Friday, July 27, 2012

Haya sasa, damu ya Yanga


Mautundu yanahitajika

Ngoja niwape cha asubuhi

Usikarike eti kwasababu mumeo akipiga 1 ndo basi hasimamishi tena, wakati mwingine wewe ndo unaepaswa kuisimamisha mpe mautundu, gusa sehemu muhimu itasimama yenyewe..kumbuka MWANAUME NI MOTO WA MABUA nadhani mnayajua mabua yanashika moto haraka sana ukiwasha sasa mwanaume yeyote rijali ukimshika mahala pake lazima utaona taratibu kitu kinakuwa kigumu na lazima ujue sehemu ambazo zinaleta msisimko kwa mwanaume wako japo huwa hazitofautiani sana. Sasa nitakushangaa sana kama unalalamika eti mume wangu au mpenzi wangu anatumia mda mrefu kusimamisha, sasa atasimamisha vipi wakati humvutii?? mpe kuwa mjanja amka

heheheeeeee umelipata hilo shostisto!! Najua wanawake huwa hatupendi kuambiwa ukweli wengi watachukia hapa, tofauti na wanaume wengi wanapenda kujifunza, sasa uchukie usichukie mi ndo nisharopoka kuwa mtundu, utaibiwa bure!

Leo niko tayari nirushiane tu mawe

Hilo ndo langu la leo

Thursday, July 26, 2012

Sababu za mwanamke kutofurahia tendo la ndoa

Naongelea upande wa mwanamke

Ni wanawake wachache sana wanaofikia climax pia si wanawake wote wanaenjoy sex, sasa ulishajiuliza kwanini hauenjoy?? Kwa utafiti wangu kuna vitu nimegundua ndo mara nyingi hupelekea mwanamke asifurahie tendo hilo au asiridhike

1. Kama hajampenda mwenza wake, ni vigumu kufurahia tendo hili kama huyo unaefanya nae hujampenda au hata kumfeel kidogo. Kama mapenzi kwa mchumba wako yameisha usifikiri ukifanya nae mapenzi utafurahi, unajidanganya!! hakuna kitu hapo labda aridhike yeye tu

2. Kufanya mapenzi kwa malengo fulani, hata siku moja huezi kufurahia sex huku ukiwa na nia ya kufaidika na kitu fulani kutokana na hilo tendo kwasababu najua muda wote utakuwa unatamani huyo mwanaume amalize saa ngapi ili upate unachokitaka na hii inatokea kwa wasichana wanaojiuza(machangudoa) na pia hata kwa wale wenye mahusiano na vizito na mapedeshee  anafanya sex huku akijua atafaidika na nini na mara nyingi hawa wanakuwa hawana mwanaume mmoja

3. Mawazo, unafanya sex ukiwa na msongo wa mawazo. Hauwezi kuenjoy huku unawaza mtoto anaumwa au tatizo lolote tu linalokukabili pia kwa wanawake wenye mwanaume zaidi ya mmoja wanakuwa na hofu za kufumaniwa so akili yake haitakuwepo hapo kabisa na hivyo kusababisha upande mmoja tu kufurahia tendo

4. Kutoandaliwa, hili ni kosa ambalo wanaume wengi wanafanya, mwanamke ni lazima aandaliwe ili naye afurahi. Mwili wa mwanamke unahitaji taarifa kuweza kujua kitu gani kinakuja ili kuweza kulainisha viungo vya mwanamke na asiweze kuchubuka wakati wa tendo jua kwamba mwanamke akiwa mkavu lazima ataumia na hatoweza kufurahia tendo. ILA katika mzunguko wa mwanamke kuna siku ambazo sehemu zake nyeti huwa kavu sana hata kama mwanamke atakuwa na hamu sana, sasa ukiona hali hii ni vizuri mkatumia vilainishaji au mafuta maalum

5. Ugonjwa,  kuna baadhi ya magonjwa humfanya mwanamke asiwe na hamu kabisa na sex hapa ningependa kuwaachia madaktari zaidi, kama unajua huna tatizo lolote kati ya niliyoyataja hapo juu basi nenda kamuone daktari utakuwa unatatizo linngine, na hii pia hutokea nilishashuhudia rafiki yangu akiwa na hili tatizo kumbe alikuwa na tatizo dogo tu ambapo alitibiwa akapona sasa yuko freeeeeesh!

Kumbuka raha ya sex uipe nafasi yake bwana unatakiwa ujiachie mpeane mautundu yooooote. Binafsi hili tendo nalipenda sana coz huwa nazingatia hayo niliyoyasema hapo juu, kama limekukera kalale hili ndo langu la leo,

Kuhusu maswala ya kufika climax nitaeleza siku nyingine, mada ndo naipika bado haijaivaa

Monday, July 23, 2012

Bi harusi mtarajiwa huna haya!!!

Hii kitu inanisikitisha sana, najua ni wengi wanatamani kuolewa kiasi chakufanya hata wasijue maana yaa ndoa wala nini majukumu yao pindi watakapoingia,

Kuna dada mmoja ambaye yupo kwenye maandalizi ya mwanzo ya ndoa ila mambo anayoyafanya nina uhakika ndoa itamshinda na huyo mume atakuja mkimbia, anatabia ambazo msichana yoyote hapaswi kuwa nazo.
Kwanza ana asili ya umalaya miezi michache kabla ya ndoa na bado anaendelea kuchakachua halafu anajifanya anawivu sana kwa bwana'ke
Kingine hana ufikiri wa kike hajui majukumu yake, ukiwa kama msichana au mwanamke unaishi na mwanaume yoyote kwenye nyumba awe mchumba, awe baba au awe kaka lazima ujue jukumu la chakula na usafi ni lako wewe hata kama pesa hutoi wewe ni lazima uhakikishe nyumba ni safi na msafishaji mkuu ni wewe na si mwanaume, hata siku moja huwezi mwambia baba yako aoshe chombo au umuache mpenzi wako aoshe chombo halafu wewe umelala au unaangalia tv kitamaduni hii sio sahii wapo wanaume wengine wanapenda kuwasaidia wake zao kwa mapenzi tu labda ameona kazi zimekuzidi au unaumwa hii sio mbaya, pia jukumu la kujua leo ndani kitu gani kinapikwa ni wewe mwanamke sasa utakuta mijanawake mingine hadi inafika jioni imekaa tu inasubiri mwanaume wake ndo aseme kama ni viepe au nini kitaliwa usiku, sasa unataka ndoa wakati uchumba tu unakushinda...Na wengi wanaofanya hivi ni wale waliobahatika kupata kazi za kipato cha juu KAMA UNAJIONA UKO JUU SI UOLEWE NA KAZI YAKO BASI wewe mtoto wa kike usimpande kichwani mwanaume hata iweje jua yeye ndo kichwa cha hiyo familia mnayokwenda kuianzisha...Halafu huyu mtu alienigusa hadi nikamuongelea hapa ni mbinafsi sana eti hataki wakae na ndugu wa mwanaume anataka ahamishwe, sasa wewe kabla ya ndoa unaanza vituko hivyo ndani ya ndoa itakuwaje?? acha kumtesa mwanaume wa watu, kumbuka wako wengi wanatamani kuolewa sasa ukifanya mchezo UTAOLEWA KWA VYEI TU KILA KITU WENGINE WATAKUSAIDIA u hujui kama wengine wanatafutaga tu wanaume za watu.... nawewe mwanaume hebu amka bwana toa sauti basi ukikaa kimya huyo anaendeleza vituko lazima ajue uwepo wako katu usikubali kupandwa kichwani.

Tafadhali usirushe jiwe nataka kukusaidia tu!


Friday, July 20, 2012

KICHEKO



Jamani hii sasa kali

                                               KUTOKA GLOBAL PUBLISHERS

Mpenzi wako akiwa hivi kimbia!

Kama mpenzi wako atakuwa na tabia hii nitakayoielezea kimbia,
Kama mpenzi wako anaweza kukaa muda mrefu bila kuwasiliana na wewe kwa njia yoyote ile na wala hayupo mbali, chapa lapa.....kwani najua lazima akikutafuta atakwambia dear nimekumiss kweli njoo home basi, na ukienda shughuli ni moja tu kungonoka(sex) baada ya hapo subiri wiki ipite au wiki mbili anakutafuta tena . We hujiulizi hayo ndo mapenzi gani?? kwani wewe umekuwa mashine kila akiwa na nyege ndo akutafute?? Najua hii imetutokea wengi kutokana na mapenzi tulionayo kwa hao wapenzi wetu, sasa wenyewe ndo wanatufanya kama wajinga, ukiona hali ndo hii basi chapa lapa. Usikubali mtu akutumie namna hii.

Watu hawa hawakufai

Kuna watu leo napenda niwaongelee

Naanza na marafiki,
Muda mwingine huwa nakaa nafikiri ila nashindwa kuelewa, kuna baadhi ya watu sijui wameumbwaje yuko radhi akununulie kreti mbili za pombe kuliko kukukopesha wewe kiasi cha pesa kidogo tu ili uongezee ulipe ada ya mtoto tena hapo unamwambia unamlipa mwisho wa mwezi, sasa hapo sijui mtu wa namna hii tumuweke kwenye kundi gani mchoyo, au mbinafsi, mnafiki asiependa maendeleo yako au sijui tumpe jina gani. Nadhani ni vizuri kujitenga na marafiki wa namna hii kwasababu utakuwa unajitafutia aibu na fedheha kwa familia, ndugu, majirani na marafiki wengine kwasababu watakuona kila siku unalewa lakini mtoto akisedai ada unasema huna unadhani hapa utaeleweka wakati kila siku unarudi umelewa?? kumbe maskini wa Mungu pombe unapewa na rafiki yako ambaye kukusaidia hataki ila anataka kukunywesha tu pombe ilimtadi tu ajifurahishe kwa kampani yako, kwahiyo ndugu yangu uwe makini na marafiki wa aina hii

Nakuja kwa wapenzi:
Hapa ni pande zote wanaume na wanawake kwani wanawake wengi siku hizi wanauwezo wa kuwazidi wapenzi wao
Sasa utashangaa mpenzi wako mnakula nae bata sana viwanja vyote mnazunguka, mtalala hotel za bei ghali na hapo utakuta anajua kabisa shida ulizonazo labda una ndugu yako mgonjwa au shida nyingine yoyote tu lakini hakupi senti 5 japo na wewe umalize tatizo ulilonalo. Yeye anachojua ni starehe tu, utashangaa anakupigia sasa dear, nakupitia hapo tukakae sehemu tujivinjari yani hana muda wa kujua ratiba zako hana muda wa kujua maendeleo yako ndugu yangu huyu mtu hakufai kimbia.

Thursday, July 19, 2012

Pochi ya mdada inatakiwa iwe na nini??

Naomba niwaambie kinadada  vitu muhimu vya kuweka kwenye mapochi kwa shughuli za kawaida,

Kwenye pochi yako hakikisha una pedi kipande kimoja kwaajili ya emergency pia ukiweza beba na chupi especial kama ndani utakuwa umevaa vile vichupi vyetu(bikini), kuwa na kipande cha kanga au mtandio kama utaona kanga ni nzito sana, uwe na pini ndogo hii ni kwaajili ya kushikiza shati lako kama kifungo kitakatika na kudondoka bila wewe kujua pia sindano na uzi endapo nguo itachanika au zipu ikiharibika, leso au handkerchief kwaajili ya jasho endapo utapata mzururo wa ghafla...hivi vitu ni muhimu sana kubeba utakuwa ujinga unabeba pochi kuuuuuubwa halafu hivi vitu havipo....

Pochi kutoka Qila Qi2 Fashions ukihitaji  piga  0718065194
Kwa mitoko ya jioni hivi vitu si lazima sana labda pedi tu endapo utaona haupo siku nzuri hapo najua viwallet vinahusika zikiwa zimejaa make up tu!

Aibu gani hii

Kabla hujatoka jiangalie bana nguo gani unavaa yani nguo nyingine unajua kabisa imeisha lakini mzee umo tu dah unataka hadi iongee?? pia kama nguo haikutoshi na inakubana sana usiivae bila hivyo utaaibika kama huu shosti

Mishemishe za jana

Nikiwa katika hekaheka za kutafuta pa kupata lunch nikaona hivi
Mnaona hayo mafuta yalivyo meusii?? angalia kalai la kushoto dah!


Wenye haya magari ndo wameenda hapo mlipoona hayo makalai juu hapo, kwenda kupata lunch!

Nikafunga ofisi tayari kwa kurudi home
Huyu mtoto mzuri jamani muweke kwenye screen saver na wewe!
Qila Qi2 fashions/Ivy Shop Kigamboni

Baada ya kazi nikapita Ivy shop aka Qila Qi2 fashions nikakuta pochi za ukweli


Hii pochi ilinivutia ina rangi zilizotulia halafu unaweza kumatch na nguo ya rangi yoyote


Walet za kike zilikuwepo za rangi mbalimbali halafu bei yake ndogo sana nitafute nikupe direction za duka


Hii ni wallet ya kiume lol


Kwa ndani inavyoonekana

Jamani hii wallet imenimaliza zipo pia za njano, red, pink na green
sasa nimefika home napiga mahesabu ya matumizi  lakini hainipi kabisa dah hali ngumu










Nilianza kujaribu viwalo nilivyobeba jana

Hapo je??

Hii top niliipenda sana ni nzuri kwa jumapili mchana hivi au jumamosi zipo rangi mbalimbali pale Qila qi2 fashions
Then nikaenda kuoga, nikala msosi dah jana dada alipika wali nazi na samaki pembeni kuna parachichi mweh nilijilambaje?? baada ya hapo nikapiga mbonji

Salamu za pole





Seagul ikiwa inazama



Napenda kuwapa pole Wazanzibar na Watanzania wote kwa ujumla kwa msiba kubwa uliotokea jana kutokana na ajali ya meli ya Seagul, MUNGU AZILAZE ROHO ZA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI na awajalie afya na uzima majeruhi wote

Wednesday, July 18, 2012

Mtu mwenye lips kubwa duniani!


Christine







 Jina kamili ni Christina Rey , ana umri wa miaka 22 mwenye asili ya Russia.
Kwa mara ya kwanza amevunja rekodi kwa kuandikwa kwenye kitabu cha World's Guiness Record kwenye category ya  " THE WORLD'S LARGEST LIPS"

Add caption
Akiwa na mpenzi wake
Hapa katika harakati za kukuza tobo la sikio
sikio lake kama linavyoonekana baada ya operation
Alichoma sindano kwa mara ya kwanza ya kuongeza lips akiwa na umri wa miaka 17 tu na jumla ilimgharibu paundi 4000 ambayo kwa haraka haraka ni zaidi ya milioni nane za kitanzania lakini Christine haishii hapo bado anaendelea na majaribio kwenye mwili wake, ambapo amefanya upasuaji kuyafanya masikio yake yawe na muonekano kama ule ma'elves' tunayoona kwenye movie...pia amejitoboa sehemu mbalimbali na kuchora tatoo sehemu mbalimbali...kama nilivyosema haishii hapo anamatarajio ya kuongeza matiti yake yawe na size kubwa kabisa..
Sehemu ya kichwa ikiwa imechorwa tatoo

Hayo ndo maajabu ya dunia wewe unatafuta umaarufu kwa njia gani??

Meno yake aliyoyachonga
Ulimi ukiwa umekatwa

Pedeshee

Hawa ndo mapedeshee wa ukweli, cheki madini shingoni hayo,..wapi papaa msofe wapi pedeshee ndama mtoto wa ng'ombe na mapedeshee wooooote wa mjini

Kicheko


BEDROOM DEMOCRACY 
Young wife, who was becoming
 
frustrated with her young husbands constant demands for sex,
 
decides to make a schedule for him, to cut down on the
 
amount of times that they will have to make love for the
 
rest of their marriage.
 
While getting ready for work, she writes on a piece of paper, 
"Honey, you know I love you, but your never ending
 
 requests for sex are leaving me
 
drained and really tired. So I propose that we only have sex
 
on days that start with the letter 'T', to minimize
 
the frequency of our lovemaking sessions. Don't be mad
 
at me honey, just understand where I am coming from, and let me
 
know if my request is too demanding of you."
 
On her way out the door, she uses a
 
refrigerator magnet and sticks the note to the fridge door,
 
hoping that her sex craved husband will be understanding and
 
accepting of her proposal when he reads it.
 
  
Upon returning home, she glances at
 
the refrigerator and
 
 notices that her note has been replaced with a note from
 
her husband that reads, "Baby, I didn't'
 
realize that I was putting you under so much pressure and
 
I'm sorry.
 
  
I accept your proposal and have even
 
taken the extra step of listing at the bottom of this
 
letter, those days starting with the letter 'T' to
 
make sure that we are on the same
 page. 
  
 1. TUESDAY
 
  
 2. THURSDAY
 
  
 3. TODAY
 
  
 4. TOMORROW
 
  
 P.S. I love you too, and remember
 
it's still TODAY, I am waiting for you
 
upstairs."
 
    
Thank you.

Fashion


Mtoto wa kike vaa upendeze
Qila qi2 Fashions  call 0718065194

Qila qi2 Fashions  call 0718065194

Qila qi2 Fashions  call 0718065194

Qila qi2 Fashions  call 0718065194
                                                  "Yellow" rangi adimu hakikisha unakipata
Qila qi2 Fashions  call 0718065194

Qila qi2 Fashions  call 0718065194
Qila qi2 Fashions  call 0718065194
                                             Hata waname vyenu vipo
Qila qi2 Fashions  call 0718065194

Qila qi2 Fashions  call 0718065194

Qila qi2 Fashions  call 0718065194
                                               Hiki nitahakikisha namnunulia MR
Qila qi2 Fashions  call 0718065194

Qila qi2 Fashions  call 0718065194

Qila qi2 Fashions  call 0718065194

 Moja ya Duka la Qila Qi2 Fashions lipo Kigamboni pale ferry wengi wanalijua kama Ivy Shop fika pale upate vitu vizuri kwa bei rahisi kabisaaaaa! Lazima uwake banaaaaa

Tuesday, July 17, 2012

Acha kutembea na Shemeji yako



Ni kwanini unatembea na rafiki au ndugu wa mpenzi wako(shemeji yako)?? Yani umeshindwa kufanya umalaya wako woooote huko nje hadi uufanye kwa mtu wa karibu na mpenzio?? sasa nakwambia hii ni mbaya sana kwasababu ikigundulika aibu yake ni kubwa mno, na usifikiri huyo shemeji yako anakupenda saaana ila amekuona maharage ya mbeya na malaya wa kutupwa na ndio maana wala hajaona aibu kujiingiza kwenye mahusiano na wewe...na siku ikigundulika usifikiri wao watagomba na kuwa maadui bali watakuona wewe ndo unawachonganisha kutokana na umalaya wako na utaachwa kwenye mataa.

We kaka au dada jitahidi sana usiwajengee mazingira ya faragha mpenzi wako na rafiki/ndugu yako, la sivyo utakuja juta, nakueleza ukweli kila mtu ana mapungufu yake!! Simaanishi ndo wawe wanaogopana la hasha ila kuna yale mazingira ya faragha, kwani we huna wivu bwanaaa sasa inakuwaje hapo??

Na kuna mijitu mingine imebobea kwa kutembea na shemeji zao utakuta umeenda tu chumbani umewaacha sebuleni tayari mtu anaanza kutia sumu mara "ooh shemeji unajua we waukweli sana" au "shem we mi nakukubali sana yani natamani ningekuwa na mtu kama wewe" basi ataanza kummwagia misifa paleeee na kama mwanamke nae mdhaifu basi mwenye mali hana chake watakuwa wanamvizia kila akitoka huku nyuma wao wanakiss au wanachezeana mradi laana tu....na we utagundua mazingira ya ajabuajabu kila ukirudi utashangaa kama walikuwa wanaongea basi watanyamaza halafu kama kunakuwa na ukimya na kujibaraguza flani hivi!

ACHA TABIA MBAYA TAFUTA WA KWAKO!