Tuesday, July 17, 2012

Njia nzuri ya kuachana na mpenzi wako

Habari zenu wapendwa??

Jana usiku nilikuwa naongea na mtu kwenye simu nikajikuta naikumbuka hii mada ambayo kwa muda mrefu nilitamani kushare na watu wengine. Kuna baadhi ya watu hawajui njia sahihi ya kuachana na wapenzi wao pindi wanaposhindwana.

Mmeshindwana??
Jiulize, umefikia mahali ambapo unaona hauna mapenzi kabisa na hauwezi kabisa kuendelea na huyo uliyenae? Najua wengi huwa hawajui jinsi ya kuachana na huyo mtu sanasana wengi wanajifanya kupotezea na kujifanya wako busy halafu ghafla anakata mawasiliano. Sasa hii si njia nzuri sababu kama huyo mpenzi wako ni king'ang'anizi basi jua atakusumbua sana na hata ukiwa na mpenzi mpya ataendelea kukusumbua au atakujengea chuki na uadui wa hali ya juu.

Pia kuna watu wanatabia chafu sana ambayo mimi binafsi siipendi ya kukutafutia visababu tu, mwingine anakuwekea mitego kwa marafiki zake ili wakutongoze/uwatongoze then akufumanie aisee mimi ukinifanyia hivi rafiki yako nitatembea nae na kukuacha nakuacha tena kwa KISHINDO, mwingine mnaweza kwenda out halafu mara utashangaa kakuacha kiajabu ajabu tu akaondoka bila wewe kujua au akakutafutia kisababu tu akajifanya amekasirika halafu anaondoka anakuacha wewe peke yako, sasa wewe mtu( esp. wanaume) unamuacha huyo msichana hapo baa au club au hotel unajua atarudije nyumbani? tena ukute hakubeba hata senti mtoto wa watu, akipatwa na matatizo mfano avamiwe na vibaka wambake au wamuue jua wewe utakuwa hatiani kwasababu ndiye mtu wa mwisho kuwa nae.



Jitahidi asikufumanie
Sioni umuhimu wa kuachana na mtu halafu mkawa maadui, chakufanya  we mtoe out jioni au mkae sehemu yoyote iliyotulia mueleze hisia zako zilivyokuwa kwake hisia zako kwa sasa na kwanini unataka muachane jaribu kutomcrash saaaana ili asije kujisikia vibaya sana pia usisahau kumpa sifa zake na umuombe msamaha kwa kitu ambacho unafanya(kuachana nae) muombe kuendelea kujuliana hali kila inapobidi pia mshirikiane pale mnapokuwa na matatizo mbalimbali( japo najua hamtokuja kufanya hivyo) pia epuka fumanizi kabla ya hamjaachana, haitakujengea picha nzuri endapo mtaachana eti sababu amekukuta na mtu mwingine unajiharibia CV ndugu yangu...kwa kufanya hivi basi jua kwamba utakuwa umejipunguzia mzigo na nina uhakika ukimaliza hapo utajiona mwepesiiiiiii ila kama utashindwa kumface basi unaweza mpigia simu au kuchat nae kwa sms.... nadhani kwa mtu muelewa anaeachwa hili ni jambo la busara sana kwasababu mi naona ni BORA KUAMBIWA UKWELI MMOJA UNAOUMIZA KULIKO KUFANYIWA VITENDO MIAMOJA VINAVYOUMIZA, Hivyo basi na wewe unaeachwa jaribu kuwa muelewa na kumbuka kuwa MAPENZI HAYALAZIMISHWI so we muachaji usimfanyie vituko mwenzako we mtiririkie tu na wewe unaeacha jaribu kumuelewa mwenzako banah si utapata mwingine? heshimu maamuzi yake bwanaaaa acha kuwa king'ang'anizi!

HII HAIWAHUSU WALIO KWENYE NDOA!

5 comments:

  1. thats nice advice GT bt mmmmmmh i'll try to follow yo advice, n c f it wll work.

    GOD HELP ME

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ila ni lazima uwe na uhakika kuwa hauhitaji kuwa na huyo mtu tena

      Delete
  2. no comment...!!!!!!!!!

    ReplyDelete
    Replies
    1. weeeee! demu wa kibongo usijaribu atakuroga, kuolewa ajira, baba heee.usithubutu bana, au km unajua hajakupenda,kwani huja wahi kuachwa!

      Delete