 
Kiukweli wasichana wanafanikiwa kupevuka kiakili ya maisha haraka kuliko wavulana. Najua wanaume wengi mtalipinga hili lakini ngoja nitoe mifano michache ambayo itadhibitisha haya.
Leo msichana wa darasa la pili anaweza kukabidhiwa familia akawapikia, akafua nk. Mvulana wa umri huo huo km kuna kubwa anaweza kufanya bac ni kuendesha gari la mabati tena alilotengenezewa. Tayar huyu msichana kakuacha mbali na huenda mvulana akamaliza primary hajapiga hiyo hatua. 
Jiulize leo mabinti wangapi waliachiwa mimba hawana nyuma wala mbele lakini wamelea bt akili ya mwanaume ilifika kikomo na kuona kukimbia au kukana mimba ndiyo suluhu?
Hiyo ni mifano michache tu kati ya mingi. Kwa ufupi inadhibitisha ukweli huu kwamba wasichana wana upeo mkubwa sana kimaisha kulikio wavulana. 
Watu wawili hawawezi kwenda njia moja wasipopatana na kwa kila kitu hasa kiakili na kifikra. Utakubaliana na mimi kwamba kutokana na mifano hiyo hapo juu kwa mwanaume kwa akili ya maisha analingana na binti mdogo kwake kiumri may be zaidi ya miaka 6 na kuendelea. Niishie hapo ntamalizia siku nyingine. 


Haya kama kuna mwenye chochote cha kuongeza tiririka hapo chini!!

Friday, September 28, 2012

Tusaidiane kumshauri huyu!


Habari zenu wapendwa kuna rafiki yangu wakaribu kanitumia hii email nimemshauri ila naomba nanyie mtoe mawazo yenu hapahapa na siyo facebook wala Twitter.
Hellow!
Jesca kuna issue nahitaji comment yako. Hii imemtokea Mdogo wangu. Ni ndefu Ila usichoke tafadhali nisaidie huu mzigo.
Iko hv: Dogo alitokea kupendana na binti mmoja then wakaanzisha mahusiano mambo yakaendelea na kweli Dogo anakiri alishikwa kwa maana alimpenda sana na alijitahidi kufanya kila lililokuwa ndani ya uwezo wake. Walidumu km mwaka na zaid bila matatizo! Muda baadae yule binti akajichanganya kwa siri na Daktari mmoja hv. Baadae siri ikafichuka Dogo akamuuliza kuhusu hilo akakiri ni kweli na alifanya hivyo kwa sababu alikuwa na shida ya kifedha kwa hiyo kuwa naye alikuwa anapata fedha. Ilimuuma sana mdogo wangu akaamua kumuacha yule binti lakini kwa huzuni coz alikuwa anampenda sana. Bac akawa anajitahd kujikeep busy ili amsahau na kweli akafanikiwa.
Baada ya miezi 3 binti akawa amempigia cmu akimtaka waonane bac tayari ikawa imemuathiri sana Dogo akaja kunilalamikia. Akawa ananiambia cwez kuacha kumuona coz bado nampenda na kweli jana kaja wameonana ss aliyomueleza ni haya!
Kwanza kipindi chote cha zaidi ya miezi mitatu alikuwa na huyo jamaa na ameshabebeshwa mimba Ina zaidi ya mwezi ss km na nusu hv. Anachotaka yy binti anataka warudiane na Dogo na watunze huo ujauzito ambao anakiri kweli ni wa huyo jamaa na mbaya zaidi huyo mhusika ameukataa. Kwa upande mwingine binti anajua Dogo anampenda so anachukulia hiyo advantage.
Mm nimeombwa ushauri nikashtuka nisijibu lolote naweza kuharibu Ila ww nakuamini naomba isome scenario vizuri na uamue km mwanamke. Nashukuru sana mpenzi wangu kwa ushauri wako!


USHAURI WANGU:

Huyo mwanamke anasumbuliwa na tamaa ya fedha, siku zote ukimpenda mtu basi utamvumilia tu. Pia yuko hatarini sana kuambukizwa Ukimwi na magonjwa ya ngono. Na inavyoelekea huyo msichana ashajua mdogo wako anampenda na ndiyo maana alikuwa hata na uhuru wa kumwambia yupo na Doctor kwaajili ya pesa tu. Hii ni hatari sana kama mwanamke anaweza kuwa huru kiasi cha kukwambia anatembea na mtu fulani kwasababu ya pesa basi ni wazi anajua ashaichota akili yako angekuwa mwingine angeogopa tena angeweza hata kudanganya mradi asikupoteze.

Kama ameweza kuja na mimba kesho atamletea UKIMWI, hivyo basi huyu binti aachane naye mara moja na jua kwamba amerudii kwa mdogo wako kwakuwa kule ametelekezwa asingetelekezwa wala asingemkumbuka.

Hata kama akiamua amsamehe na kurudiana naye inamaana mimba itabidi watoe hapo watakuwa wametenda dhambi kubwa pia siyo rahisi kwa fikra za binadamu wa kawaida akasahau hicho kitendo siku zote itaendelea kumuumiza kwenye kichwa chake, kiufupi itamuharibu kisaikolojia na pengine hata mapenzi ya zamani aliyokuwa nayo kwake yatakufa, HAWAWEZI TENA KUWA NA FURAHA! Huyo binti azungumze na familia yake wajue jinsi ya kwenda kuzungumza na huyo dokta au familia yake taratibu nyingine za sheria zifuatwe nadhani hilo ni fundisho kwa wasichana wote.

Huyo mdogo wako mwambie aendelee na maisha yake wasichana wapo wengi sana kwasasa atulie afanye kazi kwa bidii iko siku atajitokeza mtu ambaye atamdatisha kuliko huyo wa sasa.

WASICHANA JITUMENI WENYEWE TAFUTENI KWA MAJASHO ONA SASA MNAJIKUTA MNAWAPOTEZA WAPENZI WENU KWASABABU YA TAMAA YA PESA

Kama kuna ushauri wowote tiririka!

Kama limekuuma CHOMA GANZI

Tuesday, September 25, 2012

Wapenzi kufanya kazi ofisi moja!

Ni wengi sana wameshajiingiza katika mahusiano na mfanyakazi mwenzake yaani ofisi moja kwahiyo najua wengi litawagusa.

Ki ukweli kwa jinsi nilivyoona wengi waliodumu kwenye mapenzi haya hadi kufikia ndoa na ndoa zao zikadumu ni wazee wa zamani lakini si kizazi hiki cha sasa, japo wapo wachache ambayo wameweza kufikia malengo yao ila si wote.

Sasa naomba niwaelezee kwanini wengi hawajafika popote

Kwenye maofisi kama mnavyojua kuna mambo mengi sana bila kusahau utani bila kusahau maneno ya umbeya.
 Sasa shida itakuja kama mmoja wenu anapenda kusikiliza maneno ya watu na pia wivu, wewe kama umekubali kufanya kazi ofisi moja na mpenzio basi punguza wivu pia usisikilize maneno ya watu, Kwasababu maneno ya pembeni huwa hayakosekani especially mpenzio awe ndo mtu wa kutaniana na watu.

Ngao yenu kubwa ni mazungumzo, kama mtakuwa huru kuzungumza chochote basi hakika mtafika mbali pia jaribu kupunguza wivu hata kama unamuona mwanaume wako anamshika mfanyakazi mwengine kiuno huku wanacheka, we assume wapo katika matani then mkifika home sasa mkae chini mzungumze vinginevyo wala hamfiki kokote kwasababu kwenye maofisi kuna changamoto nyingi sana.

Kingine epuka kuwa na mahusiano ya karibu na bosi wako ilihali mpenzio naye anafanya kazi hapo, itamfanya ajisikie vibaya kwani atakuwa anahisi moja kwamoja bosi anatumia cheo chake kukurubuni na mwisho wa siku mmoja wenu ataona kazi chungu na atajikuta hana kazi bila sababu zozote za msingi.

Asanteni sana, wala sijamlenga mtu msinirushie mawe mtoto wa mwenzenu au kama vipi CHOMA GANZI

www.jescatarimo.blogspot.com

Friday, September 21, 2012

Mwanaume kutokuwa Smart nini shida?

Nitakushangaa sana wewe mwanamke unamuona mumeo anaondoka lakini kavaa nguo ya ajabu.

Hivi kweli kabisa kwa moyo mweupe bila hata kutikisika mumeo anatoka nyumbani anaenda kazini shati limejikunja halijanyooka vizuri, au chafu halijafuliwa au ndo kalirudia la jana tena linanuka jasho ukimuangalia miguuni viatu vichafu tena mwingine hata nywele hajachana mindevu imekaa tu ovyo?!!

Unajisikiaje unapopita barabarani ukiwaona wanaume wengine wako smart halafu mumeo ndo vile?? Tena wengine wanavaa hadi mashati yaliyochanika au soksi zilizotoboka, we hauoni kama unajiaibisha wewe?

Hakikisha havai soksi iliyotoboka wa kutoa harufu!

Kumbuka yeye ni mwanaume hana shida yeye kichwa chake kinawaza wapi apate pesa familia ikae vizuri kwa hiyo usipomwangalia anaweza kwenda kazini hata na kaptula, jukumu la mavazi ni lako wewe mwanamke hata kama na wewe unamajukumu ya watoto ila kumbuka mume ndo mtoto mkubwa naye anapaswa kuangaliwa kama hao wadogo kabla hajaondoka mtupie jicho mumeo, sio umchunguze?la hasha muangalie tu nguo alizovaa je ni zile ulizompangia avae?? kama siyo zinaendana?hazina kasoro? Manake wewe ndo utakuwa unazijua nguo zake kuliko hata yeye mwenyewe, usikubali mumeo atoke ndani kavaa shati la njano, tai ya blue, suruali ya kijani viatu vya brown. Soksi zinanuka hatari. Huoni aibu wewe?? Hakikisha soksi za mumeo ziko katika mpangilio na hazijatoboka manake wao wakiona soksi wanavaa tu hata kama zimetoboka au chafu wao hawajali tena na kama ziko tofauti anavaa hivyohivyo hawana muda wa kuangalia soksi nyingine iko wapi, na  kama mume wako muwazi atakwambia "uwe unaniandalia nguo"! sasa hili ni tusi kwa mwanamke, haupaswi kukumbushwa majukumu yako, japo kuna wanaume wengine wanakujipenda, yeye hata usipomchagulia nguo atajing'arisha mwenyewe.
Mwanaume akiwa smart anavutia!

Hivi hujisikii raha watu wakimsifia mumeo alivyosmart? hujisikii raha hata kumtambulisha kwa mtu 'jamani huyu ndo mume wangu'

Wengi mtasema mnaogopa kuibiwa, asikwambie mtu mwanaume hapendewi mavazi kwahiyo watu wakiamua kukuibia watakuibia tu!

Hili ndo langu la Ijumaa, najua sana kuna watu litakuwa limewauma kama ni mmoja wao CHOMA GANZI!
Kama siyo basi freshh! Endelea kuvisit www.jescatarimo.blogspot.com

Ijumaa njema

Thursday, September 20, 2012

Unapiga kelele wakati wa tendo?Soma hapa

Hili najua litakuwa linatugusa wengi!

Utamu bwana nikitu kingine asikwambie mtu, pata picha unawashwa sehemu yoyote ile kwenye mwili wako mfano mkononi halafu unakucha kidogo ndefu jinsi unavyojikuna unaonaje raha yake? Tena hapo ukute muwasho ndo umekushika balaa, dah yani kama nakuona unavyojikuna huku unafumba macho assshhhh! Unasikia raha eenh?? Haya sasa nadhani hapo mtanielewa kitu nitakachokiongelea hapa

Kila mtu anajinsi anavyoreact anapojisikia furaha, hasira, wivu, uchungu na hata utamu, sasa mimi naongelea utamu wetu uleeee! Unakunwa na mtu hadi unajihisi uko dunia nyingine unajikuta bila kutegemea unatoa kelele tena mwingine hadi kulia kabisa, mwingine yeye wala hatoi sauti atafumba zake macho tu huku anausikilizia utamu.

Sasa kama unajijua wewe ni wa kupiga kelele tena zile za sauti kubwa basi ni vizuri ukafungulia redio na kama ikiwezekana hakikisha wakati unataka mautamu nyumba haina watu haswa watoto.
Najua wengi mtasema hili haliwezekani kama haiwezekani basi wakati mnaendelea na utamu vuta shuka au mto kuwa kama unaung'ata huo mto au hilo shuka, kidogo itasaidia sauti isisikike nje. Pia kama mtakuwa katika pozi ambalo midomo yenu inaweza kukutana wakati utamu unaendelea ni vizuri mpenzio au mzinzi mwenzio akawa anakunyonya ulimi basi hapo sauti itaishilia mdomoni mwake na pia itazidi kuongeza msisimko kwake!

Ila maswala ya USWAZI chumba kimoja wewe kinachofuata mpangaji mwingine halafu huna hata kiredio au umeme ndo umekatika mnapiga gemu sauti wanazisikia wao sio vizuri unawaletea kero na mwisho wa siku mtajikuta mnapigwa chabo!

Umelipata ndugu yangu? milio kwenye sita kwa sita ina raha yake. Pale unapojisikia utamu jiachie tu!! Muache mwenzio ajue anakupagawisha kiasi gani!!!

Hilo ndo langu la leo.

Limekuuma?? Kama kawa CHOMA.......................???

Wednesday, September 19, 2012

Utambulisho

Hii ni kwa watu wote, watu wengi sana wanapenda kutambulishwa na wapenzi wao kwa watu wao wa karibu au marafiki zao pindi wakutanapo nao.

Hujisikia sana kupendwa pindi umtambulishapo kwa watu wako, mfano;mmetoka mmeenda sehemu kukaa kwa chakula au drinks mara wakatokea marafiki au ndugu mkawa mnajumuika nao kitendo cha wewe kuwaambia watu wako jamani huyu mpenzi wangu(tena wengi hupenda kuitwa mke/mume hata kama hawajaoana) huwa anajisikia raha sana na utaona tu jinsi atakavyoongeza mapenzi.

Ila kuna utambulisho mwingine unaweza kumfanya akajisikia vibaya mfano, unamtambulisha jamani huyu anaitwa fulani(unataja jina lake) halafu unamwambia na yeye hawa ndugu zangu au marafiki zangu, hapo lazima atajisikia vibaya ataona kwamba wewe kumbe huna future naye yoyote na wala humpendi ataanza kufikiria upo naye kwaajili ya ngono tu au unaona aibu kumtambulisha kwa vile labda anakuaibisha yeye mbaya au kavaa vibaya...Ni wengi sana huwa na mawazo haya japo huwa si kweli. Sasa kwa ushauri tu kama mpenzi wako si muelewa bora tu usimtambulishe waache wasalimiane basi! ila kama mpenzi wako muelewa basi we mtambulishe tu kwa jina au kama rafiki sababu najua kuna sababu za wewe kutomtambulisha kama mpenzi kutokana na kwamba labda bado hujaamua kuweka wazi au bado hamjajuana sana na sababu nyingine nyingi.

Nakuja kwa wewe ambaye unataka kutambulishwa ni vizuri ukawa muelewa sababu ukijifanya kuchukia kisa hujatambullishwa mwenzako atakushangaa kwanini unataka kurush vitu na hapo utajikuta unaharibu mambo.

Ila kama kweli unampenda mpenzi wako na hakuna unachomficha kwanini usimtambulishe kwa watu wako wa karibu? Atajisikia raha sana na atazidi kukupenda na atazidi kuwa huru na wewe!

Hapo najua nimewagusa wanaume wengi kwasababu wao ndo wagumu wa kutambulisha, manake jana katambulisha mwingine, juzi mwingine na leo tena mwingine watu watamshangaa ndo maana huwa wanakuwa wagumu kweli

Kama vipi CHOMA GAAAAANZI!

Ahsante!

Monday, September 17, 2012

Simpendi huyu!

Nadhani ni mmoja ya watu ninao wachukia tena kazidi kunikera kwa kuwa aliyemtukana ni Kiba . Naombeni msome ujinga huu wa TID


TID


"ALLY KIBA NA MAMA YAKE WANAMAMBO YA

KIJINGA SANA"......HILI NI TUSI LA TID

Baada ya kukabiliwa na scandal kubwa ya
kupanga njama za kumuua Ali Kiba, Khalid
Mohamed aka Top in Dar, amezungumza na
kusema Ali Kiba na mama yake wamekosa la kufanya na anawaona wajinga wakubwa. Akizungumza kwenye kipindi cha Tagz Weekly
cha DTV, msanii huyo amesema huenda Ali Kiba
alienda kwa mganga ambaye alimwambia TID
anataka kumuua. Msanii huyo wa ‘Nyota Yangu’ aliongeza kuwa
kutokana na kusingiziwa kitu asichokijua, kamwe
haiwezi ikatokea siku atampigia tena simu Ali Kiba
Ali Kiba(left) & TID(right)
aliyekuwa mshikaji wake wa karibu. “Siwezi naogopa,” alisema. “Naweza kumpigia simu nikaambiwa sasa ndo natamtafuta kumuua, achana naye tu mwache yeye aendelee na vitu vyake, because I felt he and his family were up to it, mama yake namuona sana, najua mama yake hanijui hajawahi kuniona hata siku moja. Ali Kiba kwa kitu gani ambacho amefanya yeye mimi nimfanyie baya? Nipo na watu kibao pale nao wamejilist eti nataka kuwaua sasa mimi hela ngapi nitatoa kuwaua watu wote wale? For what purpose watu kibao wamejilist. Am not gonna tell you what reactions I’m gonna do, I’m keeping it to myself, I aint gonna talk about it, seriously they are stupid, yaani they should come up with the best concept.” Pia Top In Dar alisema ameshakutana na Diamond
ambaye amesema hata haelewi kinachoondelea
na hana tatizo naye.
Ali Kiba

Saturday, September 15, 2012

Kuna umuhimu wa kumtajia mpenzi watu waliokutongoza?

Japo si vizuri kufichana mambo wewe na mpenzi wako ila si kila kitu unatakiwa umwambie, kwasababu binadamu tumetofautiana kuna mwingine hana shida akijua watu ambao wameshakutongoza ila mwingine inakuwa kidogo shida japo hatosema, kwanza kwanini umwambie lazima ujifunze kuhandle vitu vidogo kama hivi

Kumbuka kwamba kutongoza siyo kosa wala usimchukie anayekutongoza kwasababu majibu unayo wewe kukubali au kukataa. Wewe ndo umebeba maamuzi yote ya kusema YES or NO.

Si vizuri kumwambia mpenzi wako kila mtu anayekutongoza haswa ambao atakuwa anafahamiana nao au marafiki zake kwasababu inamadhara yafuatayo
1. Kama mpenzi wako ana wivu sana basi mahusiano baina ya watu hao wawili au kama ni marafiki utavunjika

2. Unazidi kumjengea mazingira ya wivu mpenzi wako bila we mwenyewe kujijua

3. Unajikosesha uhuru wako bila kujijua kwasababu akishaona unafuatiliwa sana ataanza kuongozana na wewe kila mahali ambapo unataka uende, usipopokea simu itakuwa ugomvi au akikukuta upo na mtu yoyote hata pengine ni ndugu yako halafu yeye hamfahamu atahisi unatongozwa au unamahusiano naye kutokana na namba 2 hapo juu yani umeshamjengea wivu

4. Kwenye mikutano yake na marafiki zake utakuwa huendi kama zamani sababu atakuwa anaogopa kuibiwa

Madhara yapo mengi tu kuendana na mtu atakavyolichukulia hili swala, tena mwingine anaweza hata kukuacha manake atakuwa anajiuliza kwanini utongozwe wewe tu kila siku au ndo unajirahisisha kumbe mtoto wa watu wala.

Kama nilivyosema hapo juu watu tunatofautiana mwingine anapenda aambiwe ili tu ajue so ni vizuri kumsoma mpenzi wako ni wa aina gani sio tu unakurupuka unaanza kusema fulani na fulani wamenitongoza leo.

Ila kuna wale ving'ang'anizi wa kutongoza hata umkatalie vipi yeye bado yumo tu ukiona anakupanda kichwani bora tu umwambie mpenzio ili siku ya siku asije akashuhudia mwenyewe ikawa balaa!

Hilo ndo langu la leo lilionijia kichwani na upeo wangu unavyonituma, kama utakuwa na wazo lako tofauti basi tupia

Leo hakuna ganzi dawa zimeisha mahospitalini ila nadhani hakuna mtu limemuuma.
Basi pouwa!


Wednesday, September 12, 2012

Kisa cha kweli!

Kuna siku niliongelea wivu na madhara yake, sasa leo naongezea jambo ambalo nimeliona hivi karibuni, na hii ikiwa ni matokeo ya wivu.

Kuna dada mmoja alikuwa na wivu sana kwa mumewe alikuwa akihisi mumewe anawanawake zake wa nje, japo kwa upande mwingine ni kweli yule jamaa ana wanawake wengi tu ambao huwa anaburudika nao akishatoka kwa ofisi na wakati mwingine anachelewa hadi kurudi nyumbani, sasa hichi kitu kilikuwa kinamuumiza sana huyu dada(mke) . Japokuwa hakuna ushahidi wowote ule ila alikuwa tu akihisi mumewe anamchezea rafu.

Akajaribu kutumia njia ya marafiki wamchunguze ila kwa kuwa jamaa ni very smart hawakupata kitu walimpa tu jibu mumeo huwa anatoka na marafiki zake tu then anarudi home. Lakini yule dada(mke) bado hakutaka kuamini ndipo siku moja akamuamulia,

Ijumaa moja asubuhi jamaa akaaga kwenda kazini kama kawaida na akamwambia wife leo nitachelewa kidogo kurudi ila hakumpa sababu na wife nae akamwambia leo naenda kwenye kitchen party nami nitachelewa kurudi, basi mume akaondoka. Ilipofika mida ya saa 10 mke akachukua taxi bubu akaenda maeneo ya karibu na ofisi ya mumewe akapaki gari imefika saa 11 kasoro akamuona mumewe anatoka ofisini, wakaanza kumfuatilia hadi wakafika maeneo ya Uhuru park kinondoni. Mumewe akatafuta mahali akakaa baada ya muda wakaja marafiki zake mumewe wakaendelea kujumuika yeye(mke bado anamfuatilia hapo)
Hapo usiku umeingia, katika kuendelea kuchunguza mara akatokea mume wa shostito wake wakaanza kusalimiana huyo shemeji mtu akamwambia rafiki yako yupo ndani mango garden twende ukamsalimie na ukae japo kidogo, sasa kwavile hakutaka huyo shemeji ajue lolote ikabidi tu amdanganye kwamba kaja kuenjoy kidogo tu halafu anarudi home so ikabidi akubali, wakawa wanasubiri magari yapite waweze kuvuka barabara upande wa pili ili waingie mango. Kumbe huku mumewe kanyanyuka anataka kuondoka ndo mara anamuona wife yupo na jamaa wanavuka barabara na jamaa wala hamjui. Si ndo akaanza kuwafuata? Ile jamaa anataka kulipia kiingilio tu mume huyu hapa, kawaka kafura bila kuuliza kitu, ngumi zikarushwa na yule shemeji nae ili kujitetea akarusha ngumi basi pakawaka kweli! Baada ya kuamuliwa jamaa akaenda kuwasha gari yake hadi home, ikabidi mwanamke achukue ile taxi bubu aliyokuja nayo hadi home. Kwakuwa jamaa alikuwa keshafika akaiona ile gari ikiondoka so moja kwa moja akajua mkewe kaletwa na yule jamaa.

Kibaya zaidi mkewe alivyoondoka alibeba nguo za harusi kwa mawazo yake ni kuwa akiwa anarudi azivae mumewe aamini alitoka kwenye kitchen party, sasa ameingia ndani mumewe kumkagua begi lina nguo.

Sitaki kukwambia kilitokea nini ila baada ya kutengana kwa mwezi mmoja ndoa ikaja kusuluhishwa na familia zote mbili akiwepo yule shosti yake na mume wa shosti

Sasa isingekuwa kuchunguzana haya yangetokea????



Is It true??Hahahahaaaa