Hii kitu inanisikitisha sana, najua ni wengi wanatamani kuolewa kiasi chakufanya hata wasijue maana yaa ndoa wala nini majukumu yao pindi watakapoingia,
Kuna dada mmoja ambaye yupo kwenye maandalizi ya mwanzo ya ndoa ila mambo anayoyafanya nina uhakika ndoa itamshinda na huyo mume atakuja mkimbia, anatabia ambazo msichana yoyote hapaswi kuwa nazo.
Kwanza ana asili ya umalaya miezi michache kabla ya ndoa na bado anaendelea kuchakachua halafu anajifanya anawivu sana kwa bwana'ke
Kingine hana ufikiri wa kike hajui majukumu yake, ukiwa kama msichana au mwanamke unaishi na mwanaume yoyote kwenye nyumba awe mchumba, awe baba au awe kaka lazima ujue jukumu la chakula na usafi ni lako wewe hata kama pesa hutoi wewe ni lazima uhakikishe nyumba ni safi na msafishaji mkuu ni wewe na si mwanaume, hata siku moja huwezi mwambia baba yako aoshe chombo au umuache mpenzi wako aoshe chombo halafu wewe umelala au unaangalia tv kitamaduni hii sio sahii wapo wanaume wengine wanapenda kuwasaidia wake zao kwa mapenzi tu labda ameona kazi zimekuzidi au unaumwa hii sio mbaya, pia jukumu la kujua leo ndani kitu gani kinapikwa ni wewe mwanamke sasa utakuta mijanawake mingine hadi inafika jioni imekaa tu inasubiri mwanaume wake ndo aseme kama ni viepe au nini kitaliwa usiku, sasa unataka ndoa wakati uchumba tu unakushinda...Na wengi wanaofanya hivi ni wale waliobahatika kupata kazi za kipato cha juu KAMA UNAJIONA UKO JUU SI UOLEWE NA KAZI YAKO BASI wewe mtoto wa kike usimpande kichwani mwanaume hata iweje jua yeye ndo kichwa cha hiyo familia mnayokwenda kuianzisha...Halafu huyu mtu alienigusa hadi nikamuongelea hapa ni mbinafsi sana eti hataki wakae na ndugu wa mwanaume anataka ahamishwe, sasa wewe kabla ya ndoa unaanza vituko hivyo ndani ya ndoa itakuwaje?? acha kumtesa mwanaume wa watu, kumbuka wako wengi wanatamani kuolewa sasa ukifanya mchezo UTAOLEWA KWA VYEI TU KILA KITU WENGINE WATAKUSAIDIA u hujui kama wengine wanatafutaga tu wanaume za watu.... nawewe mwanaume hebu amka bwana toa sauti basi ukikaa kimya huyo anaendeleza vituko lazima ajue uwepo wako katu usikubali kupandwa kichwani.
Tafadhali usirushe jiwe nataka kukusaidia tu!
huyo mwanaume ndo mwenye makosa mwanamke kabla ya ndoa lazima uwe umeridhika na tabia na matendo ya mwenza wako. sasa huyo hajitambui
ReplyDeleteyaani kama umeniona mimi, tabia haina dawa,mchumba tuu aanze na ameanza kweli
ReplyDeletePole sana nadhani, jaribu kumueleza jinsi ambavyo tabia zake zinakukera ikishindikana basi achana naye coz huwezi kuwa na furaha, na ndoa isiyo na furaha si ndoa
Delete