Jesca |
Asalaam aleykuum!( kama nimekosea mnisamehe), habari zenu wapendwa... nina kila imani mmemealiza week end salama basi hatuna budi kumshukuru Mungu wetu.
Wale ndugu zangu waislam mmejiandaaje na mwezi huu?? nini mikakati yako??
Mi nadhani kabla hujaanza kufunga kaa chini na kutafakari mwenendo mzima wa maisha yako kumbuka uliyoyatenda hapo nyuma je mema mangapi umetenda?? mabaya mangapi umetenda?? je uzito upoje kati ya mema na mabaya? Pia tafakari ni mabaya yako mangapi yamewachukiza watu wanaokuzunguka?? Sasa jiulize lengo la wewe kufunga ni nini?? na nini matarajio yako baada ya mfungo kuisha?? kuendelea na yale uliokuwa unayafanya kabla ya mfungo au kuanza ukurasa mpya? Basi ukishajiuliza haya maswali nadhani utakuwa unanielewa nini nataka niongelee hapa chini
Kuna watu huwa wananshangaza sana yani baada ya kumaliza mfungo tu anasa na ufuska mwanzo mwisho.. kama huamini subiri uone siku Idd gesti zote zimejaa japo simaanishi wanaojaza wote ni waislam, wapo wengine ambao wanaitumia vizuri sana na familia zao.
Ni mimi huyo jamani |
Hili ndilo langu la leo... Nawatakia kila la kheri ndugu zangu wooooote wa kiislam, mnikaribishe futari baibui ninalo!!
No comments:
Post a Comment