Kuna watu leo napenda niwaongelee
Naanza na marafiki,
Muda mwingine huwa nakaa nafikiri ila nashindwa kuelewa, kuna baadhi ya watu sijui wameumbwaje yuko radhi akununulie kreti mbili za pombe kuliko kukukopesha wewe kiasi cha pesa kidogo tu ili uongezee ulipe ada ya mtoto tena hapo unamwambia unamlipa mwisho wa mwezi, sasa hapo sijui mtu wa namna hii tumuweke kwenye kundi gani mchoyo, au mbinafsi, mnafiki asiependa maendeleo yako au sijui tumpe jina gani. Nadhani ni vizuri kujitenga na marafiki wa namna hii kwasababu utakuwa unajitafutia aibu na fedheha kwa familia, ndugu, majirani na marafiki wengine kwasababu watakuona kila siku unalewa lakini mtoto akisedai ada unasema huna unadhani hapa utaeleweka wakati kila siku unarudi umelewa?? kumbe maskini wa Mungu pombe unapewa na rafiki yako ambaye kukusaidia hataki ila anataka kukunywesha tu pombe ilimtadi tu ajifurahishe kwa kampani yako, kwahiyo ndugu yangu uwe makini na marafiki wa aina hii
Nakuja kwa wapenzi:
Hapa ni pande zote wanaume na wanawake kwani wanawake wengi siku hizi wanauwezo wa kuwazidi wapenzi wao
Sasa utashangaa mpenzi wako mnakula nae bata sana viwanja vyote mnazunguka, mtalala hotel za bei ghali na hapo utakuta anajua kabisa shida ulizonazo labda una ndugu yako mgonjwa au shida nyingine yoyote tu lakini hakupi senti 5 japo na wewe umalize tatizo ulilonalo. Yeye anachojua ni starehe tu, utashangaa anakupigia sasa dear, nakupitia hapo tukakae sehemu tujivinjari yani hana muda wa kujua ratiba zako hana muda wa kujua maendeleo yako ndugu yangu huyu mtu hakufai kimbia.
No comments:
Post a Comment